Makapuku Forum

Makapuku Forum

"habari yako dada"
"safi shkamoo"
Alisalimia dada huyo, lakini ni kwasababu haoni, kwani laiti kama angelikuwa anaona basi asingesalimia shikamoo, lakini sheby kumuangalia vizuri aligundua huyu sio yule aliomuona supamaketi, ila wanafanana kwa kila kitu
"marahaba... Aaahh Samahani dada kama vile nilikuona pale supamaketi, ila nimeshangaa sana kukuona hapa"
Sasa swali la sheby liligeuka kuwa kilio kwa dada huyo

SASA HAPA NAKUPA STORY MBILI KWA MOJA.... NAKUPA KIPANDE CHA KABLA YA KUWA KIPOFU HUYU DADA, AFU TUNARUDI HUKU KWENYE STORY YENYEWE...

Ikiwa ni familia ya watoto watatu, ila wote walikuwa wakike tupu,... Akianza na dada yao aitwae Rehema aliozaliwa peke yake yaani sio mapacha,.. Na uzao wa pili ni wa hawa mapacha ambae mmoja wapo ni yule kipofu,...
Watoto hao walizaliwa mapacha na wapewa majina ya ZAITUNI NA ZAINABU, watoto wote walikuwa kwa upendo kutoka kwa wazazi wao, lakini upendo wao ulikuja kuvurugika baada ya kuwa wasichana wakubwa walioitaka kuolewa,...
Sasa ZAINABU akiwa na rafiki zake maeneo ya nyumbani kwao na familia hio ilikuwa ni ya hali ya chini sana hivyo wazazi wao walitamani sana watoto wao waolewe mapema kwasababu hali ya maisha ilikuwa sio nzuri.. Hivyo kwakuwa watoto wa kike walishakuwa walitaka waolewe ili wakaishi na waume zao... Lakini zainabu alikuwa ni mschana ambae hajatulia hivyo wanaume wengi walikuwa wakipita tu,... Yaani tabia za mapacha hawa zilitofautiana,.. Zaituni alikuwa mpole mpenda dini, lakini zainabu amekuwa mtoto wa mjini yeye na disco yeye na wanaume japo ni kwa siri sana,... Zainabu akiwa na rafiki zake maeneo ya nyumbani kwao wakiwa wanapunga upepo katika mti uliopo hapo kwao...

Haikupita muda zaituni alipita akiwa anatoka msikitini,...
"hhhhh ostadhati huyo umemuona"
Aliongea zainabu kumwambia rafiki yake alioko nae hapo
"ila we zai, mdogo wako mbona anapenda dini lakini wewe hhhmm"
"heeeee shost,.. Kila mtu na mambo yake bwana"
Alijibu zai huku akibinua mdomo kwa dharau, wakati huo zaituni alikuwa anaona vizuri sana... Lakini chuki alizonazo zainabu ni kuwa posa zilizokuwa zinakuja zilikuwa ni za kumhusu zaituni, na ndio maana zainabu alikuwa na chuki na pacha mwenzake,.. Tena zaituni alikuwa akiletewa poza na watu wa heshima, lakini zainabu yeye hakiwa na posa wala nini, japo walikuwa wamefanana sana lakini tabia zao ndizo zilizowatambulisha wanaume kuwa huyu ndio anafaa na huyu hafai,
"lakini zai, ina maana mpaka sasa wewe hujapata posa"
"hhhhmmm shost, posa itoke wapi na wakati hilo kahaba lipo, naona kila anaekuja tu anaulizia zaituni, najipendekeza lakini wapi analetewa yeye tu, afu mbaya zaidi anazikataa"
"heeeeeeee, anakataaa??... Kwanini"
"eti anasema yeye bado wakati wa kuolewa, na wakati mama kasema kila mtu atafute mchumba wake aolewe"
Aliongea zainabu huku akimuona ndugu yake kuwa kama gundu juu yake,
"lakini zai, kwani hao watu wanaokuja wengi wao wakoje"
"ni Waislamu tupu"
"sasa huoni upo tofauti nae,.. Wewe ni muislamu lakini huta itikadi hio, hivyo tafuta wale ambao ni taipu yako"
"sawa lakini hata hao nilio nao, pia nikimwambia swala la kuoana wanabaki kunichezea tu, ila zaituni analetewa posa tena kwa heshima ya hali ya juu"
"Nikwambie kitu shost..... Badilika dada"
"kivipi we ney"
"sikiliza, ukishajua kuwa gari yako ni ya petroli, basi anza kuwa rafiki na muuza petroli"
"una maana gani lakini"
"kuwa kama mdogo wako"
"aahhhhhh mi nashindwa kutwa kushinda msikitini yaani siwezi... Ila ili wanione kama yeye lazima nifanye kitu"
Aliongea zainabu huku akipiga chini kwa hasira
"ufanye kitu gani"
Aliuliza neema ambae ni rafiki yake na zainabu,....
"mpaka sasa hivi mdogo wangu zaituni ndio anapendwa kuliko hata mimi, yaani lazima nimfanyizie"
Hata neema aliogopa sana huku akiwa kafumba mdomo, kana kwamba zainabu alikuwa katili wa kutisha
"zai, unataka umuue ndugu yako"
"simuuwi wala nini... Ila chamoto atakiona"
"mungu wangu zai sio vizuri lakini.. Kumbuka ni pacha wako huyo"
"pacha anaenifanya nikose raha mjini, nani kasema??.... Nakwambia nakupa siku tatu tu.. Na iwe siri yako wewe na mimi tu.. Utakula vingi kama utakuwa msiri"
Aliongea zainabu na kumfanya neema kuwa na wasiwasi juu ya maneno hayo, ila neema hakuonekana kuridhika na kitu anachotaka kukifanya zainabu...

Je? Zainabu anataka kufanya nini kwa ndugu yake??...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom