Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Heshimu Mazingira

...kiukweli leo naandika nikiwa na masikitiko makubwa, nilipaswa kuandika tangu juzi, so vumilia tu kusoma ninachoandika maana ndicho napenda. Masikitiko yangu ni kwa taifa kupoteza wanajeshi walinda amani kule Congo, inauma sana si kwa sababu tu rafiki yangu mzenji mmoja kapoteza kaka yake lakini pia watu wanaotufanya tuwe salama mipakani mwetu wameuliwa wakiwa wanalinda amani. Bahati mbaya haya ni mambo ya kijeshi hata kuweka mishumaa tu hatukupaswa kuweka. Wanajeshi wetu, nchi yetu tumepoteza watu muhimu na pengo lao ndilo linatufanya tuwe na ari zaidi ya kusimamia amani si nchini tu bali Africa nzima. Huhitaji kupitia JKT au mgambo kuyajua haya, mimi nayajua sababu huwa naangalia sana muvi za komandoo John na komandoo Suzi

Heshimu mazingira, heshima ni kitu cha bure, unalijua hilo. Sio unakuwa kwenye nyumba ya ibada unatafuna jojo (big G) kwa sauti utasema breki za treni. Unaenda kupiga picha kwenye swimming pool umevaa suti na nguo za vitenge na mbaya zaidi umeona kabisa kibao usikojoe hapa, wewe unakunya kisa kuna tofauti ya haja ndogo na haja kubwa.

Muziki sasa, ujue nakufurahia nikikuona hapa na siku zote sichoki kusema kuwa Kapuku forum ni sehemu bora kabisa kwa sababu wewe ni mmoja wa member muhimu.

 
...mmh, yaani kama msagaji na msagishaji wa mashine zile za unga? Mnaoishi mjini mnaweza mkaconfuse hili maana hamjui kuwa kupata unga huku kwetu hadi uende mashine kwa msagaji au jina maarufu msagishaji
Makubwa haya kwahiyo umetafsili hivyo woiiiiiii hapo nimekosea nilitakiwa niandike au loh binamu nitake radhi msagaji hapana aiseee dushe ilivyokua tamu ebu nijilalie mie mama angu nisamehe tu ni duduwasha hilo
 
Makubwa haya kwahiyo umetafsili hivyo woiiiiiii hapo nimekosea nilitakiwa niandike au loh binamu nitake radhi msagaji hapana aiseee dushe ilivyokua tamu ebu nijilalie mie mama angu nisamehe tu ni duduwasha hilo

...wewe unaishi mjini? Mmezoea kula ugali unga wa azam hamjui kuwa mahindi lazima yasagwe ndo upate unga, na yule anayesagisha mahindi anaitwaje?

usifanye wadau hasa BH akanielewa vibaya tafadhari
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom