Makapuku Forum

Makapuku Forum

Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, hatojiunga na kikosi cha kwanza kwa ajili ya kuanza mazoezi siku ya Jumanne huku akiendelea kufuatilia uhamisho wake kuondoka Stamford Bridge. (Marca)
 
Beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26, atakuwa na mazungumzo na meneja wake mpya Mauricio Pellegrino, wiki hii, huku Liverpool wakijiandaa kuvunja rekodi yao ya usajili kumchukua beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi. (Liverpool Echo)
 
Liverpool wamekataa kukata tamaa katika kumfuatilia beki wa Southampton Virgil van Dijk na watajaribu tena kufanikisha usajili huo kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Daily Mail)
 
Dau la euro milioni 100 kutoka kwa Barcelona kumtaka Philippe Coutinho, 25, limekataliwa na Liverpool. Barca walipanda dau jingine baada ya euro milioni 80 za awali pia kutupiliwa mbali huku Liverpool wakisisitiza kuwa mchezaji huyo hauzwi. (RMCSport)
 
Tottenham na Inter Milan zinafikiria kwanza kabla ya kutaka kumsajili beki wa Paris Saint-Germain Serge Aurier, 24, wakiwa na matumaini kuwa ada yake ya uhamisho itapunguzwa. (La Parisien)
 
Manchester United wamefikia makubaliano na beki wa kulia Serge Aurier, 24, wa PSG, lakini atalazimika kwanza kwenda mahakamani ili kupewa ruhusa ya kuingia Uingereza. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alikutwa na hatia ya kumpiga polisi. (The Mirror)
 
Wachezaji kadhaa wa Barcelona 'wamechoshwa mno' na sakata linaloendelea kuhusu uhamisho ambao huenda ukavuja rekodi ya dunia wa Neymar kwenda PSG, huku wengine wakiwa wamekata tamaa licha ya kumshawishi mchezaji huyo asiondoke. (SPORT)
 
Watford wanatarajia kukamilisha usajili wa Richardlison, 20, kutoka Fluminese katika siku chache zijazo baada ya mchezaji huyo kutoka Brazil kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza. (Hertfordshire Mercury)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom