Makapuku Forum

Makapuku Forum

IMG-20171010-WA0016.jpg
Asubuhi njema wadau
 
Zaburi 131

1 BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.

2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu.

3 Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.

MBARIKIWE
Amin
 
Baba katika jina la Yesu Kristo tunakushukuru umetuamsha salama tunalitukuza jina lako Takatifu .Asante kwa Asubuhi njema hii ya leo ya jumanne.
Tunaomba toba pale tulipoenda kinyume na mapenzi yako kwa mawazo,maneno,matendo na kutotimiza wajibu mbalimbali tusamehe Baba mwema twakusihi.

Tunajikabidhi mikononi mwako siku ya leo ikawe njema kwetu na tutende ya kukupendeza Mfalme wa Amani.
Tunaomba ponya wagonjwa majumbani na mahospitalini na wenye shida mbalimbali waguse ee Baba.
Tunaombea kazi za mikono yetu ukazibariki na zikawe baraka kwa wengine pia.
Tujalie Amani,furaha upendo na mshikamano.
Tunaomba Roho Mtakatifu asituache popote tutakapokuwa leo.
Tunawaombea wasafiri na wote wanaopitia changamoto mbalimbali Baba uwe nao na wakuone kwa namna mbalimbali.
Waliombali na familia zao watie nguvu na uzilinde familia zote.
Asante Baba maana utatenda sawa na mapenzi yako.
Katika jina la Yesu Kristo tunaomba na kuamini
Amen.

SIKU NJEMA WAPENDWA
 
Zaburi 131

1 BWANA, moyo wangu hauna kiburi, Wala macho yangu hayainuki. Wala sijishughulishi na mambo makuu, Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.

2 Hakika nimeituliza nafsi yangu, Na kuinyamazisha. Kama mtoto aliyeachishwa Kifuani mwa mama yake; Kama mtoto aliyeachishwa, Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu.

3 Ee Israeli, umtarajie BWANA, Tangu leo na hata milele.

MBARIKIWE
ubarikiwe sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom