Makapuku Forum

Makapuku Forum

Muziki: Kipenda Roho

Ninakusalimia kapuku mheshimika, yes, wewe tunayeheshimiana sana maana wote tuko kwenye boti moja. Aliyekaa mbele na aliyechagua siti ya mwisho kabisa wote tutafika pamoja. sema nini ujue, wenye kushuka, alokaa mbele ndo hutangulia. na kutokana na sababu hii, kwenye hafla iwe ya kufurahia au msiba huwa sikai siti za mwisho, maana huchelewi kukuta vipande vya matikitimaji na toothpicks tu. Jitahidi uwe unakaa mbele, ila sio mbele sana maana siti za mbele zina watu wao.

mara chache sana huwa inatokea nakuja kuambia 'mzee Obe' karibu siti yako iko kiti cha safu ya mwanzo kabisa, nami naamka natingisha mkono kuangalia saa kama inasoma majira kiusahihi na kubeba samsung galaxy yangu toleo jipya basi najisogeza kuungana na Makapuku wengine walio safu ya mbele kabisa. Leo nasema tu kipenda roho husema hula nyama mbichi, sasa najiuliza, kipenda mwili hula mbogamboga au.

muziki sasa, alivuma na hajawahi kuchosha kuangalia


Chenkyuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom