
Tuombe
Bwana Yesu asante kwa
Jumanne ya leo.
Asante kwa sababu ni siku njema tena uliyoifanya Mungu
Tunasema asante kwa ulinzi wako
Umetulinda na hila zote za adui na umetuamsha tukiwa wazima na wa Afya kabisa.
Siku ya leo tunazidi kujikabidhi kwako uendelee kuwa nasi usituache Bwana.
Bariki kazi za mikono yetu .
Tulinde na tuepushe na hatari zote za adui shetani za mwili na za roho.
Bwana Yesu.
Ukatuongoze katika maisha yetu tukuone wewe.
Kumbuka wenye shida,taabu na mateso .
Ponya wagonjwa wote majumbani na mahospitalini.
EeeMungu ukawakumbuke. Yatima ,wagane na Wajane Mungu ukawatetee.
Ongoza hatua zetu Bwana ktk Jina la Yesu Kristo Amina.!!!.