Muziki: Kufungia Mwaka
Nikutakie wikend njema ya mwisho wa mwaka 2017. Sina hakika kama nitakuwa nimejiwahisha sana nikikutakia mwisho mwema wa 2017. Kapuku wewe, na unajijua kuwa muda wote tangu tumekutana humu mwanzo wa 2017, umekuwa ni ntu makini, mwelewa, mcheshi, mkali, mpuuzi, unayejali, mwenye utayari wa kusaidia na kuongea kilichoko moyoni mwako. Hata mimi nimekuwa hivyo hivyo maana nami kama wewe ni binadamu asiyekamilika.
Natamani kukuambia kitu ambacho unajua kabisa nimekuwa sichoki kukwambia kila mara. Wewe, yes wewe unayesoma aya hii, bila uwepo wako hapa Jukwaa hili lingebaki kuwa la kawaida sana, lakini kwa sababu wewe uko hapa na umeweka input za maana kulisongesha jukwaa hili, MF imekuwa ni jukwaa bora sana. Shukrani sana.
Binafsi nimejifunza mengi hapa, maarifa ya kutosha nimeyapata hapa. Tofauti zetu zimekuwa ni nguvu yetu, nakosa maneno mazuri ya kukwambia wewe mtu makini kabisa na umekuwa na nafasi ya kipekee katika maisha yangu.
Muziki sasa, leo ni maneno matupu, nitajitahidi kuchagua muziki nilioamini ulibamba vizuri hapa, ni kwa maoni yangu na Jumapili nitakukaribisha kuchagua wimbo wako uliokushika katika kipengele hiki, kwa hizi siku chache zilizobaki kumaliza mwaka. Wikend njema