Muziki: Hesabu Saa, Miaka Itakuchosha
...ni muda umepita Kapuku mwenzangu na leo ni Jumamosi ya mwisho kwa mwaka 2017, kuna mengi ya kutakari siku hii ambayo naamini kabisa umejipumzisha. Bado likizo inaendelea kwa wengi wetu, eeeh, likizo naamaanisha ya kazi, shule na vitu kama hivyo maana kuna mambo mengine hayana likizo hata uwe mjanja mjanja namna gani. Ukiyapa likizo tu, imekula kwako. Utakuja unalia sisi unatukuta tunatoa machozi.
Muziki sasa, Jumamosi maneno kidogo tu na muziki unafuata. Video hizi zilibamba sana hapa kwenye kipengele cha muziki. Furahia leo ni wikend ya mwisho 2017