Makapuku Forum

Makapuku Forum

Nimezaliwa jana binamu asante sana ubarikiwe.

....oh, basi ihesabu kama belated borndate wishes. Mwaka mpya umeuanza mapema.

Sijui kwanini nakuwaga wa mwisho kujua, inauma sana kuchelewa kujua yaani hata anko hakunistua nikuletee zawadi maana korosho hazidanganyi

Anko Lyon Lee inabidi utubu
 
....oh, basi ihesabu kama belated borndate wishes. Mwaka mpya umeuanza mapema.

Sijui kwanini nakuwaga wa mwisho kujua, inauma sana kuchelewa kujua yaani hata anko hakunistua nikuletee zawadi maana korosho hazidanganyi

Anko Lyon Lee inabidi utubu
Ankooòoooooo
 
TUOMBE:

Bwana Yesu asante kwa ljumaa njema ya leo. 29 DESEMBA 2017

Baba hata kufika tarehe hii ya leo ni kwa neema,Mungu wetu tupe kumalizia mwaka huu salama huku tukikuangalia wewe mfalme wa Amani.

Asante kwa ulinzi wako kwetu Mungu Mkuu

Umetulinda
Bwana wa majeshi

Ni wengi walitamani kuiona hii siku lakini hawakuweza kufika.

Baba siku ya leo ni siku ambayo wengi Tunakuwa ktk maombi

Mungu ninakuomba katika Jina la Yesu Kristo Maombi yetu Bwana yakawe ni manukato mazuri mbele zako.

Kumbuka wenye shida mbali mbali
Taabu na mateso ya kila aina EeeMungu ukawakumbuke

Angalia ndoa/familia ambazo hazina amani wala furaha

Mungu warudishie upendo wao wa kwanza

Ambao hawajakujua wewe Mungu wa kweli katika jina la Yesu Kristo Bwana ukawaokoe.

Kumbuka wamama wanaohitaji Watoto
Bwana ukafungue matumbo yao.

Na wale wajawazito wawe salama pamoja na uhai uliowakabidhi wautunze na kuuleta duniani..wape kujifungua salama.

Waangalia Wanafunzi, wagonjwa ,Yatima na wajane
Wakumbuke BWANA Yesu

Nimeomba haya nikiamini,NA nashukuru maana utatenda sawa na mapenzi yako katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareth

AMEN

IJUMAA NJEMA..MBARIKIWE
 
tenor.gif
 

Muziki: Kufungia Mwaka


Nikutakie wikend njema ya mwisho wa mwaka 2017. Sina hakika kama nitakuwa nimejiwahisha sana nikikutakia mwisho mwema wa 2017. Kapuku wewe, na unajijua kuwa muda wote tangu tumekutana humu mwanzo wa 2017, umekuwa ni ntu makini, mwelewa, mcheshi, mkali, mpuuzi, unayejali, mwenye utayari wa kusaidia na kuongea kilichoko moyoni mwako. Hata mimi nimekuwa hivyo hivyo maana nami kama wewe ni binadamu asiyekamilika.

Natamani kukuambia kitu ambacho unajua kabisa nimekuwa sichoki kukwambia kila mara. Wewe, yes wewe unayesoma aya hii, bila uwepo wako hapa Jukwaa hili lingebaki kuwa la kawaida sana, lakini kwa sababu wewe uko hapa na umeweka input za maana kulisongesha jukwaa hili, MF imekuwa ni jukwaa bora sana. Shukrani sana.

Binafsi nimejifunza mengi hapa, maarifa ya kutosha nimeyapata hapa. Tofauti zetu zimekuwa ni nguvu yetu, nakosa maneno mazuri ya kukwambia wewe mtu makini kabisa na umekuwa na nafasi ya kipekee katika maisha yangu.

Muziki sasa, leo ni maneno matupu, nitajitahidi kuchagua muziki nilioamini ulibamba vizuri hapa, ni kwa maoni yangu na Jumapili nitakukaribisha kuchagua wimbo wako uliokushika katika kipengele hiki, kwa hizi siku chache zilizobaki kumaliza mwaka. Wikend njema
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom