Makapuku Forum

Makapuku Forum

77facdb1a7df82bc850e6396ef8cb6fe.jpg
 
Muziki: Ongea, Okoa Maisha

...u khali gani wewe kapuku tunayethaminiana bila kuaminiana maana kuaminiana ni jambo moja, tofauti kabisa na kuthaminiana na ndo maana unakuta mke na muwe hawachangii mswaki, yaani wanaingiliana maungoni, midomoni na kote unakojua kuonesha wanathaminiana lakini kwenye mswaki hawaaminiani kabisa. Ndo hivyo bhana, maisha yetu ni full changamoto na ukijidai kuyawekea changabaridi basi utakachopata ndo utajua kwanini nyavu nzuri ni ile yenye matundu na si matobo.

Leo naandika mada ngumu, sio ngumu kwa ugumu bali ngumu kwa sababu hatupendi kuiongea, kujiua. Yeah, suicide ndo kujiua kwa kiswahili. Inakadiriwa kwa mujibu wa WHO (2017) watu karibia ya 800elfu, lakini nane hiyo hujiua kila mwaka na nchi zinazoendelea ndo zina namba kubwa ya wanaojiua. Kujiua ni sababu kubwa zaidi ya vijana wenye umri wa miaka 19-29. Kujiua ni tendo linalosababishwa na ugonjwa wa akili, msongo na sababu kadha wa kadha. Kama binadamu tuliokamilika tunapitia mengi hadi kufikia hapa tulipo leo, wengi tumewaza kujiua na kupuuzia si kwa sababu tuna akili kuwazidi wanaochukua maamuzi haya bali tulijipa nafasi ya kuongea na walio karibu yetu. Wengi wa wanaoamua kujiua ni kwa sababu hawakujipa nafasi ya kukaa na kuongea na wanaowajali, waliamua kukaa kisiwani, peke yao, wakamezwa na giza.
Kujiua kunazuilika, jipe nafasi kama sio wewe au mimi basi kuna mmoja tunamfahamu na tuko karibu naye, tuongee kwa kujaliana ili kuondoa ugonjwa wa kujiua, maana kujiua kunatibika kwa kuongea na kuona kuwa unathaminiwa hata kama huaminiki.
Muziki sasa, nimeongea na mjomba wangu, mengi tu kuhusu mwaka unavyoisha na nini tufanye kuwa na wakati mzuri wakati tutakapoenda kutembelea familia mwisho wa mwaka, ila tatizo la anko sasa hakuwa wazi alimung'unya maneno pale nilipomuuliza kama ataenda na aunt yangu mnayemjua. Niliuliza sababu niliona text ikimwambia CM kuwa ajiandae na safari, dada yake ambaye bahati mbaya ni mama yangu ana kazi kwa huyu kaka yake. Furahia muziki na tambua kabisa Jukwaa hili ni sehemu nzuri kwa sababu wewe uko hapa, bila wewe hata mimi nisingekuwa hapa maana sichangamani na wasamalia mimi myahudi wa kuchora

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom