Makapuku Forum

Makapuku Forum

Maisha ya pale kijijini yalikuwa magumu sana kwa Kinoge na si ugumu wa kula au kuvaa bali ni ugumu wa kuchangamka na marafiki.
Hakukuwa na watoto wengi kama ilivyokuwa Dar na mambo yao yaliendeeshwa kimira sana tofauti na Dar walivyokuwa wanaishi kizungu na kujiachia sana.
Na hata alipoamishwa shuleni bado mambo yalikuwa magumu na alikosa kabisa marafiki wazuri walioendana na rafiki ake aliyemuacha Dar ambae alikuwa amemzoea kwa jina la Zungu.

Upweke uliendelea kwa Kinoge miezi mitatu zaidi kabla ya siku moja ambapo alishuhudia ugeni wa watu kadhaa nyumbani kwao walioeka kikao na wazazi wake kwa muda mrefu huku yeye akiwa amekaa nje na mtoto wa kiume aliyekuja na wale wazee ambae yeye alionekana mkubwa kuliko Kinoge na kuliko hata rafiki ake wa Dar Zungu.
"Eti wewe unaitwa nani?"
Kinoge alimuuliza rafiki ake yule mpya waliekuwa wanacheza wote pale nje.
"Naitwa Mwin-Chaa-nde umeona mjina wangu huoo!!!? wewe jee?"
alijibu yule mtoto na kumuuliza tena Kinoge swali
"Mi naitwa Kinoge."
"KINOGE!!!?"
"Eeeh"
"hahahahahahaaaaaaaaaaaa"
"sasa mbona unanicheka?!"
"Una jina la Kishaaaambaa Duh!.. Kinoge??!"
alicheka sana na kustaajabu yule mtoto wa kiume aliyejitambulisha jina la Mwinchande na kulicheka jina la Kinoge kabla wazazi wake hawajatoka mara baada ya kumaliza kikao mule ndani na kuagana nae huku Kinoge akiwa amekasirika kwa kuchekwa na Mwinchande juu ya jina lake.

Na huo ndio ukawa mwanzo wa Kinoge kukutana na Mwinchande ambae nae alihamishiwa shule ile aliyokuwa amepelekwa lakini tofauti Mwinchande alikuwa darasa la sita huku Kinoge ambae awali alikuwa anaingia darasa la tatu ila alianzishwa tena la pili kutokana na kuwaishwa sana shule.
Mazoea yao yaliyoambatana na utani ndio ikawa sababu Kinoge kutaka kubadilishiwa jina na wazazi wake ambao awali walijua ni mambo ya utoto lakini walipoona mtoto wao anang'ang'ana sana na kukosa furaha na amani shuleni na mtaani ndipo alipofika la tatu walifanya masahisho ya jina Shuleni na kumwita jina la Zainab.
Jina ambalo lilitolewa na bibiake, mama wa babaake waliekuwa wanaishi nae pale kijijini.

Kuanzia siku hiyo Kinoge alifurahi sana na kulitangaza kila sehemu jina lake jipya huku akiwa hataki kabisa mtu amwite jina la Kinoge.
Safari hii alimtambia rafiki ake yule ambae hakujua wanakoishi lakini ilikuwa kawaida kila baada ya siku mbili wazazi wake walikuwa wanakuja kukutana na wazazi wa Zai kuzungumza na katika hali ya kushangaza siku hiyo Zai alishangaa kuona wazazi wa rafiki ake wakija kwao huku mikononi wakiwa wameshika kamba zilizokuwa zinawavuta Ng'ombe wawili wakubwa na kuwaingiza katika zizi moja la miba lililokuwa awali kwaajili ya mbuzina kuwachanganya wale ng'ombe.
Awali ya yote Zai alikuwa hajui nini Kinaendelea kwani mifugo ilizidi kuletwa taratibu na hatimae baada ya mwaka mmoja lilijengwa zizi kubwa lililokuwa na Ng'ombe sita sambamba na mbuzi wanane wote wakiwa wameletwa na wale wazazi wa yule rafiki ake wanaetaniana taniana aliyeitwa Mwinchande ambae mwaka huo ndio alikuwa yupo darasa la saba huku Zai akiwa darasa la tatu.

Kumbe nyuma ya pazia kilichokuwa kinaendelea na ambacho kimeongelewa na wazazi wa pande zile mbili ni juu ya kuwaunganisha watoto wao ili watapokuwa wakubwa waishi pamoja.
Na hivyo wazazi wa Mwinchande walikuwa wanalipia kabisa mahali ya mtoto wa bwana Juma ambae ni Zai ili awe mke halali wa mtoto wao wa kiume ambae ni Mwinchande.
Habari ile ambayo kumbe hata Mwinchande alikuwa anaijua na pindi alipokuwa anamwita Zai mke wangu nae Zai akimwita Mwinchande mume wangu akihisi ni utani tu bila kujua kuwa tayari kuna ukweli ndani yake hadi siku moja alipoitwa na wazazi wake na kumwambia kuwa anapaswa awaheshimu sana wale watu aliokuwa anawaona wanakuja na Ng'ombe pale nyumbani kwani wamelipia gharama za yeye kuja kuishi na Mwinchande baadae pindi atapomaliza masomo yake.
Ilikuwa ni kawaida kimila kipindi hiko kuwaoza watoto wangali wadogo japo serikali ilipiga marufuku suala hilo na kuwapa adhbu kali kisheria wale waliobainika kuwaoza mabint zao wangali watoto lakini pia ilikuwa ngumu kuwagundua kama ilivyokuwa kwa Zai na Mwinchande ambao wazazi wao waliwahimiza kuhusu shule.

Baada ya shughuli za kimila kukamilika kipindi hiko Mwinchande alimaliza darasa la saba na Zai ndio alikuwa anaendea darasa la Nne waliunganishwa kwa kufungishwa ndoa ya siri nyakati za usiku na kuanzia siku hiyo kila mmoja alipewa nasaha na kuonywa na wazee kuwa asije kuthubutu kumtaka mtu mwengine wa kuishi nae hapo baadae kwani tayari wao ni mke na mume na watapokuwa wakubwa hawataoana tena bali wataishi pamoja na kuanzia siku hiyo jukumu la huduma za Zai lilisimamiwa na wazazi wa Mwinchande.

* * * * *

Mikosi ilianza kumkumba Hussein miezi michache baada ya kumpoteza kwa kuhama rafiki ake kipenzi aliyekuwa akitaniana nae kama mkewe na hatimae babaake kipenzi ambae ndie aliamini rafiki wa ukweli nae alifariki dunia.

lilikuwa ni zaidi ya pigo kwa mtoto Hussein japo ndugu wengi walitaka kumchukua lakini hatimae aliondoka na mamaake ambae nae haikupita miezi mitatu alifariki ghafra na kuzidi kuongeza pengo la uyatima moyoni mwa Hussein na hapo ndipo alipochukuliwa kulelewa na mjombaake kaka wa mamaake lakini bado hakuwa tena na furaha kwa kuwapoteza wazazi wake mfurulizo namna ile pia aliumizwa mno na maneno ya watu yaliyokuwa yanasemwa mitaani kuwa wale wazazi wake wote walikuwa na virus vya Ukimwi na ndio ilikuwa chanzo cha kuachana kwao miaka mitano iliyopita.
Aliumia sana Hussein kwa kuwa tayari alikuwa darasa la nne na mambo ya Ukimwi walishaanza kufundishwa tokea darasa la tatu na alijua kuwa ni ugonjwa m baya na wa aibu mtu kukutwa nao kwa hiyo wanaohadithia wazazi wake walikuwa na ugonjwa huo aliwachukia sana na kuwaona ni watu wabaya upande wake.

Maisha na kwa Mjomba hayakuwa ya kudumu sana baada ya kuchukuliwa na babaake mkubwa aliyekuwa mganga wa kienyeji lakini huko nako alikaa muda mchache kabla shangazi yake kumchukua baaaaasi ilimradi Hussein alikua kwa kulelewa kama mpira wa kona mpaka ile siku alipowashangaza watu kwa kusema anataka aishi mwenyewe kwenye nyumba ya kupanga.

... Maisha yalienda ilimradi siku zinaenda na Hussein alisoma kwa Shida mpaka anamaliza darasa la saba hapo ndipo alipoanza kuhangaika mitaani kufanya kazi mbalimbali ili mradi mkono uende kinywani na hakuchoka kujituma.
Muda wote alipenda kujichanganya na watafutaji wenzake huku akiwa na ndoto siku moja maisha ataweza kuyamudu nae kujenga nyumba kutimiza mawazo ya babaake ambae mpaka anafariki hakuweza kuwa na nyumba japo alitamani kufanya hivyo.

Wahenga walisema 'Mungu hamtupi Mja wake' na ndivyo ilivyokuwa kwa Hussein miaka sita baada ya kuhitimu darasa la saba alibahatika kupata kazi kwenye kampuni moja ambayo iliweza kumlipa pesa zilizomuwezesha kuyamudu sasa maisha yake na kuheshimiwa hata na baadhi ya ndugu zake kwa juhudi alizozionesha na hapo sasa alianza kuyafurahia maisha.

Kipindi hiko alikuwa ana umri wa miaka 21 na hapo ndipo alipoanzisha mahusiano na msichana mrembo aliyeitwa Mariam huku akiwa kasahau mambo mengi ya utoto akiwemo yule rafiki ake wa utotoni aliyeitwa Kinoge.
Mapenzi yake na Mariam yalikuwa mazuri mwanzoni lakini baadae kidudumtu kiliingia mara baada ya mwaka mmoja wa mahusiano yao pindi alipokuwa anaangalia kipindi cha YA WALIMWENGU kupitia Becker TV ambapo kulikuwa na mada ambayo msimuliaji alilaani kuwa Wanawake ni Wauaji.
Mada hiyo ndio iliyompotezea muda Hussein na kusahau juu ya ahadi ya kukutana na mpenzi wake yule ambae tayari karibu robo tatu ya ndugu zake walishamjua.
Ugomvi wao wa ghafra uliosababishwa na kile kipindi mara baada ya Mariam kufika pale kwa mchumbaake na kukuta muda mwingi akiwa bussy na tv kuliko yeye na zaidi alichefuliwa na kile kipindi hali iliyomfanya Mariam aondoke kwa hasira na katika kumtafuta kwake Hussein kwa mara ya kwanza ndipo alipoyaelewa maneno ya kile kipindi mara baada ya kuchezea kichapo cha aibu ndani ya fukwe za coco pindi alipomfumania Mariam akiwa na mwanaume mwengine na hapo ndipo alipoapa kutopenda tena, lakini mapenzi yana nguvu sana na hii ilidhihiri mwaka mmoja baadae baada ya maisha ya kibachela walipopata safari ya kikazi Arusha huko ndipo alipokutana na msichana ambae awali alitokea kumuota kabla hawajaonana kweli akiwa na rafiki ake.
Msichana huyo ndie Zai kama alivyoota lakini hakuwahi kufikiria kama Zai yule ndie Kinoge rafiki ake wa utotoni.

* * * * *

Kwa upande wa maisha ya Zai mara baada ya kuozeshwa kimila akiwa bado mtoto maneno ya wazee na wazazi wake yalimjengea hofu ya kuja kukiuka kuwa hajaolewa au kuwa na mwanaume mwengine.
Na kwa hali ile ilibidi ampende zaidi Mwinchande na hasa mara baada ya wazazi wake kufariki kwa ajali mbaya ya gari iliyotokea Arusha mjini na hatimae Zai alibaki yatima pindi akiwa darasa la sita wakati huo Mwinchande alikuwa kidato cha tatu akisomea Arusha mjini na ilikuwa kila mwisho wa wiki alirudi kijijini na kuleta zawadi mbalimbali kwa mkewe ambae nae sasa alikuwa anaelewa nini maana na aliamini kuwa Mwinchande ndie mumewe na hana uwezo wa kupinga hilo.
Alisahau kabisa habari za Hussein ama Zungu kama alivyopenda kumwita mwenyewe na aliridhia ndani ya moyo wake pindi atapomaliza masomo kuishi na Mwinchande kama ilivyo mipango kwani alikuwa tayari ni mumewe.
Lakini kipindi cha kiangazi watu wakiwa katika kuandaa mashamba bahati mbaya lilitokea janga la moto pale kijijini.
Moto ulioacha misiba ya kihistoria na huzuni kubwa kwa wanakijiji mara baada ya nyumba nyingi kuungua na mifugo ikiwemo nyumba ya kina Mwinchande ambapo msiba mzito ulitokea mara baada ya wazazi kushindwa kujinusuru na kuteketea huku Mwinchande pekee ndie akisalimika halikadhalika kwa kina Zai napo bibi pamoja na mjukuu wote walifanikiwa kutoka salama japo nyumba yao na zizi vyote viliungua.

Ulikuwa ni zaidi ya msiba kilio kila kona serikali na manispaa ya jiji la Arusha waliwasaidia wahanga wa moto na kuwatengea eneo kulekule kijijini.
Kwa upande wa Mwinchande alikuja Shangazi yake aliekuwa anaishi jijini Dar na kujitolea kuondoka nae kumuendeleza kielimu Huko japo shangazi alijua kuwa tayari mwanae ana mke aliyeozeshwa kimila lakini alipuuzia na kuona ni mila potofu na ndio sababu ya kumuacha Zai aendelee kusoma pale kijijini na hata siku Mwinchande anaondka na Shangazi ake mara baada ya kumaliza misiba bibi alimpa moyo mjukuu wake Zai kwa kumwambia asiwe na wasiwasi mumewe anaenda kutengeneza maisha yao na atarudi kumchukua.

Lakini mambo yalizidi kwenda kombo baada ya miaka kuzidi kupita toka kuondoka kwa Mwinchande na shangazi yake huku maisha pale kijijini yakizidi kuwa magumu mpaka pale alipomaliza darasa la saba na kujikuta akikaa zaidi ya miaka miwili mbele bila kuuona uso wa mumewe hadi siku moja alipokuwa katika mizunguko Arusha kipindi hiko alikuwa na umri wa miaka 17 alistuka pindi alipoitwa jina na mtu asiyemfahamu japo kwa mbali sura yake haikuwa ngeni ila alificha.
Hakujua mwnzo kama yule ndie Zungu wake kipindi cha utoto na Zungu hakujua kuwa yule ndie Kinoge wake wa utoto na kwa bahati mbaya hayo majina yalikuwa yashakufa kwao wote. Zungu alifahamika zaidi kwa jina la Hussein ambalo Kinoge alikuwa hajalizoea na Kinoge pia alifahamika kwa jina la Zainab ambalo Zungu hakuwahi kulisikia kabisaaaaa.
...

Baada ya kukutana na yule kijana ambae hakutaka kumwambia jina lake alilijua vipi wakati hawajawahi onana Zai aliondoka huku akiwa na namba ya simu ya yule kijana ambae alimsihi na kumwambia atapompigia ndipo atamwambia amelijuaje jina lake.
Na kutokana akilini mwa Zai kuhisi kama kuna taswira ilikuwa inamjia juu ya yule kijana hakusita sana kuichukua ile namba huku akiwa nae anaumiza kichwa pindi alipoondoka kufikiria wapi aliwahi kumuona yule mtu.

Lakini kwa bahati mbaya alipofika nyumbani alisahau kabisa ile namba mara alipoiweka kwenye begi na yote ilichochewa na mawazo mengine aliyokuwa nayo juu ya mumewe Mwinchande kwani licha ya uzuri aliobarikiwa Zai lakini bado aliweza kujidhibiti na kujitunza kwa wanaume mbalimbali akikwepa vishawishi akiamini yeye ni mke wa mtu lakini huyo mumewe amekuwa mpotevua na miaka ikawa inazidi kupogoma.

* * * * *

Walionekana vijana wapya wa polisi wakiwa wanapangiwa maeneo baada ya kuhitimu mafunzo ya pili ya jeshi la polisi na kuajiliwa kuwa askali rasmi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Kila mtu alifurahi pindi majina yalipokuwa yanatajwa na mahala husika ambapo miongoni mwa majina ya wale askari wapya lilisikika jina la Mwinchande na mahala alipopangiwa ambapo ilikuwa ni mkoa wa Pwani Kibaha.
Alikuwa ndie yeye Mwinchande mume wa Zai mara baada ya kusoma mpaka kidato cha sita na kwenda kujiunga na jeshi la polisi baada ya kufanyiwa mpango na shangazi yake.

Nyota ilikuwa upande wake Mwinchande toka ajiunge na jeshi la polisi kwani baada ya mwaka mmoja zilitokea nafasi adhimu ya vijana watano waliohitajika kwenda israil kuchukua mafunzo mapya yaliyokuwa yanatolewa jinsi ya kupambana na waharifu wanaotumia akili nyingi tofauti na zile mbinu zilizokuwa zinatumiwa na nchi nyingi za kiafrika hususani Tanzania walichofundishwa ni jinsi ya kumdhibiti na kupambana na muharifu kwa utumia nguvu zaidi na silaha inapobidi.
Nafasi ilikuwa imetolewa kila nchi askari watano na kwa bahati nchi ya Tanzania miongoni mwa askari wengi walioomba hiyo nafasi, mwisho wa siku majina matano yalivyotoka na jina la Mwinchande lilikuwa miongoni mwa Askari wanaohitajika kwenda huko Israel ambapo kozi nzima ilikuwa ni ya miaka miwili.

Na huo ndio ukawa mwanzo wa Mwinchande kuvuka mipaka ya nchi na kuzidi kutanua milango yake ya kufikiri na kujengeka fikra pana huku moyoni mwake akimkumbuka mke aliyeozeshwa na wazazi wake na mara zote Mwinchande aliamini yule ndie mkewe na hatoolewa na mwengine kwa kuwa wao hawakuachana.
Na kwa jinsi alivyokuwa anamchukulia Zai moyoni na kumpenda aliamini atamkuta tu hata kama atakaa zaidi ya miaka mitano huko Israel na hii ilimpa moyo kutokana kabla hajaondoka alimpa maagizo rafiki ake aliyekuwa mganga wa kienyeji ambae alifahamiana nae mara baada ya kuugua ghafra kipindi akiwa mgeni pale pwani na kuonekana matatizo yaliyomkumba yalikuwa ni ya kienyeji baada ya watu washirikina kumjaribu na hapo ndipo alipopewa msaada na mkuu wake wa kituo ambae alikuwa ni Inspector Cyplian kwa kumpeleka kwa mtaalam wa mitishamba na ramli aliyesifika ambae alikuwa anapatikana katika kijiji cha Hakipo kilichokuwa maeneo ya Kibamba pembezoni kabisa mwa jiji la Dar.
Hapo ndipo urafiki wa Mwinchande na Mganga yule ambae alifahamika kwa jina maarufu la Mnyungunyungu ulianza baada ya kuwa anamtembelea mara kwa mara na hata zilipotokea zile nafasi alimlilia Mnyungunyungu aangalie uwezekano wa kulifanya jina lake ling'ae na liwe miongoni mwa majina yatayochaguliwa kwenda kwenye hiyo kozi.
Na kweli jina lake lilipotoka Mwinchande alizidi kuamini kuwa Mnyungunyungu kweli ni kiboko na ndio kikawa chanzo kabla hajaondoka alimuhadithia kila kitu kuhusu mkewe aliyeozeshwa angali shule na alimuomba Mnyungunyungu afanye dawa ambayo itamuwezesha pindi atapoonana na yule mkewe asije kubadilika yaani ampende vilevile kama zamani hata kama kuna mwanaume atakuwa kashaingilia kati kipindi yeye hayupo.
Na hili ndilo lililomuaminisha Mwinchande ambapo pia alimuomba shangazi yake kama atapata muda aende akamchukue mkewe kule kijijini japo alijua kwa Shangazi yake kufanya vile itakuwa ngumu kutokana yeye hakuipenda kabisa ile mila iliyotumiwa.
Na baada ya wiki kadhaa toka uteuzi ule ufanyike hatimae ndipo Mwinchande alipoungana na wenzake kwa safari hiyo ya nchini Israel kwaajili ya hayo mafunzo maalum.

* * * * *

Siku zilikatika kwa upande wa Zai maisha ya kusubiri yalizidi kumchosha lakini bibi ndie alikuwa mstari wa mbele kumsihi na kumpa moyo kuwa mumewe atarudi tu kwani ile ni mira na haivunjiki kamwe.
"Bibi mi sidhani kama kweli Mwinchande atarudi kunichukua wakati huko mjini nasikia kuna wanawake wengi wazuri kama nini.."
"Hapana mjukuu wangu Zainab Mwinchande ni wako, yule ni mume wako.. Atarudi tu kukufata wee subiri mjukuu wangu, kikubwa ni kuzidi kujisitiri na kusali kila siku.. Usiache kabisa kusali na kumuomba Mungu yeye ndie mjuzi."
alisisitiza sana bibi Zai mara Zai alipokuwa anahoji juu ya suala lile la kurejea tena kwa Mwinchande.


Lakini baada ya muda tena ndipo ilipokuja barua pale kijijini iliyotokea jijini Dar ikimtaka Zainab afanye safari ya kwenda huko ambapo anaishi mumewe.
Na barua iliandikwa na shangazi wa Mwinchande mara baada ya kuona Mwinchande akimuulizia sana juu ya kumfata huyo mkewe ambae yeye hakumpenda kabisa wala kumuhitaji kwani alihisi kile kilichofanyika ni dhulma tu kuwachagulia watoto wanaume/wanawake wa kuishi nao.
Lakini aliona kwa kuwa Mwinchande mwenyewe king'ang'anizi, aliamua kutuma tu hiyo barua kama ataweza huyo bint aende kama atashindwa basi na ndani ya barua pia kulikuwa na namba yake ya simu.

Moyo wa furaha ulimripuka sana Zai baada ya kupata ile barua na kufanya mawasiliano na shangazi mtu.
Nahapo sasa ilibaki kazi ya kufuafua na kujiandaa kwenda Dar es salaam jiji ambalo aliondoka akiwa bado mtoto na toka miaka hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kurejea tena jijini.
Lakini wakati akipekuapekua ndipo alipokiona kile kikaratasi chenye namba za simu za yule kijana aliyewahi kutana nae siku moja na hapo ndipo alipokumbuka kumpigia akiwa na shauku ya kujua alimjuaje? kwani upande wake alishindwa kabisa kumkumbuka vizuri.
Mara baada ya simu kupokelewa na Zai kujitambulisha alimuuliza tena lile swali huku akimuomba amwambie walipoona na hadi kumfahamu kwani hawatoweza kukutana tena kutokana na safari yake ya jijini Dar.
Lakini alishangaa baada ya yule kijana nae kumwambia kua yuko huko huko Dar na pindi atapofika basi wataonana na atamwambia alimjuaje.

....
 
Uf...
1fafb0a08cd4c5ef661ceee50fba2706.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom