Haya hii happa
THE DOM
Sehemu Ya 13
Mtunzi..... MoonBoy
Simu No. +255714419487 WhatsApp
Instagram....
Ilipoishia Jana →↓↓↓↓←
SON OF PRESIDENT GU
bi shot uyooo anarudi kazini"
Waliongea rafiki zake na kumpigia makofi,....
"Afadhali hata umerudi mwenzetu... Mana sisi jana hatujapata hata mwanaume wa dawa... Jana wake zao wamewabana waume zao ndani"
Ghafla wanashangaa kifaa kimetupiwa mezani,.. Ilikuwa ni dom,
"sasa ndio nini hii"
Aliongea dada mmoja huku wakikiangalia
"mwenzangu we.... Hata mimi sijapata kitu... Hiki ndicho nilichokiiba kwa huyo mkaka... Na kazi hii sitaki tena"
"heeeeeee... Sasa utakaaje hapa kama hutaki kazi"
"nashangaa anajishauwa tu apa, toka juzi unakula nguvu zetu.... Haya chukuwa jichuma lako ukaliuze na utuleteee pesa hapa, sio tukuleee tu we sio mtoto wetu Bwana"
Aliongea member wa kundi hilo huku akimtupia ile dom aende akaiuze alete pesa.... Laiti wangelijua kuwa hicho ni kifaa kinacho tafutwa na serikali, wasingekitupa hicho... Na bei yake ni mabilioni ya fedha,...
"sasa nikakiuze shilingi ngapi"
"wewe ulioiba ndio unajua thamani yake.... We tuletee hata elfu 20 tupate ya kula leo"
ENDELEA..........
Ama kweli usilo lijua ni usiku wa giza, ikiwa na maana ya kwamba... Kama hujui kitu basi utateseka sana mpaka kukijua maana yake,... Kwa mfano dom ina thamani ya shilingi bilioni 500 yaani hawa wote wakiipata hio pesa ni utajiri mkubwa kwao, lakini masikini ya mungu hawajui thamani ya kifaa hicho, hivyo wao wakidhani ni kifaa cha kompyuta kinachiitwa hard drive, yaani ni memory card ya kompyuta au kitu cha kuhifadhia mafile kadha wa kadha,...
Sauda ni Mschana mgeni katika kazi hio na mwanaume wake wa kwanza ni sahi, hakujua kazi hio ina ugumu kiasi gani hivyo hakutaka kuendelea tena na kazi ya uchangudoa badala yake kaamua kuiba ili akajiendeleze na chochote katika maisha,...
"sasa nikakiuze shilingi ngapi"
"wewe ulioiba ndio unajua thamani yake.... We tuletee hata elfu 20 tupate ya kula leo"
Aliongea dada mmoja ambae wanaishi wote katika chumba kimoja
"heeee, mi nataka nianzishe biashara wala staki kuendelea na hii kazi"
Aliongea sauda huku akikiangalia kile kifaa ambacho ndio dom Original kabisa, yaani kifaa kinachotafutwa na serikali kwa udi na uvumba...
"heheheheheeee haaaloooo.... Eti mi nataka nianzishe biashara... Weeeee na ukifanya hivyo uhame hapa kwenye hiki chumba"
Aliongea dada mmoja ambae ndio mkubwa wa kikosi hicho
"lakini dada Leah, mimi nitachangia kama kawaida pale nitakapokuwa na kibiashara kangu"
"ok.. Na ukishindwa kuchangia"
"sina budi kuondoka hapa"
"sawa.... Na huyo mwanaume ilikuwaje"
"ata staki tena, kwanza kaniumiza... Nilipoangalia pochi yake imejaa kadi tuuu, haina hata hela za kutosha nimeona buku buku tu"
"umeanza kazi vibaya sauda... Tena we una gundu wewe, sisi wenzio siku za kwanza kwanza ni elfu 50-50 tu"
Aliongea Leah huku kama vile wanamsuta, yaani laiti wangelijua sauda kaja na utajiri wa hali ya juu..
Tukija huku katika kitengo cha TSS ambako sahi ndiko anapo yapatia mafunzo yake,... Mafunzo yaliendelea vizuri sana, na sahi alikuwa ni muelewa mwenye kichwa chepesi mno.. Lakini ikumbukwe kuwa sahi anajua kila kitu, sema kaambiwa ajifanye hajui...
Masaa kadhaa mbele huku mjini jijini Dar es, alionekana sauda akiwa na mkoba wake alioifichia ile dom, alizunguuka nayo mno... Na yeye anajua klni kifaa cha kompyuta hivyo hata anapoingia anajua fika kuwa hicho ni kifaa cha kompyuta,... Hivyo habahatishi kwa ofisi anazoingia, lakini kila anapoingia anaambiwa hicho hakikai kwenye kompyuta, maana yake ni kwamba hata hao watu hawajui ni kifaa gani... Mana hakiendani na hard drive, japo maumbo ni sawa lakini option zake ni za kitofauti sana,
Sauda alichoka mana kazunguka kutwa nzima pasina mafanikio yeyote yale,.. Sasa akiwa anarudi zake nyumbani mana kachoka kweli kweli, afu hio dom ina kauzito fulani katika mkoba wake,.. Sasa hasira ukijumlisha na kuchoka, hapo utapata hasara tupu.. Saa ngapi sauda asiitoe ile dom na kuitupa dampo, mana haikuwa na faida kwake, kazunguka kila kona, mana kila anaempelekea anasema hakifai na hawajui kinakaa katika kompyuta gani,... Dom ipo dampo, kitu chenye thamani kubwa leo kinaishi dampo.. Sauda aliondoka zake tena kwa hasira mno, huku akisema kuwa
"kama vp nirudi zangu kijijini, siwezi kuuza mwili wangu"
Aliongea huku akipiga hatua za taratibu sana kwa kuchoka..
Sasa huku TSS sahi anasikia sauti katika kile kinasa sauti cha skioni
"GU hapa Naongea"
"yes, mkuu hali yako"
"salama tu... Sasa hio dom si uilete"
"mkuu, bado sijaipata"
"jana si ulisema unakwenda kuipata"
"hapana mkuu, sijafanikiwa"
"zimebaki wiki mbili kazi yako kuisha"
"nitajitahidi mzee GU"
Maongezi yaliishia hapo huku sahi akicheka sana kama vile kumdharau guu,
"hahahahahahaha.... Eti lete hio dom, anachekesha kweli huyu... Kwani mimi staki pesa"
Aliongea sahi huku akiendelea kuchapisha ramani zake kwa siri sana akiwa katika kitengo cha TSS na kazi zilikuwa zikimwendea vizuri ila hajui kama dom ilishaibiwa tena mbaya zaidi imetupwa dampo...
Baada ya wiki moja kuisha, sahi akiwa kambini, mana hio ilikuwa ni wiki ya mjini TSS... Na sasa yupo TMA, akiwa chumbani kwake na laptop yake alikuwa akiseti mambo yake ya satalaiti katika kambi hio,.. Lakini akiwa hapo mara General aliingia tena bila hata ya hodi,
"karibu mkuu"
Aliongea sahi huku akipiga saluti kwa mkubwa wake,
"unafanya nini hapa"
"aahhh nilikuwa nacheza cheza gemu hapa kidogo"
Aliongea sahi na ni kweli kwenye skrini yake kuna gemu lilikuwa likionekana...
"sasa, keshokutwa yule mzungu anakuja kuichukuwa ile dom... Hivyo utapaswa nawe uwepo ili kuisindikiza"
"lakini mkuu... Kwanini usitume vijana wengine"
"we pumbavu, kwahio umeshaona ni bidhaa ya kitunguu kila mtu apeleke si ndio"
"ok, lakini nawe si utakuwepo"
"tutakuwa kama watu watano hivi"
"sawa tutakwenda"
"halafu kingine, kenya wameamsha timbwili timbwili la kutaka silaha zao, sasa tunafanyaje"
"waache waje"
Sahi aliongea tu bila kufikiria, kitendo kilichomuuzi sana general,
"leo naona hupo sawa si kweli"
"nipo sawa mkuu... Kwani we ulitaka tufanyeje"
"tuwatumie mzigo wao"
"hapa hapatoki silaha aina yeyote ile.. Waache waje"
"ili tutumbuliwe si ndio"
"sina maana hio"
General aliondoka kwa hasira sana na anajua kumuunganisha kijana kama huyu katika kazi yake, na hawezi kumfokea sana kwasababu tayari keshajua siri nzito waliokuwa wakiifanya miaka yote, hivyo hawezi kumfanya lolote...
Sasa usiku mmoja sahi akiwa kalala, alisikia kukuru kukuru nje huko, akiwa kama kamanda hakutaka kulimezea mate, alitoka na kuchungulia... Aliona kalandinga la jeshi likisukumwa taratibu kabisa kuelekea msituni... Sasa sahi akajiuliza hili kalandinga linapelekwa wapi, lakini hakupata jibu, ikiwa ni usiku sana wa saa saba kwenda saa nane,... Sahi alilirekodi lile tukio kwa kutumia saa yake ya mkononi, na leo hakutaka kuwafuatilia, sahi alirudi zake ndani na kulala,...
Kesho yake mida ya saa nne, General na makamanda kadhaa wakiwa wamevalia suti zao, na hapo hakuna alievaa nguo za kijeshi,... Na hata gari zilizoandaliwa hazikuwa za kijeshi bali ni gari binafsi tu zenye usajili wa kawaida tu,... Lakini General alishangaa sana kutokumuona sahi katika maandalizi hayo,
"kamanda kiku"
"yes mkuu"
"ina maana salehe hajapata taarifa ya leo"
"nimemwambia mkuu, lakini hakunijibu kitu"
General aliamua kwenda katika chumba chake na kumkuta sahi akiwa anatumia laptop yake kwa mambo yake,...
"ujambo"
"sijapo mkuu karibu"
"sante... Vipi wewe, juzi si nilikwambia twende wote kuikabishi dom kwa mnunuzi"
Aliongea general huku akivua kamiwani chake,..
"mbona misheni ya jana hukuniambia"
General alishtuka kuskia mbona misheni ya jana hawakumshtua....
"unajua mimi ni General wa muda mrefu sana hapa kambini, na pia sitaki serikali yangu ijue udhaifu wangu ama kile ninachokifanya... Majangili wa kikenye wangelifika hapa na kuanzisha vita, ningeulizwa vita ilisababishwa na nini... Ningemjibu nini mheshimiwa raisi, hivyo jana niliwapelekea silaha zao, na sasa mambo ni shwari"
"ok, kwa sasa sijiskii vizuri mnaweza kwenda"
Aliingea sahi huku akikaa katika kitanda,...
"ok... Nimekuelewa, wacha tuiwasilishe dom kwa mteja wetu... Na gawio lako lipo pale pale"
Aliongea general lakini sahi kwa ujeuri hakumjibu kitu mpaka general akaondoka,... Lakini General hana imani na huyu kijana kabisa, licha ya kumuunga katika kikundi cha siri... General alimwita mwaju na kumpa kazi yake ile ile, ili ajue huyu mtu ni nani, mana bado ana mashaka nae, na alimuunga ili aropoke vyote lakini sahi mkimya hakutoa hata neno la kazi yake...
Sahi akiwa yupo ndani anaangalia skrini ya laptop inayoonyesha dashboard ya gari alilopanda general, sasa kumbe general amewekewa kamera katika kipini cha tai yake, yaani kile kipini cha tai kina kamera maalum.. Sasa kwa wakati huo General alikuwa ndani ya gari, na ile kamera ilikuwa ikionyesha dashboard ya gari, mana kidani kipo kifuani.... Kwahio kila wanapoenda sahi anaona kupitia laptop yake...
Mara ghafla mwaju kaja, sahi akafunika haraka haraka kisha akawasha gemu, na huu ndio mchezo anaoufanya yaani akija mtu yeye anawasha gemu,...
"mambo sahi"
"safi tu"
"afu leo mbona kama sijakuona mazoezini"
"mimi ndio sijakuona... Kwani yule aliodondoka kwenye mti ni nani asubuhi ile kama sikuwa mimi"
Aliongea sahi huku akicheza gemu,.. Sasa mtoto mwaju kumbe alivaa nguo ya ajabu sana, iliomfanya sahi kushindwa hata kucheza gemu,... Joto lilimpanda sahi na kujikuta anapunguza nguo bila kupenda
"heeee mbona unavua nguo jamani"
Aliongea mwaju huku akijifanya anaogopa... Kifua cha sahi kilimvutia sana mwaju na kujikuta anamwangalia tu... Mwaju nae hisia za mapenzi zilimjia na kujikuta anasogea karibu ya sahi
"nini mwaju"
"najua sote ni makamanda, lakini hisia hazina ukamanda...."
Mwaju aliongea kimafumbo, na sahi alimwelewa vizuri sana...
"kwahio"
Mwaju hakujibu kitu,.... Kumbe mwaju alimpenda sahi toka muda mrefu sana sema alikuwa anatafuta njia ya kufanya, hivyo hata kile kitendo cha kupewa nafasi ya kuja usiku kwa sahi, alikifurahia sana mana ni moja ya nafasi nzuri kwake,.
Mwaju alianza kumshika sahi, na sahi nae ni mtoto wa kiume hivyo vitu kama hivyo kwake, ni kawaida tu na uzuri anajua kuwa dom keshaipata hivyo haoni sababu ya kuto kuinjoi na wanawake,... Sahi alijibu mapigo ya mwaju,... Dakika 5 mbele mwaju alikuwa mtupu, yaani kajiachia kwa sahi, ila wakati huo sahi ndio anamalizia boxer yake.... Mara ghafla mwaju katoa jicho, tena likiwa limeambatana na mshangao... Kana kwamba kuna kitu kaona katika mwili wa sahi...
"sheby....."
Aliita mwaka aju, ila hilo ni jina la mtu mwingine lakini kamuita sahi,..
"una nini wewe... jina gani unaniita hilo"
"siamini kama kweli ni wewe.... "
"ati nini???"
Sasa mwaju kuna kitu kaona..... Sasa mwaju anakumbuka miaka mitatu iliyopita akiwa na sheby kitandani....
Je? Mwaju kaona nini???.... Na je? Huyu sahi ni nani, mana kama ni huyo sheby wanaemdhania mbona sura sio yeye.. Sasa huyu ni nani???
ITAENDELEA.....