Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Tamka Sawasawa Andika Tofauti

...nataka nikupe siri moja kuhusu kesho, najua ulikuwa hujui na kama ulikuwa unajua basi sio mbaya nikishare na wasio na taarifa. Si unajua information is power wanasemaga wanaoongea lugha zaidi ya hii tunayoipenda. Kwa taarifa yako tu, kesho ni Jumatano. Na hii kesho ni siku nzuri kujiandaa na siku inayofuata na siku inayofuata ikifika ujue kambisa Ijumaa imekaribia. Siku juu ya siku.
Asante makaveli10 na aunt yangu asiyenipenda Shunie kwa kutusogoza mchana na wakati huu, ninyi ni watu poa sana na tunawapenda, well, nisiwasemee wengine, mimi nawapenda na mnalijua hilo. Kwa makapuku wote, mjue uwepo wenu huwa kunalifanya jukwaa hili kutokuwa mfano bali kuwa origin ya majukwaa yote yanayoanzishwa kuiga. Tutabaki kuwa makapuku na hilo halina ubishi, wavue au wavuliwe, wakae uchi au wabaki watupu, waongee au wanyamaze. Ungependa kusikia nini kingine usiku huu?

Muziki sasa, wiki jana nilikuwa Ruangwa nakula pilau na sasa nimerudi Mtwara nimejipumzisha muda huu baada ya shughuli kubwa ya kushehereheka.

Asante binamu uwe na usiku mwema Yesu akulinde na damu yake
 
Sitaki binamu acha nilale tu
sxeMFHH.gif
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom