Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20171130-WA0005.jpg
 
Muziki: Sielewi Chochote, Nimelalia Masikio

....nimekaa
sehemu tangu jana, eeeeh, ndo maana ninaingia huku siku mbili tatu hizi kimachale maana tangu asubuhi hadi usiku. Kifupi niko semina na kiinglishi ni kingi kuliko Kiswahili, yaani huwezi amini nilivyokonda Kapuku mwenzenu. Usifanye mchezo kuongea kizungu tangu asubuhi kwenye breakfast hadi dinner. Ni mwendo wa kijiko na uma tu. Well, kwenye lugha nakomaa tu ila kwenye kula sasa, hivi kweli jamani samaki unaweza kumla na kijiko? Nawauliza tu wala hamna haja ya kuona wivu maana samaki ile sehemu yake ya tumboni kushuka chini chini kidogo unaweza kula na uma kweli?! Nikawaacha wanashangaa maana nikaweka uma pembeni nikanawa nikapeleka vidole na kile kidole chetu pendwa kikatest kama kuna ulaini unaofaa kunyonywa.

EEh, kunyonywa maana unaweza kunyonya kumbe hajasafishwa vizuri full, magamba bahati nzuri samaki hana manyoya vinginevyo ukimnyonya pale chini ya tumbo basi unaweza kuanza kukohoa kwa fujo kiasi kwamba unahitaji ile dawa ya kusafishia chemba iliyoziba ili kuondoa vinyoyanyoya (magamba). Basi tuachane na mambo ya kula nisijekuonekana mroho kwa kuwatia njaa tu hata picha siweki. Nimekonda jamani, usifanye mchezo na kuongea kiingilishi.

Muziki sasa, ilifika zamu yangu ya kupresent, nikamwaga umombo wa kukariri maana niliongea na anko before akanipa nondo za kuongea, ushauri wangu nilewe kwanza ndo kingereza kitakuja chenyewe tu na sitakuwa na furasturesheni kama za mkulu. Nikamwagika balaa, mzungu mmoja akanyoosha mkono, hi sir mzee Obe, we can't understand you. Nikaweka pose, well, who else is not understanding me, nimetoa macho, wote mikono chini nikajua wanaelewa, it seems you are not listening, nikamjibu huku nikiangalia saa niende nikale samaki wangu ambaye nilimuacha mjomba anamuangalia, sijui kama nitamkuta maana anko wangu Lyon Lee kwa uroho wa samaki, simshangai maana ni mambo ya ukoo. Kama umenielewa utanijulisha.
Good night my fellow great Kapuku (good thing you are not a pauper)


Asante Obe

Sent from my TECNO H6 using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom