"ni sawa, lakini boss, je tungesoma Experience ngapi ili kila mahari tupate kazi,.. Na hizo gharama za kusoma hivyo tungelitoa wapi kama hata elimu ya kawaida ilitushinda kutokana na hali za familia zetu"
Sheby akisikia jambo la familia hua anajiskia huruma sana lakini haikuwa na jinsi,. .
"tena bora hata wewe una form six nzuri tu, lakini sasa huyu mwenzio huyu, aisee sina mpango nae kabisa.. Yaani asitegemeee... Kwa wewe rose, hebu njoo kesho tujue cha kufanya lakini jua kuwa ni asilimia 50 za kupata na 50 za kukosa"
Sheby aliongea hivyo kisha akatoka kuelekea uwani, na tayari keshawapa ukweli wao.... Mary alianza kulia kwa kukosa kazi,.. Wakati huo sheby kaelekea uwani
"mary, lakini hata mimi sina uhakika, tena bira hapa tumepokelewa vyeti, kuliko huko tulipopita hata kuonyesha vyeti tu hawataki"
"kama ni kukosa wacha nikose... Lakini mimi nikafanye kazi kiwandani kweli,.. Siamini kweli"
Mary alilalamika sana kuwa yaani yeye akafanye kazi kiwandani, mana kakosa kazi karibia ni kampuni ya tatu hio, .
"sikiliza mary,.. Kwa sasa hebu tuyaache maisha ya kuigiza, tulikuwa tunavaa nguo za maana lakini hazikuwa zakwetu,.. Nguo za mwana ndio zilizokuwa zikituonyesha kuwa sisi ni wasichana wa kitajiri,... Lakini sasa tuyaache hayo tufanye kazi"
"rose.. Ni kweli kabisa lakini"
"lakini nini??.... Sasa skia mary, mimi naondoka ila wewe baki hapa hapa.. Fanya juu chini mpaka akubali, wewe ni mwanamke bwana utashindwaje kutumia umwanamke wako"
"rose,... una maana gani kusema hivyo"
"usijifanye hujui mary, tuachane na kazi za kuigiza kuonekana matawi kumbe tunalingia nguo zawatu"
"lakini sijakuelewa rose"
"sikiliza... Hata ukimpa haondoki nacho, kikubwa upate kazi tu"
Aliongea rose kumshawishi mwenzie kuwa ajirahisishe kwa sheby ili apate kazi
"basi usiondoke rose.. Nijitahidi kufanya hivyo, lakini ni ngumu kwangu"
"jitahidi tuuuu"
Basi rose aliondoka na kumuacha mary pale ndanu ili sheby akija akutane na vimbwanga vya dada huyo,.. Haikupita muda sheby karudi, na rose yeye yupo pale reception anamsubiria rafiki yake amtege mtu huko ndani...
"heeeeee bado hamjaondoka tu"
Aliongea sheby huku akikaa kwenye kiti
"boss, nina shida na kazi"
Mary aliongea hivyo lakini kila akitaka kubinua matiti yake yatoke nje, anashindwa kufanya hivyo mana sio kawaida yake,.. Alichokiweza ni kulegeza macho tu peke yake, huku akijitahidi kupandisha suruali..
"Bosiiiiiiiiii.... Nina familia kubwa, mama yangu anaumwa, nategemewa na familia yangu boss, nisaidie kupata kazi tu, na sio lazima iwe hapa, ila kampuni yeyote ile lakini uniseidie"
Sasa chidi huruma ilimjia baada ya kusikia mambo ya familia,... Lakini kila akimuangalia mary anakuta kuna action anaziona zinaanza kufanyika..
"huyu mtoto wa kike anata kazi, na ni kweli ana shida ya kazi lakini mbona anaonekana kunitega kimapenzi hivi..... Hebu ngoja nami nimtanie kama vile nimetegeka, ili nijua kuwa yupo tayari kuuza utu wake kwasababu ya kazi au laaa"