Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Utaelewa Tu, Jipe Muda

...inabidi niandike haraka haraka maana nimepata mapumziko mafupi, si unakumbuka nimekuambia toka juzi kuwa niko kwenye semina. Sasa leo kuna mabadiliko kidogo, semina yetu inaungana na washauri wa masuala ya UKIMWI sijui wametoka wizara gani lakini ndo hivyo kuna mabadiliko maana tumechangamka na kwa kuwa kesho ni sikukuu (haijalishi kama unaisheherekea au la, wewe ungana na tunaosherehekea)
Sio mbaya kuchukua muda mrefu kuelewa jambo, waswahili wana kamsemo ka ajabu kiasi kuwa harakaharaka haina baraka. Kama unakaamini au la ni juu yako lakini kwa sisi, mimi na anko wangu ambao ni waumini wa situationship (inahusiana na mahusiano) huwa tunafanya kile kinawezekana leo na kinachoshindikana leo basi tunajipa muda wa kusubiri ili iwezekane baadaye. Kujipa muda ni tiba ya mengi, usijidai ukafanya maamuzi ukiwa na hasira, jipe muda ndipo uchukue maamuzi yanastahili. Ukijipa muda, muda ni tiba kama ulikuwa hujui utaelewa tu.

Sina la maana sana leo after all, maana lazima nayo ina maana yake na kama hujaamua kuipa maana basi maana haina maana hata uipambe kwa lolote la kuvutia na uturi ulinyunyize. Nakupenda Kapuku na ninakutakia mapumziko mema, and happy Mawlid-day, a long weekend if not mistaken. Ngoja nikae na huyu dada wa masuala ya UKIMWI anishauri namna bora ya kuvaa kondomu, nitatoa mrejesho

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom