"Ati nini.... Yaani unataka kumchagulia mke???... Haiwezekani baba sheby, patachimbika hapa... Mtoto wangu hawezi kuoa mtu mzima kiasi kile, haiwezekani labda niwe nimekufa"
ENDELEA........
Mama sheby alikuwa ni mwanamke mwenye hasira za karibu sana, kwani hakutaka kujua huyo mwanamke yupoje au ana umri gani,...
Kikubwa hataki mtoto wake aoe katika nyumba hio,.. Lakini wahenga walisema kuwa mwanaume ni mwanaume tu hata iweje, ila ngoja tuone hapa itakuwaje kati ya mama na baba nani mshindi wa juu ya mtoto wao,
"Enheeee, huyo huyo, anamfaa sana mtoto wetu"
"Ati nini.... Yaani unataka kumchagulia mke???... Haiwezekani baba sheby, patachimbika hapa... Mtoto wangu hawezi kuoa mtu mzima kiasi kile, haiwezekani labda niwe nimekufa"
"wewe ndio umesema hivyo, lakini sio mimi"
Aliongea baba sheby huku akiondoka tena hakutaka maneno mengine na mke wake huyo,..
Tukija huku kwa akina zaituni, sheby akiwa yupo nje na mama zaituni akiwa kamtoa kwa ajili ya maongezi zaidi
"mama, Samahani sana... Jambo hili lilihitaji mshenga lakini kwa dharura hii sidhani kama kuna haja"
"una maana gani baba, sijakuelewa"
"kifupi ni kwamba, nimevutiwa sana na mtoto wako.. Tatamani sana hata angelikuwa mke wangu"
Mama zaituni alishangaa kuskia maneno hayo ambayo hayajawahi kuskika katika maskio yake toka zaituni apate upofu, lakini leo anayasikia
"hehehehhee kijana wangu naona unanichekesha kweli... Sidhani kama litakubalika hili"
Mama aliongea hivyo bila kujua kweli sheby alikuwa ana nia na zaituni na hataki tena akaombe kule barabarani, mana keshakuwa mchumba wa mtu..
"kwani lisikubalike mama angu... Kweli mtoto wako ana sifa zote za kuwa mke,.. Namuitaji"
"ivi baba hebu nikuulize swali.. Ivi mtoto wangu unataka kumfanyia nini haswa,.. Mtoto wangu ni kipofu.. Wewe utahitaji kufuliwa nguo zako, mtoto wangu haoni... Wewe utataka upasiwe nguo zako, mtoto wangu haoni... Wewe utataka utandikiwe kitanda, mtoto wangu haoni... Wewe utahitaji unyumba, mtoto wangu haoni... Na sio hivyo tu vipo vingi vinavyotakiwa kufanywa na mke, mtoto wangu haoni... Je? Unamtakia nini mtoto wangu na wakati hawezi kufanya chochote kile ukaridhika,.. Au pesa zenu zimekuagiza mwanamke kipofu"