Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 19

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

Sasa huku kwa shadi kumbe hata shadi alikuwa akizisikia hizo sauti za akina sheby na zai...
Huezi amini nae alikua akijitomasa katika kifua chake... Sasa swali linakuja hivi, Kama shadi ni malaya, sasa mbona anazishangaa sana na kuzifurahia sauti hizo, kana kwamba hajawahi hata kuzisikia wala kukutana nazo, na wakati yeye ni malaya.... Mi sijui twendeni mbele

Tukirudi huku katika chumba cha akina sheby na zai,.. Sheby alisitisha denda kwanza na kuanza kuongea mambo ya ndoa yao, mana zai ndio kaanza
"we sheby umeamua kuvunja kiapo, lakini sawa tu kwani kuna nini"
Hapo ndipo sheby akasitisha kumnyonya mate mpenzi wake
"aaahhhh nisamehe zai"
"No, mi nipo tayari kama utataka"
"zai... Kuna kitu nataka kukuambia ila sjui kama utakasirika"
"we bwana kama wataka mapenzi ina haja gani uniambie, we nisukumie kitandani nipe vyangu, mi ni mkeo mtarajiwa huna haja ya kusema nataka.. We nivute ule vyako jamani sheby"
"sio hilo"
"nini kwani.... Au umeanza tabia mbaya, mana nyie wanaume wa siku hizi manpenda sana tabia mbaya..."
"tabia gani tena sisi tunaipenda"
"si kurukana hovyo hovyo... Mi naomba hilo lisikupate mme wangu"
"zai.... Mi mwenzio nimeoa"
Zai ana macho makubwa yalimpendeza kutokana na umbo lake, lakini kwa maneno hayo alioyaongea sheby, macho ya zai yamekuwa makubwa zaidi... Mpaka sheby aliogopa huenda yakapasuka..
Lakini sasa kumbe......

ENDELEA.........

Mapenzi ni upofu, mapenzi hayana utani hata kidogo, na pia mapenzi nzi hayana heshima unaweza ukajikuta unapenda bila ya wewe kujijua, unashtukia tu una mpenzi, kupenda kubaya sana tena haswa akipenda mwanamke hua mpaka aje aseme itachukua muda mrefu sana, labda awe malaya, lakini kama ni mtu anaejiheshimu hawezi kumtongoza mwanaume hata siku moja, yeye atabaki kuwa kimya muda wote, akisubiri wewe mwanaume uanze kumsemesha....
Kijana sheby na mpenzi wake zai wakiwa katika ya mahaba mazito, lakini wakati huo kijana huyo alikuwa tayari kumwambia ukweli zai kuwa ameoa,
"zai.... Mi mwenzio nimeoa"
Zai ana macho makubwa yalimpendeza kutokana na umbo lake, lakini kwa maneno hayo alioyaongea sheby, macho ya zai yamekuwa makubwa zaidi... Mpaka sheby aliogopa huenda yakapasuka..
Lakini sasa kumbe Maneno hayo hayakumuumiza zai peke yake bali hata shadi yalimuumiza katika moyo wake, ukumbuke shadi anasikia kila kitu kule alipo, si unajua mambo ya nyumba za udongo hazinaga siri, labda mnong'onezane skioni, lakini bila ya hivyo ni lazima msikiwa na mtu wa upande wa pili, huezi amini shadi kshikilia kifua chake huku roho ikimuuma kwa kusikia sheby kaoa,.. Kwahio kumbe hata shadi anampenda sheby sema anaogopa kumwambia afu istoshe ana mpenzi wake ambaye ni zai,...

"mume wangu, ivi hio ni story au ni kweli"
Aliuliza zaituni huku akiivuta kanga yake avae
"sitaki kukudanganya, ni kweli nimeoa na nina mwezi wa tatu sasa toka nioe"
"sheby mume wangu, kwaio mimi sina hadhi ya kuwa mkeo... Ahsante sana lakini"
Zai alianza kulia na kukata tamaa ya kuolewa,.. Sheby akaona kumbe zai anampenda sana na anatamani siku moja waishi wote..
"nimekudanganya bwana sina mke wala nini"
Ilibidi amdanganye kuwa hajaoa, lakini ukweli tunaujua kuwa sheby ana mke,..
Sasa huku kwa shadi kuskia hivyo tu alijikuta anaropoka kwa nguvu
"afafhali huna mke jamani"
Sheby aliskia lile neno lakini zai hajaskia vizuri
"nani kasema afadhali"
"aahhh ni watu huko nje sjui wanadaiana"
Aliongea hivyo, lakini sheby kajua hio afafhali imetokea wapi..

Basi kijana sheby aliondoka zake mpaka kwenye vituo vya mikokoteni na kumpa mwenye mkokoteni wake, kisha kaingia hoteli na kuvaa nguo zake za asili yaa uhalisia wake, kama kawaida kachukuwa gari yake na kuingia zake ofisini,.. Kiukweli kijana sheby anateseka sana,..
"mary namsikia boss sjui kaingia sasa hivi"
"ebu kamcheki basi"
"mmmhhh subiri tuone kwani si lazima atembelee wafanyakazi wake"
Kweli sheby hua ana tabia ya kutembelea wafanyakazi wao ili kujua aliopo na ambae hayupo,..
"za saa hizi boss"
Ilikuwa ni sauti ya amina ikimsalimia sheby
"salama tu hali yako"
"safi tu"
Alizunguka ofisi nzima kisha akarudi kuketi katika ofisini yake, wakati huo mzee wake bado hajafika kazini,..

Sasa huku uswahilini baada ya sheby kutoka, shadi karudia kuvaa nguo zake zile zile za kimalaya kisha akachukua kipochi chake na kutoka..
"shadi unaenda wapi saa 5 hii"
"heeeeeeee mi sio golikipa mwenzangu naenda kufanya kazi"
"lakini shadi, kwanini usitafute mwanaume mmoja tu utulie"
"heeeeeeee we zai, mwanaume mmoja atanipa nini mimi, wanaume wenyewe ndio hawa wanaotembeza viazi na mikokoteni"
"no simaanisha Mchumba wangu, we tafuta yeyote yule, kwani lazima auze viazi kama sheby wangu"
"mmmhhh Eti sheby wangu.... Funguka akili wewe, unaweza ukakuta mwenzio kaoa tayari huyo, unafanywa mchepuko tu apo"
"sawa wacha niwe mchepuko tu... Lakini siwezi kumwacha sheby wangu... Shadi, mimi nilikuwa sioni mimi nilikuwa kipofu, lakini kwa uwezo wa mungu, kamjaalia mpenzi wangu akaniseidia... Siwezi kumsaliti"
"utabakia hivyo hivyo"
Shadi aliondoka tena kwa kuita tax,.. Wakati huo sasa ndio anaonyesha makucha yake...
Zai aliingia zake ndani na kuangalia mazingira ya nyumba hiyo akiangalia kitanda, akiangalia makochi ya mbao
"hivi hivi nitaishi nae tu"
Aliongea zai huku akijilaza kitandani,. Zai ni mschana mrembo sana, yaani ana umbo la kipekee sana yani...

Sasa huku kwa akina mama yake na zai aikiwa na Zainabu, pacha wake na zaituni..
"ivi mama, kwanini zaituni hajui kama mpenzi wake ni tajiri"
Aliongea Zainabu huku wakiwa wanakula, yaani mama anawapenda sana watoto wake, japo huyu mmoja ni katili lakini bado anampenda tu..
"afu wewe ndio uliompa umbea kuhusu huyo mwanaume wake"
"wala mimi sijaongea nae mwanao.. Labda alisikia tukiongea"
"naomba uache umbea wako, japo mimi sijui kwanini huyo kijana hataki ajulikane na zaituni"
"we mama weee, usije ukamuuza mwanao"
"kwa jinsi alivyofanya yule kijana, nimemuamini kwa asilimia zote"
Mama Aliongea ukweli wake juu ya kumwamini kijana huyo,..
"mmmhhhhh haya, afu dada hajaja siku nyingi nimemmisije"
Aliingea Zainabu kana kwamba anamemisi sana dada yake wa kwanza mana huyo kaolewa na keshatulia na ndoa yake,...

BAADA YA SIKU KADHAA KUPITA

Rehema ambae ni dada yake na sheby akiwa yupo nyumbani, alikuwa akishangaa sana kuskia mdogo wake kaoa,... Japo alijulishwa kwa simu akiwa chuoni..
"mama, umekubali vipi sheby aoe, huoni kuwa bado ni mdogo yule mama"
Aliuliza rey huku akiwa mkali juu ya mdogo wake kuoa akiwa na umri mdogo..
"mwanangu rey, mimi nimeongea lakini sijasikika kabisaa"
"huyu sheby ana akili kweli, yaani anadiliki vipi kuoa.. Atilist angelikuwa hata na miaka 25"
"heeeeeeee, kwani kaamua yeye, ni baba yako ndio kamlazimisha aoe"
"ati nini... Yaani baba ndio kamwambia aoe"
"sio kumwambia tu, na kumchagulia mke kabisaa kisa ni mtoto wa rafiki yake"
"na wewe mama ukakaa kimya"
"mimi niseme nini na wakati baba yake kaamua kumpa mtoto wake mke"
"wanaishi wapi sasa"
"kule bondeni"
"ngoja nitakwenda kuwasalimia"
"ila staki fujo, sitaki fujo na huyo mwanamke, na kama unakwenda kwa fujo bora usiende"
Mama anamjua mtoto wake rey sio mtu wa kudharauliwa, kitu kidogo tu ngumi mkononi...
"naenda kumsalimia tu"

Ikiwa ni mida ya jioni hivi kama saa 11, Shadi akiwa anarudi mjini tena alikuwa kavaa nguo zingine tofauti na zile alizotoka nazo asubuhi..
"shost, we zai upo"
"heeeeeeee, shadi umebadili nguo tena"
"sasa je, nifanyeje na wakati pesa inaingia tu"
"mmmhhhh umependeza"
"hata wewe unaweza kupendeza tena zaidi ya mimi"
"mmmhhhhh lakini shadi kazi yako ngumu sana kwakweli"
"sikia wewe acha ujinga,.. Una sura nzuri una umbo zuri tena kuliko hata mimi, nashangaa unabweteka tu hapa na kula viazi vya kuchemsha kila siku"
Aliongea shadya kwa kumshawishi zai nae aingie katika kazi alionayo...
"mmmhhhh... Mi nampenda sheby, hivi kwa hiki alichonifanyia, afu leo ananikuta nina mwanaume ivi atanifanyeje"
Aliongea zai huku akiwa kama anaanza kukubali
"heeeeeeee kwani hujaona sheby alivyokuja mi nimebadilika ghafla... Na ni nani atampa taarifa,.. Tafuta pesa wewe acha kubweteka una vyanzo vya pesa nashangaa unavikalia tu"
"mmmmhhhhh... Sasa"
"sasa nini zai.... Hebu ngoja niite tax kwanza nikakunyuke pamba afu usiku tutoke au vipi"
"mmmhhhhh... Sheby atanioana bwana hapana"
"sheby na umaskini aliokuwa nao atawezaje kuingia sehemu za kitajiri? Hio pesa ya kuingilia hapo atatoa wapi"
"haaaa, ina maana wewe unafanyaga na matajiri"
"sasa si ndio mana nami nina pesa, unataka utembee na kapurwa ili iweje"
"mmmhhhh lakini.... "
"acha ujinga.. Ngoja niite taxi,.. Kwanza kila siku unaniomba buku buku zangu wakati hata wewe unaweza kuzipata..... Eeehh haloo Taxi, njoo hapa uliponishusha muda huu"

Tukija huku kwa mke wa sheby akiwa kakaa kwenye kioo huku anajipodoa, yaani meza imejaa vipodozi tu, hakuna mafuta ya mchezo mchezo hapo yote ni ya bei ghali mno....
"hodii"
Alisikia hodi ikibishwa huko sebuleni, wakati yeye alikuwa yupo chumbani kwake,..
"karibu"
Aliongea huku akiuendea mlango na kuufungua
Alikutana na sura ya dada yake sheby sema hamkumbuki vizuri ila dada yake sheby anamkumbuka mana ni watoto waliokuwa kuwa pamoja pamoja, lakini walipokuwa wakubwa kila mmoja alijua mambo yake,.. Na sababu ya hawa kujuana kidogo ni kwamba baba wa mwai na baba rey, ni marafiki toka zamani,..
"mambo"
Rehema alimsalimia mwai lakini mwai alikunja mdomo na kuitikia
"poa nikuseidie nini"
Rey kaingia mpaka ndani na kukaa bila hata kukaribishwa,.. Mwai hamkumbuki kabisa rey lakini rey anamkumbuka ila sio sana yaani kama taswira yake inamjia afu inapotea, si unajua mavipodozi yakiwa mengi usoni hata uhalisia wa sura hupotea,..
"we dada vipi, nakuuliza nikuseidie nini"
Aliongea mwai huku akimjia kwa ukali
"kwanza ungeuliza mimi ni nani afu uongee unavyotaka"
"sioni haja ya kukujua, we sema shida yako nikuseidie uende"
Mwai alikuwa akijibu vibaya kama jinsi anavyomjibu mume wake.... Lakini hahajua kama huyo ni dada yake na sheby
"kwa muda ulioolewa, natumai mpaka sasa hukosi mimba,.. Mana natamani niitwe shangazi"
Sasa mwai ndio anashtuka kwa maneno hayo, na kujua kuwa kumbe huyo alikuwa ni dada yake na mumewe....
"hahahahahaha, ni kweli ninayo ina mwezi mmoja"
Aliongea mwai huku akijichekesha baada ya kujua kuwa huyo ni dada yake sheby, hivyo ni wifi yake
"una uhakika"
"ndi... Nd.... Nd....ndi...ndiooo..."
Mwai alishikwa na kigugumizi cha ghafla, huku akishika tumbo lake
"nina kipimo hapa nimekuja nacho... Unajua mi napenda sana watoto, tena haswa haswa mtoto wako nitampenda sana"
Aliongea rehema kisha akakirusha kile kipimo kwenye meza, afu akamwambia...
"tuhakikishe wote... Mana natamani sana ulete mtoto wa kiume kama mumeo

Je? Nini kitaendelea??... Mwanaheri atafanya nini na hajawahi kufanya mapenzi na mume wake hata siku moja toka waowane... Na je rehema kajuaje kama mdogo wake hajawahi kufanya mapenzi na mkewe... Vipi kuhusu zai, kakubali kujiunga na shadi... USIKOSE
 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 22

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Simulizi hii inakujia kwa udhamini mkubwa wa #km_music

#KM _MUSIC INAWAKARIBISHA WASANII WOTE KUFANYA KAZI NAO NA WANAFANYA AINA ZOTE ZA MUZIKI.PIA KAMA UKO MKOANI NA UNAHITAJI BEAT KALI WASILIANA NAO KWA SIMU NA +255743761268

#kmmusic_____musi

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

"heeeeeee kwani vipi mwenzetu"
"we acha tu, nina janga hilo sijui nilipeleke wapi"
Aliongea mke wa sheby huku wakiingia ndani, kama kawaida yao wakikutana umbea mwingiiii...
"enheee hebu nipe umbea mana wewe kwa umbea umo kweli"
"yaani huu sio umbea.. Ni ukweli mtupu"
"nini tena mwai... Au Umeachika nini"
"bora hata ningeachika rose"
Mwai alikuwa anawaza atamwambia nini sheby kuwa ana mimba yake na wakati hajawahi kulala nae hata siku moja japo ni mume wake,..
"kwani una nini"
"nina mimba rose"
"heeeeeeee sasa cha ajabu ni kipi hapo"
"nina mimba lakini sio ya mume wangu... Ni mimba ya james"
"Eeeeehhh maakubwa ya jongo hayo"
"nipeni ushauri basi jamani nifanyeje"
"lakini mwai, kwanini mtoto wa watu hujawahi kumpa haki yake ya ndoa"
"ni kweli... Lakini mi simpendi yaani hata kumpa mwili wangu naota kama vile nafanya na mbwa vile"
Ghafla mary kadakia
"we dada mwai, yaani ukifanya mapenzi na huyo unahisi kufanya na mbwa?"
"we mary kwanza we bado mdogo yatakukuta haya"
"sawa lakini sio hivyo dada mwai unamkufuru mungu"
"atajua mwenyewe mi nakaona kama kambwa tu"
Mary hakutaka hata kusikiliza akaingia zake chumbani mana wamepangisha dabo rumu....
"sasa skia mwai mi nataka nikupe ushauri mmoja tu"
"ushauri gani huo"
"tembea nae.. Leo akirudi mpokee vizuri, mpeti peti... Mpe kitumbua chako, baada ya wiki unamwambia mimba ni yake... Hakatai ng'ooooo"

ENDELEA....

Kiukweli sisi wanaume tumekuwa ni watu wa kuibiwa kila kukicha,.. Tena haswa haswa katika upande wa ujauzito, hua tunapewaga vitu ambavyo sii vyakwetu,.. Na kwa upande mwingine hatuna uwezo wa kupima DNA kwasababu ni gharama kubwa sana, wanaiweza matajiri peke yao.. Sasa kwa sisi wanyonge tunapewa damu za watu na kuzikubali... Kiukweli wanawake mnavyofanya sii vizuri kibinaadamu, mpe mtu haki yake aende... Hakikisha mimba ni yake kweli umwambie, sio uone tu kwasababu ana uwezo flani ndi9 umtupie mzigo.. Mana siku hizi ndio tabia ya wasichana wengi,.. Wakipata mimba hua wanajipitisha kwa wale wanaume wenye mwelekeo wa maisha na kutembea nao kisha kuwapa mzigo ambao haukuwa wakwake, na ndio maana baadhi ya wanaume hukataa mimba hizo...
"sasa skia mwai mi nataka nikupe ushauri mmoja tu"
"ushauri gani huo"
"tembea nae.. Leo akirudi mpokee vizuri, mpeti peti... Mpe kitumbua chako, baada ya wiki unamwambia mimba ni yake... Hakatai ng'ooooo"

Aliongea rose huku akimsihi sana mwai afanye hivyo,...
"ati nini, yaani yule kinyago mi nimpe papuch yangu kweli"
Aliongea mwai huku akijiangalia kuanzia chini mpaka juu
"ok.. Kama hutaki acha,.. Ila mi nakuuliza hivi, endapo utamwambia una mimba yake, je? Yeye atakujibu nini na wakati hamujawahi kusex?"
Mwai alikaa kimya kwa kuambiwa hivyo, kana kwamba ni lazima atembee na aheby kimapenzi japo ni mumewe na wanaishi nyumba moja lakini tendo la ndoa kwao ni ngumu mno kupatika, mana hakuna anaempenda mwenzake,.. Ghafla mary kaingilia kati
"lakini ni kweli dada mwai, lazima umpe tu, mana hutoweza kumwambia una mimba na wakati hujawahi kumpa papuch yako... Afu usipomwambia mimba itaonekana na huenda akakuuliza au pia akatulia lakini anajua sio yake"
Aliongea mary huku mwai akijiandaa kujibu
"kwani hata akiiona na nikimwambia sio yake atanifanya nini"
Aliongea mwai kwa kujiamini, lakini mary nae akamalizia kwa kusema kuwa
"yeye hatokufanya kitu kwa uzezeta wake... Lakini je familia yake na yako vipi wakijua mimba sio ya mumeo?"
Mwai alikaa kimya huku rose akisema
"hilo nalo neno mary"
"aaahhhhhhhh yaani anione uchi wangu kweli... Yaani simpendi yule kijana nyie acheni tu"
"au kama vipi kaitoe utulie"
"no, siwezi kuitoa kwasababu hata James nimeshampa taarifa hizo na kasema nimtunzie mtoto wake"
"basi lazima uonewe uchi wako mama"
"mmmmhhhhh"
"sio mmmhhh tena, wahi nyumbani akukute ndio itakuwa vizuri"

Tukija huku ofisini kwa akina sheby wakiwa ndio wanatoka,
"lakini boss siku hizi unachelewa sana kutoka kazini"
Aliongea mfanyakazi wake ambae ni Saidi,
"aaahhhh amna lolote sema for now si unajua nimeoa sasa lazima nichelewe kidogo"
"hhh ni kweli, lakini lazima uwahi ili ukampeti peti mama la mama"
"hahahahaha yule anapetiwa usiku"
Maskini kijana sheby anaongea tu, ili aonekane mwanaume ndani ya nyumba, lakini yupo kama mwanamke mbele ya mkewe, na sio kuwa hawezi kuwa mkali kama wanaume wengine, sema wazazi wake wamemsihi asimfanye chochote kile, hata akimtukana amuache tu..
"ila boss nyie mlio oa mna raha eee"
"aaahhh sanaaaa... Yaani raha za tanga si unazijua zile"
"tena mtoto mwenye si mtanga kabisa yule"
"haswaaa"
Basi sheby na saidi wakiwa katika gari, sheby alikuwa akijioshea kwa kuoa lakini siri anaijua yeye mwenyewe,...
"wewe si una mke wewe hotelini unaingia kufanya nini"
"namnunulia mtoto mapocho pocho si unajua kuoa kulivyo"
"ahahahahahahaha sawa bwana niosheee tu"
Sheby anajua kabisa nyumba yao haipikwagi, mwanamke ni yeye na CHIPSI, yeye na KUKU au NYAMA yaani anataka vitu vya kukaanga kaanga tu.. Ila kupika hataki

Walifika mahari sheby na saidi wakaachana kila mtu akaelekea sehemu yake,... Honi ilipigwa katika nyumba ya sheby mlinzi alikuwa na juhudu za kufungua... Alikuwa ni sheby ndie aliepiga hodi, sasa cha ajabu aliofungua alikuwa ni mkewe.. Sheby alitoa macho, kwanini afungue mkewe je huyo mlinzi yupo wapi, sheby alijua tu lazima mlinzi keshafukuzwa, mana sio kawaida na haijawahi kutokea mwanaheri au mkewe kufungua geti,..
Sheby aliingia mpaka ndani na kuweka gari vizuri,..
"kisoji... We kisoji"
Sheby aliita kwa hasira kana kwamba kwanini alale afu mke afungue geti
"jamani mume wangu, nae huyo pia ni binaadamu mwache apumzike tu"
Sheby alibaki mdomo wazi huku akishikwa na mshangao wa hali ya juu, leo mwai kamwita sheby mume wangu,..
"unasemaje mwai"
"kwani ni vibaya kukuita hivyo"
"ahahahaha hapana ni vizuri tu"
Sheby alikuwa kabeba kuku wa kuchoma, mwai alipoona kamfuko keusi kakakimbilia ili kumpokea mumewe, wakati siku zote anamuangaliaga tu...
"naomba nikupokee mume wangu"
Kila kitendo au neno liliotoka kinywani kwa mwanaheri lilikuwa la kushangaza sana kwa kijana sheby,...
Kijana aliingia ndani, humo ndani kwenyewe alishangaa kuona kule jikoni kunapikwa, tena kulikuwa kunapikwa vitu vinavyonukiaaa, sheby hakutaka kushangaa zaidi,.. Alipitiliza mpaka ndani, alikuta kitanda kimejaa mauwa ya kuvutia, afu shuka liliandikwa,.. KARIBU MUME WANGU... Sheby hakusema kitu pamoja na kuona vitu vyote hivyo, sheby alikuwa akivua viatu lakini ghafla alishikwa mkono na mkewe
"naomba nikuvue viatu"
Mshangao ulizidi kumuelemea kijana sheby na kushindwa kutoa hata neno moja,.. Mwanaheri alimvua mumewe kila kitu kisha akawa anampeleka bafuni,.. Sheby kufika bafuni kakutana na jambo lingine, leo haogi maji ya mvua au maji yanayotoka juu, leo anaoga kwenye ndoo, tena maji yalikuwa na mauwa kadhaa tena yaliokuwa yakinukia vizuuri kabisa.. Sheby mshangao ulikuwa mzito kwake.. Mke alitoka ili mume aoge mwenyewe,... Sheby alimaliza kuoga kisha akawa anatoka hapo sebuleni kuangalia taarifa za habari.... Mezani alikutana na chai safiiii iliowekwa viungo vyote, yaani sheby muda wote huo kabaki kua kimyaa,.. Hajatoa hata neno moja kwa mkewe..
"karibu chakula mume wangu"
Sheby alikuwa hakatai wala nini, kanawishwa maji kisha kala chakula alichopika mkewe...
Sasa kuumbe kukaa kimya kwa sheby halikuwa jambo la kawaida,.. Mwanaheri aliangalia pembeni na kujichekesha kinafki huku akikumbuka kitendo alichokifanya kabla mumewe hajaja... Sasa alikumbuka saa ile akiwa kwa marafiki zake kule kwa akina rose na mary.... Sasa kumbe alipokuwa pale ilikuwa hivi......... Usikose inayofuata
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom