Makapuku Forum

Makapuku Forum

c0c3d275b92b8caad8124147c85047e5.jpg
 
TUOMBE
Mwenyezi Mungu Mtakatifu, Mfalme wa wafalme,Baba wa Milele,Mshauri wa Ajabu,Mungu mwenye Nguvu Asante kwa kutufikisha siku hii ya leo Jumanne, 21 Novemba 2017 salama
Tunakushukuru kwa sababu Upendo wako ni mkuu kwetu, Kwa sababu unatulinda na kutuongoza, Kwa sababu unatupigania, Kwa sababu Unaweza yote,Unajua yote,Upo kila mahali. Mungu wetu tunaomba usinyamaze kila tukwitapo sisi peke yetu hatuwezi.
Tupiganie katika kila Jambo,Tufundishe,tushauri na kuturudi tunapokukosea. Mungu bariki Afya,Kazi,kusudi,Uchumi na Imani zetu.
Waponye wagonjwa wote Baba majumbani na mahospitalini,fariji wafiwa wote wape faraja yako popote walipo,angalia wajane,wagane,yatima Baba wape hitaji la mioyo yao,wasaidie wote wanaopitia changamoto mbalimbali.
Wasaidie wasafiri wote kokote waendako majini,nchi kavu na angani waende na kurudi salama..ponya mioyo yote inayotaabika kwa huzuni na dhiki ,tuongezee imani Baba tukuangalie wewe tu maana wewe Baba hukawii wala huwahi jibu lako ni ndiyo.Roho Mtakatifu kaa nasi siku zote za maisha yetu.
Ni katika Jina la Yesu tunaomba tukiamini na kushukuru Amina.


SIKU NJEMA .
 
Naona anko baada ya kuanza kurecover baada ya kile kipigo ameanza kutamba haswa na leo hii ashapanga appointment na mwarabu wake wa pemba ila hajasahau kukusalimia kapuku ...anauliza siku zenu zikoje ??


...anko, nimepita mahali nikasikia jina langu linatajwa, sasa nikajiuliza, kile kipigo si tulikisolve kijemadari japo maumivu bado ninayo hapa naandikia mkono wa kushoto maana wa kulia una PoP.

Kuna mtu anataka kunihamisha mawazo yangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom