Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mimi napenda sana na ninakufurahia maana hakuna mwingine anayependwa na anko wangu kushinda wewe. Anko wangu kama kocha Julio Alberto Perreira Kihwelo, yeye atazunguuka weeeeee ila mwisho wa siku Simba ndo timu yake. Nje anaendaga kusambaza ufundi
Mourinho wa bongo.. mzee wa kubwabwaja..[emoji23] [emoji23]
 
Muziki: Ulikuwa Hujui

Ninakusalimia kwa heshima kubwa Kapuku mheshimika, na kisha baada ya kukusalimia (nikiamini kabisa umerudisha salamu, maana salamu sio Salum kusalimiana) ninakuambia mimi nina adabu sana na kwa kuonesha adabu zangu sitakuuliza siku yako ilikuwaje. Nikiuliza ukajibu nami nikauliza kwanini siku yako ilikuwa ilivyokuwa utanichukia na utaona sina adabu. Toto baya kwako zuri kwa mama yake.

Kiukweli huwa ninajisikia amani sana ninapokuwa humu maana hakuna ninachokosa, well, vipo navyokosa, lakini kama ni maarifa tu, nayapata sana na hapo sijaongelea burudani maana KF kuna kila kitu na siwasifii maana nami ni timu ya Makapuku, wanaoingia na kutoka wanazidiwa na wanaokuja na kuweka makazi.

Muziki sasa, nilisema hili ni wiki la Kicongo na sina namna maana ndivyo nilivyotangaza na nikaweka bango ambalo anko wangu kajisahau kulibandika akaondoka nalo kwenda kutekwa. na nikitaja alikoelekea itakuwa msala humu na sitaki litokee hilo maana wewe Kapuku unayenisoma sasa unaifanya sehemu hii kuwa nzuri na ya kuvutia.

 
Back
Top Bottom