Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mama alikaa kimya kwa kuona maneno ya sheby kuwa makali,.. Sheby aliingia ndani na kuongea na zaituni
"zai?"
"abeee kaka"
"Samahani sana zai... Sikutaka kukuambia wewe kwanza... Ila nimeongea na mama yako kakataa"
"kakataa kufanya nini"
"zai... Binafsi yangu mimi nakupenda sana na wala sitaki kujali hali ulionayo, nipo tayari kuwa na wewe kama mke wangu, lakini mama yako kakataa"
Aliongea sheby huku akiwa kama anonyesha msistizo juu ya jambo hilo, na sheby hataki kutoa taarifa ya kumseidia kuona mana linaweza lisiwezekane jambo hilo..
"lakini kaka yangu, mama yangu hana kosa,.. Nadhani anataka kukuseidia wewe na maisha yako usipate tabu.. Kiukweli mimi nitakuwa mzigo kwako, mana nitakuwa mtu wa kukaa tu, sasa hio sifa ya mke itatoka wapi kama sintojishughulisha na chochote..mkubalie mama yangu ili usipate shida katika ndoa yako"

Sheby hakuamini kama atamkosa zaituni mana nia yake ni kumseidia na sheby anajua kabisa kweli hawezi kuishi nae, lakini yeye anataka kumseidia kuona tena,..
"sawa, naona familia yote mpo pamoja.. Basi nakwenda.... Lakini pale barabarani sitaki kuluona tena, kama ni hio pesa unayopata pale mimi nitakupa mara mbili yake kila siku"

Sasa kumbe wakati mama alikuwa anasikia kila kitu,.. Yaani mwanzo mwisho mama kasikia...
"lakini kaka, kwanini nikupe kazi ambayo haikuhusu... Kama mama yangu kakataa basi"
"kwasababu nilikuwa na nia ya kukuseidia, basi nitaendelea kukuseidia hata kama mumekataa... Kwaheli"
Sheby alitoka lakini akiwa kakasirika sana, yaani hata hamu hana....
 
Lakini sasa mama aliyasikia yale maneno na kumuingia katika moyo wake,..
"sasa kama mtu kakataliwa lakini bafo tu ana nia ya kumseidia,.. Ni mtu wa aina gani huyu??... Zimetupita posa nyingi sana wakati wa uhai wa macho yake, lakini toka alipopata upofu, sijawahi kuona hata wale vijana wa kihuni wakimsalimia mwanangu.... Hakika huyu sio mtu wa kumuachia.. Kama ni pesa zao wacha iwe hivyo, lakini anastahili alichokitaka"

Mama aliongea mwenyewe kimoyomoyo huku akimfuata sheby,..
"baba... Baba Samahani sana naomba tuongee"
Mama alijikuta anapiga magoti kumuomba sheby waongee tena, mana alimkashifu kuhusiana na pesa zao, kuwa labda ni hizo pesa zao ndizo zilizotuma mwanamke kipofu..
"mama sidhani kama nitakuwa na muda tena"
"baba nisamehe sana... Naomba unisamehe... Nimekubali awe mkeo, lakini sasa...... "
Sasa sheby kuskia hio lakini... Akaona ngoja amsikilize mama huyo
Sheby alimkubalia na kumsamehe..

Tukija huku kwa akina mary wakiwa ndio wanalala, lakini mary huezi amini kumbe tayari keshampenda sheby wa watu, yaani kafa kaoza.. Hivyo kila mara yeye ni mtu wa kulikumbuka lile busu la meno alilopigwa na sheby,..
"unajua sasa utakuwa chizi wewe"
"bora niwe chizi rose... Kiukweli sijawahi kupenda toka nizaliwe, na ndio mana naiona tofauti ya kupenda na kutamani,.. Kiukweli yule kijana nimempenda dada rose.. Niseidie mwenzio"
Aliongea mary kumaanisha amseidie, mana rose na mary, mkubwa ni rose.. Mana rose anaendea miaka 25 sasa, na mary yeye ndio kaifikisha miaka 22 mwezi uliopita hivyo ni rafiki yake lakini pia ni dada yake kiumri,..
"sasa mimi nitakuseidiaje na wewe shost heeee"
"Dada Rose, mi najua kidogo una umri huenda akakuelewa eti"
"heeeeee mary siki hizi unaniita dada?? Ama kweli umependa kweli,.. Toka tuanze urafiki sijawahi kuskia hilo neno, lakini leo unalitaamka.. Basi nakuahidi nitajaribu nikishindwa basi"
"Ahsante dada angu"
Lakini sasa kumbuka hata rose ni mzuri na ana umbo la kuvutia sema anapenda kujishusha sehemu kama ile aliomuacha mary na sheby ofisini, sehemu kama zile rose hua hazipendi na ndio mana anamsukumia mwenzie ili wapate kazi kupitia mwili wa mwenzie, lakini hata rose pia ni kisu cha kukalia mbali kwa uzuri na umbo aliokuwa nalo...
"yaani nimependa mpaka naumwa yani, na kitu ambacho sikukitarajia kabisa yani"
"mapenzi ni upofu mama... Ndo ushapenda hivyo"
 
yaani nimependa mpaka naumwa yani, na kitu ambacho sikukitarajia kabisa yani"
"mapenzi ni upofu mama... Ndo ushapenda hivyo"
Lakini sasa Rose akiwa anaongea hivyo huku alikuwa kama anabinua mdomo kana kwamba hajapenda ishu kama hio... Kuna kijiba roho kinaanza kati yao, na yote hayo kisa ni mwanaume tu... Ngoja tuone mwisho wao..

Tukija huku kwa mama zaituni akiwa na sheby pembezoni mwa ukuta wa nyumba yao, wakati huo inakwenda mida ya saa nne hivi usiku, kijana sheby anazidi kuchelewa kwao bila kujua kule nyumbani wazazi wake tayari wamesha chafukwa juu yake,..
"baba... Mimi nimekubali, lakini sasa utaishi ishi vipi nae"
Aliongea mama zai huku sheby akicheka sana,
"kikubwa ni ruksa yako tu.. Na tutafanya mipango ya ndoa kabisa lakini sio sasa hivi"
"kweli una nia njema na mtoto wangu... Lakini sasa kabla ya hio ndoa yenu mtoto wangu ataishi wapi.. Mana akiendelea kuishi hapa kwangu atakufa"
Mama aliongea jambo lililomshtua sheby...
"Ati nini... Afe???... Auwawe na nani"
"sio Auwawe na nani... Ivi kumbe hajakwambia"
"aaakuuu mimi sijui... Kwani kuna nini"
Sheby alikuwa tayari kuskia sababu ya kifo kwa zaituni pindi atakapoishi hapo
"ivi unajua kiwa huyu zaituni kamwagiwa tindikali na dada yake ambae ni pacha wake"
"Whaaaat"
Sasa Sheby yeye alikuwa hajui hii ishu kama upofu wa zaituni ulisababishwa na zainabu.. Sasa leo ndio anatobolewa siri
"ndio.. Na sababu ya kumwagia ndugu yake, ni hii hii ya mambo ya wachumba... Nakumbuka kuna kioindi nilikuwa sijiwezi, hivyo nikawaambia kila mmoja sasa atafute mchumba aolewe, lakini sasa zaituni ndio aliokuwa anapata posa nyingi kuliko zainabu,.. Na zaituni yeye hakiwa akitaka kuolewa hivyo posa zote akawa anazikataa eti mpaka afikie malengo yake... Lakini sasa kumbe dada yake zainabu anaona wivu na jambo lile, hivyo alifikia hatua ya kumwagia ndugu yake tindikali ili zile posa zimjie yeye.. Sasa na wewe ukiweka nia kama hio atauwawa kabisa, mana alifanya hivyo ili asiolewe, sasa kama wewe umejitokeza baba... Afu unasema tutafanya mipango ya ndoa baadaye huoni atamuua kabisa"

"mungu wangu weeeeee....ivi una uhakika na yeye ni mtoto wako kweli"
"baba, nimewazaa mwenyewe tumbo moja na walikuwa pamoja"
"sasa si umfukuze... Kwanini ukae na mtu kama huyo.. Mtu katili kiasi hicho unaishi nae vipi sasa"
Sheby alikasirika sana kuskia kuwa yule aliotaka kumbandua kwenye gari ndio aliosababisha upofu kwa ndugu yake,..
"kumfukuza siwezi.. Kwasababu kuna vitu anafanya na bila yeye hatujui tutaishi vipi"
"kwahio upo tayari familia iishe kwasababu ya hicho kitu mama... Kwani ni kitu gani hicho"
"mmmhhhh baba,.. Tuyaache tu hayo"
"we niambie mama angu, huenda nikaweza kukuseidia japo kidogo tu"
Sheby alijikuta anaingilia majukumu mengine ambayo hayakuwa yakimuhusu kwa yeyote ile,... Mama anasita kuongea, kana kwamba jambo analofanya zainabu ni kubwa sana na hata sheby hatoliweza kulifanya...
"baba, nakuonea huruma sana... Sidhani kama utaweza baba"
Hata sheby mwenyewe alianza kuogopa kuhusiana na jambo hilo, alijikuta anarudi nyuma, kwani hata huyo mama alianza kumwogopa, mana ni jambo gani analoweza kufanya mwanamke afu mwanaume ashindwe???... Sheby aliogopa na kutia hofu kubwa sana ndani ya moyo wake.. Alihisi kuna jambo kubwa hapa...
"basi mama usiseme tena.. Tuyaache hayo mambo"
Lakini sasa kabla sheby hajataka kuondoka,... Ghafla zaituni alitokea na kusema kuwa
"mama kama hutaki kumwambia ukweli bora mimi nimwambie kuliko kuishi na jambazi humu ndani"

Itaendeleaa....
 
ac53facba13047cec0da57af6afc5329.jpg
Hahahah kha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom