Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20180117-WA0008.jpg
 
SAMAKI
Mto ule ule ambao Petro na wenzake walihangaika usiku kucha kuvua bila kupata samaki, ndiyo katika mto huo huo, walivua Samaki wengi asubuhi yake walipokuwa wamekutwa na Yesu.

Swala kubwa hapa ni kwamba, Yesu alipowakuta akina Petro pale mtoni asubuhi ile aliwaambia “Mna samaki?”. Wakajibu "Hapana”. Baada ya hapo Yesu, hakusema wabadilishe waende kwenye mto mwingine kuvua samaki, bali aliwaambia watupe nyavu zao kwenye kina kikubwa cha mto ule ule ili wapate samaki.

Yawezekana katika mwaka 2017 umejaribu sana kuvua samaki lakini hujapata kitu, hukupata kazi, hukupata mchumba, hukuwa na kipato kizuri, hukupata watoto, hukuwa na Amani, mwaka ulijaa magomvi, vita na chuki, hukuwa na mafaniko yoyote uliyotegemea. Ndugu, unapoona maisha hayendi kama ulivyotarajia, huo si wakati wa kubadili mto ili kupata samaki, sio wakati wa kutafuta kazi ingine, au kuhamia kanisa lingine, au kubadili mwenza wako (mke au mume) na kwenda kwa mwingine, La..

Kikubwa ni kutupa nyavu zako kwenye kina kirefu cha mto 2018. Yaani kuongeza imani yako kwa Mungu, ongeza urafiki wako na Yesu, ukiamini kuwa Mungu atakupa yote, atakuponya, atakuongezea tumaini, atakupa kazi mpya, atakupa mahusiano mapya na atakupa Baraka na kukubariki katika kila jambo, Omba, Sali, Amini, utapata.

Mungu akupe Baraka ili uweze kurusha vyavu zako kwenye Kina kirevu cha Imani kwa Mungu, ili mwaka 2018 uvue samaki wengi Zaidi.
 
Amen
 
Maono ambayo hayajaandikwa SI Maono
Malengo ambayo hayajaandikwcfa SI Malengo
Mipango ambayo haijaandikwa SI Mipango.
Bwana akanijibu, akasema, IANDIKE njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili AISOMAYE apate kuisoma kama maji.
*Habakuki 2:2*
Hahahaaaaaaaaa
 
NGUZO YA SIKU
ISAYA 40:29
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
HALELUYA mwana WA Mungu Mungu wetu ni mwema kila wakati anatutetea kila wakati haijalishi unapitia nini umezimia wapi Bali yeye anakupa nguvu upya
Haijalishi magonjwa yamekutafuna lakini ukimuangalia yeye anakupa nguvu mpya hebu tumuangalie Yesu tumnyenyeke na tuwe muaminifu kwake naye atatenda
Inua Jina lake na wewe utainuliawa kupitia ilo Jina kuu
MITHALI 24:16
Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka Tena
Waoooo haijalishi kuanguka kwako ni mara ngapi ila utarejea Tena mana Jina ulilo nalo ni jina kuu linaweza linatosha linaheshimika likisema yes hamna anaeweza kubadili muhimu KUSIMAMA IMARA KATIKA HILO JINA
MBARIKIWE SANA
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom