Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Ulikuwa Hujui

Ninakusalimia kwa heshima kubwa Kapuku mheshimika, na kisha baada ya kukusalimia (nikiamini kabisa umerudisha salamu, maana salamu sio Salum kusalimiana) ninakuambia mimi nina adabu sana na kwa kuonesha adabu zangu sitakuuliza siku yako ilikuwaje. Nikiuliza ukajibu nami nikauliza kwanini siku yako ilikuwa ilivyokuwa utanichukia na utaona sina adabu. Toto baya kwako zuri kwa mama yake.

Kiukweli huwa ninajisikia amani sana ninapokuwa humu maana hakuna ninachokosa, well, vipo navyokosa, lakini kama ni maarifa tu, nayapata sana na hapo sijaongelea burudani maana KF kuna kila kitu na siwasifii maana nami ni timu ya Makapuku, wanaoingia na kutoka wanazidiwa na wanaokuja na kuweka makazi.

Muziki sasa, nilisema hili ni wiki la Kicongo na sina namna maana ndivyo nilivyotangaza na nikaweka bango ambalo anko wangu kajisahau kulibandika akaondoka nalo kwenda kutekwa. na nikitaja alikoelekea itakuwa msala humu na sitaki litokee hilo maana wewe Kapuku unayenisoma sasa unaifanya sehemu hii kuwa nzuri na ya kuvutia.

Asanteeee binamu yangu mambo ya bunooooooo mambo ya eloko oyo acha nimchezee baba d nitarudi
 
Muziki wa Mhisani

Nimerejea tena na nimekuja kwa sababu moja kubwa, udhamini umefikia kiwango cha uhisani, yaani makaveli10 kadhamini magazeti na muziki. Hii ni level nyingine yaani katoka kuwa pedeshee hadi Bill Gates.

Na wimbo aliouhisani ni Mockingbird, wimbo mzuri kabisa kusikiza na kama unapenda mashairi yaliyopangika bila zile fakafaka za vijana nyie basi huu ndo utaupenda. Ukizitaka zile sikiza The Storm

kutoka pedeshee mpaka .....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom