Makapuku Forum

Makapuku Forum

Karibu sana
Mama mchuchu mimi leo nilisoma hili neno hapa.
724823d80d42e6e20d8c035036ef2b00.jpg
 
ENDELEA.........

Sheby alilaani sana kitendo hicho alichomfanyia baba yake mzazi,... Na yote hayo ni kwasababu ya safari ya kwenda india ili aweze kwenda na zaituni mana kule kuna wataalam wa maswala ya macho, haswa haswa vipofu na kila kitu, na kama ataenda na baba yake basi nafasi ya kwenda na zai haitokuwepo mana baba lazima alete maneno ya hapa na pale,
Wakati huo kijana sheby akiwa karibu na baba yake Dokta alikuja na kumtoa ili amfanyie vipimo mzee rashidi..
Sheby akiwa yupo hapo nje ghafla anamwona dokta anatoka katika wodi aliolazwa baba yake
"nione ofisini kijana"
Aliongea hivyo dokta huku akiingia ndani, kijana sheby yupo nyuma ya dokta kujua hali ya baba yake,..
Walifika ofisini hapo kwa dokta, lakini dokta alikuwa akianza na maelezo meengi sana yaliomfanya sheby kukasirika sana
"dokta, tafadhali sana achana na maneno mengi... Mi nataka kujua baba yangu yupo hai"
Aliongea sheby huku dokta akitoa leso katika koti lake,..
Sheby kuona ile leso akajua anapewa yeye, kumbe dokta alikuwa anajifuta jasho lake ila hakuwa akimpa sheby..
"usiwe na wasiwasi kijana baba yako ni mzima, wala hana alipodhurika"
"dokta acha utani"
"baba yako tayari keshaaka ila achwe kwanza apumzike"
"naomba nikamwone mzee wangu"
"nimekwambia kapumzika"
Aliongea dokta, na hapo sheby akashusha pumzi kubwa sana kuashiria mwili wake umekuwa huru kwa tatizo la baba yake...
"sasa dokta... Tafadhali sana, naomba..... Naomba umwambie haruhusiwi kutoka ndani ya siku tatu"
"kivipi sasa, na wakati utatakiwa kuonfoka na mzee wako"
"sikiliza dokta..."
Sheby alitoa waleti na kumpa dokta kitu kama laki mbili hivi
"fanya hivyo.. We mwambie kutokana na afya yako kuwa sio nzuri haruhusiwi kutoka hapa hospitalini"
"sawa, hakuna shida.. Tena naandika na statement kabisaa"
Baada ya lisaa limoja mzee wake sheby aliamka na alikuwa yupo vizuri tu hakuwa na tatizo,..
Dokta huyo alikuwa karibu na mgonjwa
"mzee hutakiwi kwenda popote, hali yako sio nzuri kiafya, hivyo utalazwa"
"Whaaat, mbona mi najihisi nipo sawa"
"ndio, ila kwa vipimo vyetu sisi madakatari tumegundua umepigwa sehemu mbaya sana na imeumia ndani kwa ndani"
"eeeh mungu wangu wee, kijana wangu yupo wapi"
"yupo nje mzee"
"niitie mara moja"
Sheby aliharakisha kufika kwa mzee wake,
"baba? Vipi hali baba angu"
"aahhhh mwanangu we acha tu, kumbe nimeumia ndani kwa ndani"
"pole mzee,.. Pole sana, lakini kwani cha moto hukuwa nacho mzee"
"aahh mimi nilijua tu ni bijana wanataka pesa hivyo nilishuka niwape chochote ili watoe mawe barabarani"
"aaahhh pole sana mzee wangu"
Sheby alikuwa anakazia sana, na yote hayo sababu ni yeye,
"sasa kuhusu ile safari, nadhani sintoweza kwa mujibu wa madaktari"
"haaaaaaa mzee sasa itakuwaje, na pesa ndefu kama tutaufikisha dubai salama... Mana ulikuwa uende congo lakini kwa sasa unakwenda dubai, ni pesa nyingi sana ni zaidi ya bilioni 5 mzee"
"ni kweli, lakini sina maana ya kuziacha... Kifupi ni kwamba we jiandae uende, na mi najua documents zote unazo na tumeziandaa wenyewe hivyo kesho naomba upande ndege uondoke"
"mzee, nilitamani twende wote mzee wangu"
Sheby aliongea hivyo lakini moyoni mwake alikuwa na furaha ya hali ya juu mno, tena anasema ndio vizuri kabisa na ndivyo alivyotaka kijana huyo...
"fanya hivyo, hakikisha mzigo unafika dubai, na usaini mkataba wa bilioni 5.7"
"sawa mzee nitafanya hivyo"
Sheby alifurahi sana kuskia hivyo..

Usiku huo huo kijana sheby alikwenda kubadili nguo zake zile za kimaskini na kwenda kule kwa zaituni, uswahili sana huko..
Lakini kwanza aliingia kwa shadya
"asalam aleykh shadi"
"waaleykh msalaam hali yako"
"swalaama tu sjui weye"
"aahhh kwa uwezo wa alah subuhanahu wataalah tupo salama kabisa"
Sheby alikuja kwa shadi kumwomba kitu kimoja
"sasa shadi, kesho kuna safari nataka kwenda, lakini sasa bado nahitaji msaada wako"
Shwby wakati huo kavaa zile nguo zake za uswazi,
"kitu gani, mbona kama ni kuishi na mchumba wako naishi nae vizuri tu au kuna kingine"
"No, hakuna, ila nataka twende india"
Shadi alicheka kuskia sheby anataka kwenda India,
"ivi ulijua india ipo soko kuu kwenda kuchukuwa viazi"
"nipo siriasi kweli"
"wewe hizo hela za kuendea india umetoa wapi"
"nimekopa..."
Aliongea hivyo
"ivi sheby ngoja nikuulize, ina maana benk siku hizi wanakopesha watu kama nyie"
"ndio.. Haaaaa tena sasa hivi kwa taarifa yako kuna benki ya masikini na benki ya matajiri,.. Sasa nimekopeshwa na masikini wenzangu"
"hio benki gani ambayo hata kuskia sijaisikia"
"imeanza juzi tu kipindi cha huyu raisi wetu mpya huyu nani huyuuu aahh nimemsahau kidogo lakini ni benki ya juzi tu na inawahu mafukara na masikini wote nchini"
"kwahio sheby, hata mimi naweza kukopa huko"
"ndio ila sema wewe hujajiunga na uwanachama wetu"
"mmhhhhhhh kumbe kuna kujiunga tena"
"ndio"
"ok sasa huko india unaenda kufanya nini"
"nampeleka bibie kufanyiwa matibabu"
"waaacha weeeeeee"
"naomba ujiandae twende... Afu uje huku umuandae mwenzio ila usimwambie tunakwenda wapi sawa"
"sawa, kwani hulali hapa"
"hapana sintolala hapa... Ila nitakuja asubuhi mida ya saa mbili asubuhi"
"sawa"

Kesho yake mida ya saa moja hivi tunamuona kijana sheby kavaa vizuri sana na kuingia katika ile hoteli yake ya kubadili nguo,.. Alivaa nguo za kawaida kama vile ana safari, na wakati huo kwao alitoka akiwa smarti sana, lakini kaupunguza ule usmati wake, kavaa nguo za kawaida ila sio zile za kuuzia chipsi...
Alipomaliza hapo alichukuwa tax mpaka uswahilini kwa baby wake,...
"waaaaooo umependaza"
Aliongea shadi baada ya kumwona sheby kavaalia, kavaa vibaya vibaya lakini shadi kamwona kama kapendeza...
"ni nani huyo aliopendeza"
Zaituni aliuliza huku akitamani hata kumuona mtu aliopendaza
"ni mpenzi wangu"
"aaahhhh hahahahaha hongera yako"
Kitendo kile sheby alijiskia huruma sana, yaani mpenzi ni wake lakini kwakuwa haoni hata kuibiwa anaweza
"wala usijali baby wangu.. Ni mimi sheby"
"jamani shadi, kwanini unanifanyia hivyo, au kisa sioni jamani"
Hata shadi roho ilimuuma na wakati alikuwa akifanya utani,
"nisamehe sana zai, ilikuwa ni utani tuuu"
"najua.. Wala usijali shadi"
"sasa jamani twendeni"
Aliongea sheby huku akibeba mabegi yao na kuyaingiza katika gari..

Sasa tukija huku hospitalini ambako ndiko alipolazwa baba yake na sheby,
"mzee mbona we ni mzima tu wa afya"
Alikuwa ni dokta mwingine tofauti na yule alioongea na kijana sheby, sasa dokta huyu ndio kampima mzee rashidi na kugundua kuwa alikuwa ni mzima wa afya,
"mbona kuna dokta kuniambia nimeumia ndani kwa ndani"
"hapana mzee wangu, upo vizuri kiafya na unaweza hata kufanya shughuli zako"
Mzee rashidi bula kuchelewa anaamka kitandani na kuchukuwa simu yake, namba ya kwanza kupiga ilikuwa ni nanmba ya sheby....
Wakati huo namba ya sheby inaita kucheki jina anakuta ni baba yake
"huyu mzee ana nini tena mungu wangu weeeee"
Aliongea kijana sheby huku akitaka kuipokea simu hio... Hakutaka kuichunia, aliipokea na kuongea kwa wasiwasi mkubwa
"haloo mzee, kuna nini tena"
"subiri hapo hapo nakuja twende, nimepewa ruksa na dokta mkuu,.. Hivyo kuliko nibaki, ni bora twende wote"

Je? Nini Kitaendelea??....
 
Mama mchuchu mimi leo nilisoma hili neno hapa.
724823d80d42e6e20d8c035036ef2b00.jpg
KUTOKA 24:13
Mose akawaambia Waisraeli,Msiogope !,kaeni imara!Leo mtaona jinsi Mwenyezi- Mungu atakavyowaokoa,Maana hawa Wamisri mnaowaona leo,hamtawaona tena...14.Mwenyezi-Mungu atawapigania ninyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu

Hili ni neno la Imani na kila mtu kwa imani alishike..hayo magonjwa,kukataliwa,kuachwa,kufukuzwa kazi,kukosa pesa...kuuguliwa,kukwama kwa namna yoyote.hasirau,uchungu,majuto. Kukata tamaa..........hamtakuona tena..Mungu atawasaidia mnatakiwa kutulia tu kwa imani thabiti....MBARIKIWE
 
MKE JEURI

(The Wife's Tyrant)

Sehemu Ya 12



ENDELEA.......

Sheby akiwa na furaha ya kwenda india peke yake, huku akianza kuwaandaa akina zaituni na shadi kwa ajili ya safari, na sababu ya kusafiri na shadi ni ili kwenda kutoa msaada mdogo mdogo kwa zai, pale atakapokuwa hospitali, hivyo ndio mana mpaka shadya kaombwa aende nae,...
Wakati kijana huyo anapanga begi la nguo katika gari, ghafla simu yake ikaita, kuangalia jina alikuwa ni baba yake mzazi... Aliipokea na kumuuliza
"haloo mzee, kuna nini tena"
"subiri hapo hapo nakuja twende, nimepewa ruksa na dokta mkuu,.. Hivyo kuliko nibaki, ni bora twende wote"
Sheby alishangaa nani kampa ruksa mzee wake, na hapo ndio kwanzaa hata Airport hawajafika, na akitangulizana na baba yake itabidi zai na shadi wabaki,...
"sasa mzee, mbona mi nimeshaondoka na ndege ya saa 12,.. Yaani nipo mbali mno"
"aaahhhhhh shit, kwanini uwahi kiasi hicho"
"mambo ya kazi mzee, lazima ubembeleze kazi"
"shit.... Aaahhhh"
Simu ilikata, sasa sheby bila kuchelewa alipaki vitu haraka haraka katika gari,...
Nusu saa mbele wapo Airport,.. Maskini shadi hajawahi hata kufika Airport, yaani licha ya kupanda ndege, bali hata kufika Airport hajawahi... Zaituni yeye ndio kwanza hata hajui hapo tupo wapi,.. Sheby bila kuchelewa alifanya taratibu zote za usafiri mana yeye ni mzoefu kiasi flani mana sio mara ya kwanza kusafiri kwa ndege,... Baada ya muda mfupi walikamilisha kila kitu,.. Mpaka hapo zaituni hajui yupo wapi, ila anajua kuwa tunasafiri lakini hajui ni usafiri gani wanaoutumia kwa wakati huo,....
Shadya yeye ndio aliokuwa akiona kila kitu,.. Lakini katuliaaa, kama maji ya mtungi vile

Tukija huku ofisini kwa akina sheby, na leo ndio siku ya kuanza kazi wale akina mary na rose, mana tayari walishafundishwa na kijana sheby wameiva vizuri ila wanaingia kazini pasina mwenyeji wao ambae ni sheby,... Mapokezi iliwapokea na kuwaonyesha vitengo vyao mana kazi walishapata wiki iliopita sema wakadanganyiwa na sheby kiwa walipata msiba, hivyo waende msibani kwanza misha warudi kuendelea na kazi,.. Lakini haikuwa msiba kweli, bali ilikuwa ni ujanja ujanja wa kijana sheby ili awafundishe kazi, hivyo mpaka sasa wadada hao wameshajua kazi na leo ndio siku ya kuanza kazi,
"karibuni"
Alikuwa ni Secretary ndie aliewakaribisha katika ofisi zao wanazotakiwa kufanyia kazi.. Secretary aliwapeleka mpaka kwa boss mkubwa ambae ni baba yake na kijana sheby
"boss? hawa ni wale wasichana wa juzi"
"ooohhh sawa sawa kabisa,.... Habari zenu"
"salama boss shkamoo"
"marahaba hamjambo"
"hatujambo boss"
"ok... Poleni sana na msiba"
"tumeshapoa boss"
Akina rose na mary walikuwa na heshima mno kwa baba yake na sheby, mana mzee huyo ni mkali sana katika kazi zake...
"aaahhhh amina unaweza kuwapeleka katika ofisi zao,.... Na chumba ni kimoja ila chumba hicho kina patision (kimegawanywa) hivyo kila mtu na ofisi yake"
"sawa boss, ahsante"
"naombeni kazi ifanyike, sitaki mchezo na kazi"
"sawa boss"
Secretary aliwapeleka akina mary mpaka ofisini kwao, na kuwaelekeza baadhi ya vitu vidogo vidogo vya hapo ofisini... Mpaka hapo rose na mary wameshapata kazi

Tukija huku kwa mama yake na sheby akiwa nyumbani kwake na mama yake mkwe aliomtembelea kwa siku hio,...
"kweli mama kuna kitu kinaniuma sana katika moyo wangu"
Aliongea mama yake sheby huku akitamani hata kulia
"kuna nini tena mama"
Aliingea bibi yake sheby ambae ni mama wa baba yake na sheby,..
"baba sheby anataka kumpa mke sheby na umri huo kweli"
Aliongea mama huyo huku akitamani hata kugombana kwa swala la mume wake kutaka Sheby aoe,..
"lakini mbona mjukuu wangu ni mkubwa tu"
"mama??.. Miaka 22 ni mkubwa kweli, mjukuu wako bado mdogo mama"
Mwajabu hataki kabisa mtoto wake aoe na umri huo, mana anaona bado ni mtoto mdogo sana na umri wa kuoa bado haujafika,..
"hata mimi sijapenda, lakini kumbuka baba ni baba mwanangu, kama kaamua hivyo sawa,.. Wacha mtoto azoee maisha ya ndoa mapema, mana kama ni pesa mnazo sasa mwahofia nini"
"lakini mama, huyo mschana ni mkubwa, yaani hata mwanangu rehema ni mdogo kabisa yani"
Rehema ni mtoto wa kwanza kwa huyu mama yake sheby... Na sheby ni mtoto wa pili, kisha anafuata Rajabu akiwa ni mtoto wa mwisho katika familia hio...
"mmmhhh kwanini lakini afanye hivyo"
"mimi sijui,... tena nilitaka kuja nyumbani kukupa habari hizi, lakini mmhhh"
"mwajabu, punguza hasira, ngoja nitaongea nae vizuri"
"sawa mama"
Moyo wa mama huyo ulitulia baada ya mama mkwe wake kusema kuwa ataongea nae vizuri

BAADA YA MASAA 10 KUPITA

Na sasa akina sheby wakiwa ndio wanaingia ndani ya hospitali hio yenye matibabu ya kimataifa,.. Walipokelewa vizuri sana lakini sasa sheby alikuwa anatafuta njia ya kuwakabidhi hapo hospitali ili atoke kufuata kazi iliomleta huku india, mana kuja hospitali ni ziada yake tu, lakini kikubwa ni kazi, na huko kwenye kampuni wanafunga mida ya saa 11 hivyo akichelewa tu, imekula kwake.. Zaituni alichukuliwa na kupelekwa katika wodi ya wagonjwa wa macho, alianza kufanyiwa vipimo na madaktari bingwa katika hospitali hio,
"ivi dokta, kuna uwezekano wa kupona kweli?"
"aahhh mbona hajaathilika sana huyu, kunaletwa wagonjwa hapa mpaka tunahaha, lakini nimempima huyu ni lazima apone"
Aliongea dokta huyo huku akiahidi kupina kwa zai...
Huku india kiukweli kila kona anayopita kinana sheby kulitakiwa kuandikwe kwa Kingereza, lakini ili nisiwachanganye mashabiki zangu katika kusoma.. Basi itabidi niandike Kiswahili, lakini ilitakiwa Kingereza kwa huku india, hivyo hata sheby anapoongea anaongea Kingereza lakini mwandishi kaifanya tu kama kiswahili tu....

"itachukuwa siku ngapi"
"wiki moja tu"
"aahhh ok sawa"
Wakati sheby anaendelea kuongea na dokta, ghafla simu yake iliita, kuangalia jina alikuwa ni mr mageshi, tajiri mwenye mzigo unaotakiwa kufika dubai
"ndio mkuu"
"mbona hufiki, muda unakwenda huu"
"ok nafika hapo mara moja"
Kijana sheby alimaliza kila kitu hapo hospitali, lakini ilikuwa ni kisiri siri hata shadi hajaona pesa ilivyotoka,.. Alipomaliza kulipa malazi ya wiki nnzima mpaka matibabu yote,.. Alimfuata shadya..
"sasa mama, chukuwa hii laki moja kwa ajili ya kulinda mfuko.. Mana chakula malazi kila kitu ni hapa hapa, hivyo kaa karibu na mgonjwa"
"sawa kaka... Sasa unaenda wapi.. Mana mi mwenzio sijui wanavyoongea hawa watu"
Sheby ndio anastuka kuwa kumbe shadya hajui kuongea hata Kingereza, duu kazi ilikuwepo kwa kijana sheby
"kwaioooo, dahh, lakini sio tabu mimi narudi sasa hivi"
"sawa usichelewe basi"
Aliongea shadya huku akiingia katika chumba cha kulala ambacho ni kama hostel humo humo kwa ajili ya wauguzi wanaowaseidia wagonjwa wao...
Sheby aliingia mahari na kubadiri nguo zake za kawaida kisha akavaa nguo za asili yake,.. Mara moja anachukuwa tax iliomfikisha katika kampuni ya mr mageshi,..
"yes boss"
"umechelewa sana lakini hakuna shida"
Aliongea mr mageshi huku wakielekea katika godown lenye mashine inayotakiwa kusafirishwa,..
"sasa kama unavyoiona Mashine ni kubwa na itatakiwa kusafirishwa na ndege kubwa"
"ookee na documents zote zipo tayari"
Sheby aliuliza kana kwamba alitamani sana kuambiwa bado,
"ndio, hapa ni wewe usaini, kisha niite ndege ije ipakie mzigo uondoke"
Aahhh kijana alichoka baada ya kusikia kila kitu kipo tayari,..
"ok nadhani kesho itatakiwa ifike dubai"
"yes, yes,.. Tena ina haraka sana"
"ok unaweza ita ndege ije kupakia"
"malipo yao unayo kabisa"
"ndio"
Haikupita muda ndege kweli imefika mpaka katika kiwanda hicho kinachotengeneza injini za vyombo vyote duniani, hivyo kuna injini ya meli toleo jipya, ambayo ina injini nne ndani lakini zipo sehemu moja, mana ndege na meli hua zinakua na injini zaidi ya moja, lakini hii ni moja lakini imekusanya injini nne,.. Ina ukubwa wa nyumba yenye rumu mbili...
"imeshalipiwa vibali vyote"
Sheby alizidi kuuliza ili tu kimoja wapo kikosekane aweze kuendelea kuwepo karibu na hospitali...
"kila kitu, yaani ni wewe kupanga unaondoka saa ngapi"
"itabidi niondoke kesho"
Sheby alikwenda kuongea na wahusika wa ndege kuhusiana na usafirishaji..
"kiasi cha transporter kinakwenda vipi"
"milioni mia mbili"
"duuuuu... Mr mageshi.. 200 milion from here to dubai?"
"tena hapo umefanyiwa fea sana, wanachajiwaga mpaka 300"
"mmhhh ok, tutaondoka kesho saa mbili"
Kila kitu kilienda sawa, malipo ya usafiri,.. Mashine yenyewe inauzwa bilioni 15 za kitanzania, na hapo ni tofauti na usafirishaji,.... Hivyo bilioni 5.7 watalipwa akina sheby kwa kufisha mzigo na kufanya kila kitu mpaka mzigo kufika eneo husika..

Mara moja baada ya kila kitu kwenda sawa, sheby alisaini mikataba yote kila kitu, kasoro mkataba wa pesa ndio bado hajasaini...
Baada ya kufanya hivyo kifuatacho ni kwenda hospitali,.. Alipofika alimkuta zaituni kafungwa mabandeji katika macho yake,..
"usijali mgonjwa wako atatoka salama"
Aliingea dokta huku akiendelea kufanya mambo yake ya kidokta,..
"ok hakuna shida.... dokta, kuna yule mschana nilikuja nae hapa atakuwa kalala"
Aliuliza hivyo kwasababu ilikuwa ni kagiza kameshaanza kutanda,..
"kwani ulikuja na mschana mwingine"
"ndio, mweupe mweupe hivi"
Mara ghafla kuna nesi kaja na kusema kuwa
"kuna mschana wa kiafrika yupo mochwari"
"unasemaje wewe nesi??"
Sheby alishtuka kwa kusikia hivyo, hata mapigo yake ya moyo yalianza kwenda mbio
"ndio.. Alidondoka baada ya kuona mtu kajeruhiwa vibaya, alifanyiwa vipimo vyote, lakini ameonekana keshapoteza maisha"
"Mungu wangu shadya wa watu"
Sheby alilalamika huku akipelekwa chumba cha watu waliokufa (mochwari)..
"si ndio huyu hapa"
Aliongea dokta mmoja huku akinyoosha kidole, kuashiria ndio huyo waliokuwa wakimsemea... Kijana sheby alitoa macho kama mjusi aliobanwa na mlango
"mungu wangu... shadya wewe, nitakwenda kujibu nini kwenu mimi"
Sheby aliongea hivyo huku akiinama chini, kumkagua vizuri.... Lakini sheby akiwa anaendelea kumkagua shadya pale chini, ghafla simu yake inaita, kucheki jina alikuwa ni baba yake..
"haa... Ha... Haloo mzee"
Kinana aliipokea na kusema haloo lakini huku akiwa na kwikwi za kulia
"we una nini mbona unalia?? ... Afu mbona GPS yaxngu inanionyesha upo hospitali ya india, umefata nini huko"

Je? Nini kitaendelea??...
 
KUTOKA 24:13
Mose akawaambia Waisraeli,Msiogope !,kaeni imara!Leo mtaona jinsi Mwenyezi- Mungu atakavyowaokoa,Maana hawa Wamisri mnaowaona leo,hamtawaona tena...14.Mwenyezi-Mungu atawapigania ninyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu

Hili ni neno la Imani na kila mtu kwa imani alishike..hayo magonjwa,kukataliwa,kuachwa,kufukuzwa kazi,kukosa pesa...kuuguliwa,kukwama kwa namna yoyote.hasirau,uchungu,majuto. Kukata tamaa..........hamtakuona tena..Mungu atawasaidia mnatakiwa kutulia tu kwa imani thabiti....MBARIKIWE
Awww! Asante mama mchuchu
 
KUTOKA 24:13
Mose akawaambia Waisraeli,Msiogope !,kaeni imara!Leo mtaona jinsi Mwenyezi- Mungu atakavyowaokoa,Maana hawa Wamisri mnaowaona leo,hamtawaona tena...14.Mwenyezi-Mungu atawapigania ninyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu

Hili ni neno la Imani na kila mtu kwa imani alishike..hayo magonjwa,kukataliwa,kuachwa,kufukuzwa kazi,kukosa pesa...kuuguliwa,kukwama kwa namna yoyote.hasirau,uchungu,majuto. Kukata tamaa..........hamtakuona tena..Mungu atawasaidia mnatakiwa kutulia tu kwa imani thabiti....MBARIKIWE
 
KUTOKA 24:13
Mose akawaambia Waisraeli,Msiogope !,kaeni imara!Leo mtaona jinsi Mwenyezi- Mungu atakavyowaokoa,Maana hawa Wamisri mnaowaona leo,hamtawaona tena...14.Mwenyezi-Mungu atawapigania ninyi mnachotakiwa kufanya ni kutulia tu

Hili ni neno la Imani na kila mtu kwa imani alishike..hayo magonjwa,kukataliwa,kuachwa,kufukuzwa kazi,kukosa pesa...kuuguliwa,kukwama kwa namna yoyote.hasirau,uchungu,majuto. Kukata tamaa..........hamtakuona tena..Mungu atawasaidia mnatakiwa kutulia tu kwa imani thabiti....MBARIKIWE
Amen
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom