Muziki: Sunday Mduara
Ninaamini kabisa ushapangilia wiki hii iweje upande wako na wanaokuzunguka. Mimi wikend ilikuwa nzuri sana na inaendelea kuwa nzuri maana kuna mambo mazuri yametokea na mojawapo ni la kukuona wewe hapa Jukwaani. Asane sana kwa kuwepo hapa. Mbarikiwe sana mlioenda masjid Jumaa ya jana, kanisani Jumamosi na kanisani Jumapili. hongera kwenu mlioenda nyumba za ibada na bado mkawa na muda wa kwenda bar kunjenga uchumi wa nchi, ya kaisari mpeni kaisari. wenye ratiba za kibaiolojia wikend ndo muda mzuri wiki hii kujenga mwili.
Nilikuwa na anko mkubwa tunatazama soka hapa Chelsea akifanya mauaji ya kimbari (naelewa it sound not okay, lakini hapa maana ya kimbari ni ya kisoka zaidi si yale mauaji ya watu 800,000 kule Rwanda) kwa timu ya Man U. Hongera pia Arsenal kwa kilichowapata, ndo maisha na huu huwa ni mwezi wenu.
Muziki sasa, tulipiga story kidogo na anko zaidi akitaka mbinu za kujieleza namna akirudi kwa aunt yangu maana inaonekana majirani wameanza kung'amua kuwa hayupo kwa mkewe. Nikaskuti weee, ushauri wangu akabaki ananitolea macho tu maana ushauri nilioutoa hakuamini kama unaweza kutoka kwangu mimi mtaasisi na mshauri nasaha napima kwa macho. Anko tuwaroge majirani wasiseme ulikokuwa umetekwa. Punguza miduara upate mzingo