Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katika dondoo za bbc. ..



Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa ameilaumu Korea ya Kaskazini kwa kulazimisha vita kutokana na majaribio yake ya makombora ya mara kwa mara.

Baada ya tume ya uchaguzi nchini Kenya kutangaza marudio ya uchaguzi wa Urais kuwa ni Oktoba 17,baadhi ya wagombea waliokuwemo katika kinyang'anyiro cha nafasi hiyo awali na ambao kwa sasa hawatagombea wametishia kwenda mahakamani.

Polisi nchini Rwanda imethibitisha kummkamata mwanasiasa wa upinzani Diane Rwigara,Mama yake pamoja na dada yake kwa tuhuma mbalimbali.

Wananchi nchini Uganda wamebaki vinywa wazi kutokana na mauaji kadhaa ya wanawake,ishirini wameuawa Kaskazini mwa jiji kuu la Kampala pamoja na wilaya jirani.

Nchini Kenya Visa vya moto kuzuka katika mabweni ya shule vimejitokeza tena huku kufikia sasa shule tatu zikiwa zimeripoti visa kama hivyo chini ya wiki moja.

Ni karibu siku tano sasa kumekuwa na uhaba wa mafuta mjini Kinshasa katika nchini Kongo DRC. Baadhi ya wachuuzi wa mafuta wanatishia kupandisha bei kulingana na namna fedha ya kongo imepoteza thamani yake.

Wakati darasa la saba wakiwa katika maandalizi ya mwisho kufanya mtihani wa kumaliza Elimu ya msingi September 6 na 7 nchini Tanzania,baadhi ya wanafunzi hususan katika shule za maeneo ya visiwa, hali yao ni ya wasiwasi kuendelea na masomo.
 
Uf...
18b8101bd169db6c239b49b538b47828.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom