Makapuku Forum

Makapuku Forum

THE DOM

Sehemu Ya 15

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Instagram....

Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←

SON OF PRESIDENT GU

Na rais hataki mtoto wake ajue kama anamtumia sahi kama mpelelezi mkuu nchini, na wakati huo sahi yupo kambini.... Joseph ni mpelelezi aliosomea nchini hivyo ana utaalamu wa hali ya juu,... Kwanza alishangaa kuona jumba hilo kuzungukwa na kamera kila kona, Joseph alichukuwa laptop yake kisha akachukuwa number ya kamera moja wapo, ili azime, lakini alishangaa hazizimiki hata moja...
Sasa GU anatamani kumpigia simu mtoto wake kuwa atoke katika nyumba hio, lakini sasa hatakiwi kujua kama rais na sahi wana ukaribu mzuri sana.... Mzee GU hakutaka nyumba hio isachiwe....

Ghafla simu ya Joseph inaita, kuangalia jina liliseviwa BABA... Maana yake ni rais ndie aliekuwa akimoigia, na wakati huo wanafanya mbinu za kufungua mlango....
"hello mr President"
Joseph alikuwa na utani sana na baba yake, pale wanapoongea kwa simu,...
"unaweza ukaniambia ruksa ya kuingia hapo ulipewa na nani"
Joseph alishtuka kuskia hivyo, tena alitoa macho huku akijua kuwa tayari keshakuwa JIPU.....

ENDELEA.........

Jumba hilo lilijengwa maalum kwa ajili ya sahi, yaani sahi akiwa yupo nchini Korea, huku Tanzania anajengewa jumba lake spesho kwa ajili ya kazi yake ya upelelezi,... Licha ya akina Joseph kwenda kuipeleleza nyumba hio, lakini wasingeweza kuingia katika chumba cha sahi, mana mlango uliopo katika chumba hicho hauwezi kuuona mana umefanywa kama ukuta, hivyo unaweza kuona ni muunganiko wa ukuta lakini kumbe papo hapo ndipo mlango ufike, na ili ufunguke kina mahali unagusa ndipo ufunguke, hivyo hata akina Joseph wangeliingia wasingefanikiwa chochote, mana vyumba vingine havina vitu zaidi ya vitanda na meza tu...

Sasa Joseph na watu wake wakiwa katika nyumba hio, na ukumbuke kuwa nyumba hio ina kamera kila kona, na system ya kamera hizo zimeunganishwa mpaka Ikulu katika ofisi ya rais, na licha ya ofisi ya rais pia sahi ameiunganisha katika laptop yake, sema kwa wakati huo alikuwa akiangalia kamera inayorekodi tukio la General wakati akiwa anauza dom kwa gharama ya shilingi bilioni 500, na hio sio bei ya hio dom, bali inazidi mara 10 hapo... Lakini kwakuwa hawataki iwapotee mikononi mwao hivyo waliamua kuuza kwa bilioni 500, unajua kitu cha kuiba hakina bei sahihi, tena kinauzwa kwa hasara mno....

Sasa mzee GU kaamua kumpigia mtoto wake simu ili asiingie katika jumba hilo
"hallo mr President"
"unaweza kuniambia ruksa ya kuingia hapo ulipewa na nani"
Joseph alishangaa, ina maana baba yake anaona kila kitu...
"ni nyumba tulio ihisi vibaya hivyo ni lazima ikaguliwe"
"kwa amri ya nani"
"kwa amri ya kitengo cha TSS"
"haraka na muondoke eneo hilo"
Sasa Joseph hua hamuogopi baba yake yaani kutii amri yake ni ngumu sana hivyo aliikataa amri ya baba yake na kuingia ndani
"jamani, tu ingieni mpaka tujue kila kinachoendelea"
Aliongea Joseph huku akiwaamuru vijana aliowazidi cheo, yaani walio chini yake...

Mr GU kuona mtoto kakiuka amri yake, alipiga simu kwa sahi....
"GU"
Sahi kusikia neno GU alijua ni President GU, alimwangalia mwajua kama vile kalala, kisha akaipokea simu ya mr GU,
"yes mkuu"
Lakini kumbe mwaju hakulala, yaani alikuwa kama anamchezea akili sahi, na ndio mana sahi aliambiwa asipendelee kuwa na mwanamke wakati wa kazi zake...
"huoni kinachoendelea katika nyumba yako"
Aliongea raisi GU huku sahi akishtuka na kutafuta system ya nyumba yake,
"kuna nini mkuu"
"TSS wamevamia"
Kweli sahi kuangalia anaona watu wakiwa wanasachi kila chumba, na mlango wa kwanza hajui wamefungua vipi, na wakati unakwenda kwa finger print...
"wamefunguaje huu mlango"
Sahi alimuuliza mheshimiwa lakini nae pia hajui, mana TSS ni kitengo makini sana sema rushwa imetawala katika serikali yetu,..
Sasa sahi anamuona Joseph akiwa anatafuta chumba cha sahi, ukumbuke kwamba chumba cha sahi ni cha utofauti sana, mlango wake hauonekani, sasa hapo Joseph ndipo anapo changanyikiwa kwa kukosa chochote katika jumba hilo,... TSS walikata tamaa sasa wakawa wanatoka kiunyonge sana, mana hawakupata lolote litakalo wasaidia kumjua sahi ni nani,... Lakini sasa Joseph aliookuwa anatoka, kwa bahati nzuri akagusa ile sehemu ambayo ikiguswa mlango hufunguka,. Kwanza walikaa atesheni mana walijua kuna mtu kafungua, walishangaa sana mlango uliofanana na ukuta,... Sasa hapo umefunguka lakini kuna mlango wa ndani yake huo ni mpaka finger print,... Yaani huezi amini Joseph alikuwa kavaa nailoni fulani katika kiganja chake na hio inasadikika kuwa ni finger print za sahi sasa sijui walizipata vipi... Ukiwa na finger hizo popote kwenye mlango wa mtu husika unafungua bila shida.... Joseph ndani ya chumba cha sahi, alishangaa kuona kuna vitu vya hatari sana hasa mambo ya upelelezi... Joseph hapo ndipo mahali alipo pataka, sasa ukumbuke katika chumba cha sahi hakuna kamera hivyo hata sahi mwenyewe hawezi kuona mana kamera ya chumba hicho ilitolewa hivyo hatoweza kuona kinachoendelea..
Joseph aliona kila kitu, lakini sasa alipoangalia kwa juu akaona kile kibegi ambacho kuna siku alimwona nacho akiwa kakibebea dom original, alipoangalia ndani ya kibegi hicho aliona hard drive tu basi, lakini dom haikuwepo,.. Ukumbuke kuwa dom iliibiwaga na changudoa hivyo mpaka sasa sahi hajui kama dom iliiniwaga mana anaamini ipo mule katika kibegi chake,... Joseph aliachana na kibegi kile baada ya kuona vitabu vingi sana vikiwemo vitabu vya kijeshi vya korea na vitabu vya shule ya upelelezi nchini korea...
Alipoangalia vitabu hivyo, ndani yake kulikuwa na picha zikimuonyesha akiwa jeshini, Joseph alizidi kupekua na kukuta picha akiwa anatunukiwa shahada ya uwanafunzi bora wa Afrika mana hakuwa yeye tu katika jeshi hilo na hakuenda kwa ajili ya kazi, bali alikwenda kusomea ujeshi tu kisha arudi nchini kwake, mana kila nchi inatengeneza jeshi lake sasa kama kuna muafrika basi ujue amekwenda kuchukuwa mafunzo ya kijeshi ila sio kuitumikia nchi hio... Sasa Joseph alipozidi kufunua kurasa alikutana na picha ya mama yake sheby, yaani mke wa General,..
Joseph alishangaa sana kuona picha ya mama wa rafiki yake sheby ikiwa ipo katika mazingira ya kijana huyu,..

Sasa huku mzee anasikia sauti ya sahi ikisema
"ni mtoto wako, unashindwaje kumzuia"
"tatizo yupo ndani ya kazi yake sasa hata nikimzuia atatuhisi na istoshe tayari keshajua kuwa nami naiona nyumba yako"
"ivi unajua kuwa mtoto wako nae ni jipu"
Aliongea sahi wakati huo mwaju nae yupo karibu anasikia kila kitu,
"unasemaje???... Ana kosa gani"
"nae anahusika na wizi wa dom"
"what, hio taarifa uliipata muda gani"
"nina wiki moja niko nayo"
"kwanini hujaniambia"
"nilikuwa nalifanyia upelelezi kwanza"
"basi... Lazima nilifanyie kazi, wacha niandae sindano"
Mzee GU aliongea hayo mana ni mzee wa majipu, kukutumbua hua hachukui muda mrefu, ni dakika tu tayari umeshakuwa jipu

Sasa huku kambini General ndio anarudi akiwa kabeba begi kubwa liliojaa pesa,... Magari kama mawili yalio ongozana, gari moja general ndani gari ya pili ni watu wanaoshirikiana nae, yaani baadhi ya makamanda wake wanaomsikiliza.. Mwaju alipo hisi General kafika kambini, aliomba kutoka zake nje mana viongozi hawataki wanawake au wanaume kuwa na wanawake kwasababu watakuwa dhaifu katika mazoezi pindi watakapo endekeza mapenzi,.. Sahi hajui kama mwaju alitumwa na sijui ni kwanini sahi kamuamini mwaju kwa haraka kiasi hicho, ama kweli wanawake ni watu hatari sana katika upande wa kazi, sasa sahi anataka kuchepuka hapo kambini ili kuwahi jijini Dar es Salaam, na usafiri wake ni wa ndege ili kuwahi katika nyumba yake,... Sasa akiwa ndani anajiandaa kwenda, wakati huo mwaju anamwaga siri zote alizozipata katika chumba cha sahi, alimwambia kila kitu kuwa alirekodiwa hio safari yake
"mkuu,.. Kwanza nahisi huyu ni mtoto wako... Kwasababu sasa hivi nimetoka kushiriki nae, ni mtoto wako kabisa kasoro hio sura ndio havifanani.... Afu kingine, hii safari yako unayotoka sasa hivi, tulikuwa tunakuona kupitia laptop yake... Afu nilisikia akiongea na mtu lakini hakuwa akitumia simu ya kawaida... Huyu kijana ni mpelelezi"
Mwaju aliongea kila kitu, lakini General alicheka sana huku akimshukuru mwaju kwa kazi alio ifanya, pale pale alipewa kitita cha pesa kisichojulikana, yaani hata kukificha alishindwa,.. Mwaju alitoka hapo na kwenda katika chumba chake kuzihifadhi... Wakati huo sahi anajiandaa ili atoke kuelekea jijini Dar es Salaam, yaani kama liwalo na liwe, na kama ni kujulikana wacha ajulikane tu... Ghafla General anapokea simu yoka kwa Joseph
"halo JJ habari yako"
"safi mkuu.... Aisee mkuu tumeumia tayari"
"kwanini"
"huyu mtu ni mpelelezi, na istoshe ni mwanajeshi mwenye taji la uwanajeshi bora Afrika Mashariki kwa wale waliokwenda kuchukua mafunzo nje ya nchi"
"ina maana huyu kijana ni mwanajeshi"
"sio mwanajeshi tu, bali ni mwanajeshi bora Afrika na mpelelezi mwenye kiwango cha hali ya juu mno, mana kuna vitabu hapa naviona ni vitabu hatari sana,... Huyu mtu sio wa kawaida eti"
"umefanikiwa kuingia nyumbani kwake"
"ndio, nipo hapa ndani kwa sasa"
Sasa General alipoangalia nje anamuona sahi kwa mbali akiwa kabeba begi....
"hebu ngoja kwanza naona anatoka"
"sikiliza kwanza mkuu... Afu sasa mbaya zaidi, anashirikiana na baba"
"Whaaaaat..... Unasemaje Joseph"
"anashirikiana na mr President GU
"mungu wangu.... Hebu subiri naona anatoka kambini"
"mzuie, yaani hapo ataondoka na siri zetu nyingi na bila hivyo tumekwisha"
Simu ilikatwa huku Joseph anazidi kupekua huko ndani, yaani mpaka aone vingine, kumbe walikuwa wakishirikiana na mtu ambae anamilikiwa na raisi,..

Sasa sahi bila kujua anatoka kambini tena wakati huo keshajipanga, na hua anatoka wiki yake ya kambini ikiisha anaruhusiwa kutoka kwa mujibu wa sheria kwa upande wake yeye,.. Lakini sasa wiki yake bado haijaisha
Sahi alishangaa anazingilwa katika geti kuu,... Alishangaa makamanda wakubwa tena wa shoka wakiwa wanajitokeza kila kona, sahi akiangalia nyuma yake kuna makamanda wasiopungua 10, akiangalia mbele kuna makamanda wasiopungua 10, kushona na kulia ni hivyo hivyo, mana hapo ni kambini makamanda ni wa kumwaga.... Sahi alikuwa amebeba kibegi chake mgongoni, aliwaangalia makamanda zaidi ya 50 wakiwa wamemzunguka.. Hajakaa sawa mara General Nyange katokea huku akisema
"sijawahi kuona mtoto anaempeleleza baba yake"
Aliongea general akizani kuwa ni mtoto wake
"ulizani kwa maneno hayo utaachwa"
"haijalishi... Lakini nami sintokuacha hai hata kama unasemekana ni mtoto wangu,.."
Sasa generally akiwa anaendelea kuongea mara simu yake inaita... Kuangalia jina alishtuka sana,...
"hallo boss"
Aliongea general huku akiiskiliza kwa makini sauti hio
"kwanini umeniuzia Discate feki... Unataka kuanzisha vita na mimi..."
Aliongea yule mzungu aliouziwa dom masaa machache yaliopita,..
"unasemaje boss"
"dom ulionipa ni feki haisapoti kwenye mashine yangu... Sasa nakupa masaa sita, nisipoipata hio original dom, shingo yako ni halali yangu, washenzi wakubwa nyie"
"basi boss, niongezee masaa sita mengine"
"kesho saa sita dom nisipoipata, weka tayari shindo yako... Pumbavu sana, bilioni 500 unanipa dom feki??"
General kwa hasira alikata simu kisha akamuangalia sahi kwa hasira, huku akimfuata pale alipo..... Kambi haijamjua sahi vizuri kuwa ni nani na ana uwezo gani.....

Je? Nini kitaendelea???.. Nani atafanikiwa kuwa na dom original, mana dom ilishaibiwa takribani wiki imeisha sasa na haijulikani ilipo...

ITAENDELEA.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom