Utafiti: Msaada
Nimeangalia data za magari yaliyoandikishwa hapa Tanzania, nimejaribu kuingia webpage ya TRA ambao ndo madhamana wa uandikishaji magari, sijaona idadi ya magari yaliyosajiriwa na yapo Tanzania. Nimeangalia NBS pia sijaona
Ikabidi niingia webpage ya WHO ambako nimekuta data za 2011 na zinaonesha magari yaliyosajiriwa hapa nchini ni 977,468 ikihusisha magari madogo 378,485, malori 70,254 na mabasi 41,625 idadi iliyobaki kuunda laki 9.8 inajumuisha pikipiki na vyombo vya moto matairi mawili na matatu.
Kama kuna mdau ana data za hivi karibuni anaweza kuziweka hapa ninapenda kufahamu kuhusu kitu.
Usiku mwema wadau