.........Na safari hii waliunganishwa sambamba mzee Aly77 na Dokta Asha katika mission ile ya kuisambaratisha familia ya Mzee Mnyungunyungu ili Kamishna Shebby na wenzake wasije kujua siri zozote kuhusu Mr. X
Na hivi ndivyo mchezo ulivyokuwa unachezwa katika location ya Mkuyuni ambao Mr X ndie alikuwa mtengenezaji na mtazamaji na aliishia kufurahi na kujisifu kwa vile ambavyo mambo yalianza kutokea Mkuyuni kwenye mchezo ambao wachezaji wake walitumia akili na mbinu nyingi lakini kwake yeye aliuita Mchezo wa Vipofu.....
.....Haikuwa shida kwa Asha baada ya kuwasili usiku wa manane Mkuyuni na kukutana kwa siri na mzee Aly77 ambae alimpa maelekezo yote muhimu na zaidi kuhusu simu fake waliyopiga na kumuhadaa mganga yule mtoto wa Mnyungunyungu kwa kudhani kuwa anaongea na mteja wao wa siku nyingi juu ya kukutana kesho kwa niaba ya dawa ambazo sharti lake lazima aamke asubuhi sana akaziandae na kutokana na hali ya mazingira ya pale kijijini watu kuchelewa sana kuamka huo utakuwa wasaa mwepesi kwa Lady Ninja kufanya kazi yake ya kummaliza kwani endapo kina Shebby wakirudi na kuongea na yule bwana basi ajue fika tayari siri ya maisha ya tajiri wao mr X yatakuwa hatarini sana kwani waliamini pia Shebby anafanya kazi ile kwa shinikizo la babaake bwana Mwinchande ambae kwa maelekezo waliyopewa na mr X ni kuwa Mwinchande ni adui ake anayemtafuta miaka mingi ili amuue baada ya kumfichua ubaya wake kipindi akiwa polisi mkubwa na hivyo ameeka kisasi ambacho kinapitia mgongoni mwa mwanae anaejua kuwa mr X ni mtu m baya kutokana na hadithi za uongo alizopandikizwa na babaake (Mzee Mwinchande).
Kazi ilikuwa kama kumsukuma mlevi kwenda kilabuni ama kumfungulia mlango wa choo aliyebanwa na tumbo la kuhara,
yaani namaanisha kazi ilikuwa nyepesi mno kwa Lady Ninja kumuondoa duniani mtoto wa mzee Mnyungunyungu pindi tu alipoingia kibandani mwake bila kujua kwa juu kuna LadyNinja anamuinda na pindi alipokua wanainama yule bwana ili akae hapo hapo Lady Ninja Asha alijiachia kiwiliwili na kunining'inia mithili ya popo huku mikono yake kwa speed ya hatari ilifanikisha kupora panga dogo aliloshika yule mganga na kumkata eneo la koromeo huku mkono mwengine akimzuia kwa kumnusisha unga wa dawa frani zilizomfanya yule mganga ashindwe kupiga kelele na kubaki anatapatapa kwa krusha miguu akiwa amekaa amezuiwa kichwa na Lady Ninja huku ameshikishwa kipanga kilichonasia shingoni mwake wakati koromeo lililokatwa liliendelea kurusha damu mithili ya bomba la maji.
Ndipo hapo aliporidhia yule muuaji na kumuachia kichwa baada ya kuona damu zimepunguza kasi ya kuluka hapo nae alijikunja tena Lady Ninja na kujiachia chini ambapo alitumia dawa maalum za uchawi wa Kininja kisha akatoweka kimaajabu eneo lile.
Alisikilizia kwenye maficho yake ya siri kwa siku mbili huku akipewa taarifa na mzee Aly77 kuhusu kinachoendelea baadae na hapo akapata habari za kuja tena kwa Kamishna Shebby na kuziwasilisha kwa code maalum ya mr X kupitia simu yake iliyofungwa chipu ambayo haisomi kwenye mtandao mwengine wowote wa kawaida.
)('Sikia My Lady Ninja, hao watu wamenizidia ubaya sasa nami ni mtu mwenye huruma sana lakini muda mwengine sina jinsi kwa kuwa ni maadui na wamenianza, sasa hakikisha unaua wote wataojifanya kimbelembele, tena usije kumuacha mjukuu wa Mnyungunyungu huyo kijana ndie mrithi wa kila kitu hapo.. ili kuwazuia kabisa hao askali hakikisha na huyo humuachi hai pia Askali wote watakaotaka kukuzuia ua mara moja kasoro Kamishna wao Shebby yeye mpe onyo na umwambie kama anataka kupambana na mimi basi akafanye mazoezi ya kusimama juani na kukamata kivuli chake')(
Ndivyo ujumbe wa mr X ulivyosomeka na hapo ndipo Lady Ninja alipoweka mtego wake wa pili palepale msibani juu ya mti mkubwa kwa zaidi ya masaa 12 bila kusinzia wala kupepesa jicho akiwa kabanisha juu ya tawi moja lililokuwa usawa wa kile choo akiamini lazima yule mjukuu wa Mnyungunyungu aliyepewa amri ya kumuua iwe isiwe atakuja tu pale chooni kujisaidia.
* * * * * *
Na kweli Kipindi kina Kamishan Shebby na st,sirjent Kimaro wanaondoka muda mfupi baada ya shughuli ya mazishi kumalizika ndipo yule kijana akiwa na ndoo yake mkononi aliingia bafuni kwa lengo la kujisaidia haja Kubwa na hapohapo kwa mtindo wa ajabu na aina yake Lady Ninja aliweza kukirusha kitanzi maalum cha waya ambao aliuunganisha kwenye mashine ndogo aliyoifunga juu ya tawi la pili alipokuwapo na kweli kile kitanzi kilifika usawa wa shingo ya yule kijana na kabla hajapiga kelele kwa mstuko Lady Ninja aliwahi kutight kitanzi kwa kutumia ile machine na kuanza kuzidi kuzungusha skurul iliyokuwa ikiukusanya ule waya kwenye mviringo wake wa ile machine.
Na hivyo ndivyo alivyokuwa ananyongwa yule kijana na Lady Ninja Asha aliyekuwa kalala juu ya tawi la ule mti na kumpandisha juu yule kijana kupitia wire uliotight barabara shingoni mwake na pindi alipofika usawa alioutaka Lady Ninja alichomoa kamba nyengine ya Katani na kuifunga juu ya tawi baada ya kutengeneza kitanzi kisha akampachika shingoni yule kijana ambae tayari alishakuwa marehemu na kuulegeza tena ule waya wake kwa kutumia ileile mashine yake maalum na baada ya hapo alimvua kitanzi cha waya na kumuacha akining'inia kwa kitanzi cha kamba ya katani.
)(("Nimemaliza kazi Bosi"))(
aliwasiliana na mr X, Lady Ninja Asha pindi aliposhuka kwa style ya kipekee pale juu ya mti pasi na kuonekana na kuingia kule maporini kwenye makutano yake ya siri na mzee Aly77.
))("Weldone My Lady Ninja, Ushawekewa Mil, 200 kwenye account yako, lakini Umebakiza mtu mmoja ambae hana budi nae auawe")((
)(("Nani bosi"))(
))("Mzee Aly77")((
)(("Aliy77!!? si mwenzetu huyu?"))(
))("Kuna kitu bado hujaelewa Lady Ninja, ila ni muhimu ufanye hivyo kwa sababu ya usalama zaidi na uhai wa siri yako kama Dokta Asha huna budi kummaliza huyo babu kwani anaweza kustukiwa na hana mbinu wala si mwepesi kupambana kama wewe kutokana na hali yake pia hutakiwi kuwa na share kwa kazi hii kuanzia sasa kila kitu utaongoza mwenyewe Lady Ninja")((
)(("Sawa bosi, nasubiri signal yake ya kukutana nami nimalize mchezo"))(
))("All the Best My Lady")((
Na hayo ndio majibu aliyoyapata Lady Ninja Asha kutoka kwa Mr X mara baada ya kumjuza kilichokuwa kinaendelea na ndipo aliposubiri signal ya kukutana na mzee Aly77 ili atimize agizo la bosi wake ambae ni Mr X.
Na kweli baada ya muda mzee Aly77 alimtumia signal maalum Lady Ninja na kukutana pale kwenye kimsitu huku mzee Aly77 akiwa anahema mno kuonesha ni mtu aliyekuwa anakimbia kwa hofu pia.
"9121, Toweka eneo hili mara moja kuna msako unaendelea, yule Kamishna Shebby amekuja na polisi wengi sana uuuphh daah! Toweka haraka hapa si salama sasa mi nataka nirudi wasije kunitafuta harafu wakakosa kuniona uuuppph"
aliongea huku akitweta mzee Aly77 lakini katika hali ambayo hakuitarajia palepale Lady Ninja Asha alichomoa kisu na kumkita kifuani kwa Nguvu.
"AAAAAAAAAAGHH.."
Alitoa ukelele wa maumivu mzee Aly77 na kuanguka chini na muda uleule Lady Ninja alisikia sauti za miguu ya watu wakikimbilia eneo lile nae bila kupoteza muda aliruka beki mfurulizo kurudi nyuma mpaka usawa wa miti mingi mikubwa ambapo alidanda danda kwa speed ya Ajabu na kuibukia juu ya mti mmoja ambao aliamini isingekuwa rahisi kuonekana.
Hapo aliwashuhudia askali wengi wakiongozwa na Kamishna Shebby wakija mkuku eneo lile alipotoka ambapo alimuacha mzee Aly77 akiugulia maumivu pale chini akiwa bado hajakata roho.
Lady Ninja alifungua zipu ya mfuko uliojengewa na sambamba na mavazi yake na kutoa kifaa kimoja kimoja ambpo alipomaliza kuviunganisha ilionekana bunduki kubwa ya udunguaji ikiwa kamili.
Na hapo ndipo alipojieka sawa na kuanza kumlenga mzee Aly77 mara alipoona amepakatwa na Kamishna Shebby akilazimishwa kusema kitu.
Alisogeza lenzi na kumjaza vizuri kabisa sehemu za kichwa mzee Aly77 na papo hapo alifatua risasi iliyofumua kichwa cha mzee Aly77 mbele ya kamishna Shebby kabla hajatoboa siri yoyote.
Kitim tim ndio kilianzia pale Kamishna Shebby alipotoa ukelele na kuwaamuru vijana wake wakae makini watafute alipo mdunguaji, lakini bila presha wala papara Lady Ninja Asha aliendelea kumtungua askali mmoja mmoja na kuzidi kumchanganya Shebby hasa pale alipomshuhudia rafiki ake kipenzi st,sajent Kimaro akipoteza maisha na kuingia kwa kiza kilichowafanya washindwe kuona vizuri, lakini kwa Lady Ninja mambo yalikuwa mepesi kwani alivaa miwani maalum ya kuonea usiku.
)("Amebaki mwenyewe Shebby bosi")(
alichart kimtindo pale juu ya mti na mr X
(("Huyo mvunje mguu tu inatosha ili asikufate lakini hakikisha unampa Onyo nililokwambia"))(
Msg ilirudi na kipindi hiko Shebby alikuwa anahangaika akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa kwa hasira akimtukana muuaji huku akimlaumu kwa kuua watu wasio na hatia na kumlazimisha kama kweli anajiamini basi asijifiche bali ajitokeze wapambane.
Kipindi akiyasema hayo Shebby na kutupa bastora yake alikuwa maeneo ya mti uleule aliokuwa Lady Ninja Asha ambae aliamua sasa kushuka kwa kutumia kamba maalum aliyoinasisha kwenye lile tawi huku akitoa kicheko cha dhalau.
Na hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza Kamishna Shebby kukutana na Lady Ninja Asha kabla hajageuka kuwa Dokta wake na hatimae kuwa mke mtarajiwa.....
Baada ya mabishano ya Shebby na Lady Ninja hadi kufikia kumpiga risasi ya mguu na kuchomoa bastora ndogo iliyokuwa na risasi maalum yenye kisindano kidogo ambacho mtu akichomwa nacho kikagusa karibu na fuvu la kichwa basi kinapoteza kumbukumbu zote muhimu ambazo muhusika alikuwa anazifikiria na kumpoteza.
Alifanya hayo yote kwa niaba ya usalama wa mr X.
Aliamini mr X ni mtu mwema anayewindwa na wabaya siku zote.
Hakujua kama amepofuliwa na kile anachojua ama kuona kuhusu mr X sivyo hivyo kabisa.
alimpiga risasi ya ile sindano kichwani Shebby ambae alipoteza fahamu palepale.
* * * * * *
Baada ya Lady Ninja kumaliza na kuzima kabisa tukio lililotaka kuvumbua siri na ukweli wa bosi wake ambao hata yeye aliyeulinda hakuujua wala hakuwahi kumfikiria sivyo bosi wake ambae mbali na kutoonana nae lakini alimuheshimu siku zote na kufata matakwa ya kile alichoamrishwa nae kutokana na vile alivyosaidiwa na kujengwa kiimani juu yake tangia anaokolewa kwenye msuko suko kule India bila kujua kuwa yote ilikuwa mipango.
Baada ya kurudi kama kawaida yake siku hiyo hiyo aliingia kwenye kile chumba chake cha siri na kukuta ujumbewa Mr.X kuwa akae tayari muda wowote atapigiwa simu kwa niaba ya kwenda kumtibu Kamishna Shaaban kupitia mbinu ambayo hakufafanuliwa zaidi ya kuambiwa kuwa Mzee Mwinchande ameshatekwa kiakili na kuaminishwa yeye tu (Asha) ndie atayeweza kumtibu vizuri mwanae kutokana na kuchanganyikiwa kwake baada ya kupata taarifa ya tukio.
))("Kumbuka Lady Ninja, kinachokupeleka pale sio kumtibu tu, bali ni kujieka karibu na ile familia kama alivyowahi kujieka Aly77 kwenye familia ya Mnyungunyungu. nawe jichomeke na umtibu kwa umakini sana pia fanya kila mbinu hadi aanze kukupenda na ukifanikiwa kumteka kimapenzi utakuwa umemaliza kazi kwani utaelewa kila kitu kama kutakuwa na ubaya unasukwa juu yangu naamini utanisaidia mapema")((
Ndivyo alivyoagizwa na Mr X mara baada ya kuwasiliana nae kwenye kile chumba chake cha siri kisha alitoka na kweli alipigiwa simu na mtu asiyemfahamu akihema na kumuomba afanye msaada wa moyo wake ili kuweza kumsaidia mtoto wake ambae ameshambuliwa huko Mkuyuni.
Taarifa zile alizipokea kwa masikitiko makubwa Lady Ninja ambae sasa alijivisha kivuli na kuwa Dokta Asha kisha akamuaga mamaake na kwenda kukutana na mgonjwa yule ambae babaake alimtangazia kumlipa dau nono ili tu ahakikishe mwanae anarudi na kuwa kama zamani.
Na kweli Dokta Asha alikuwa mtaalam sana wa maswala yale na alikuwa na cheti cha kimataifa.
Alimtibu Kamishna Shebby kwa moyo wa kivuli cha Dokta Asha lakini akiwa anatega makucha kama Lady Ninja jasusi wa mr X.
Siku zilienda na alizidi kumuonesha mapenzi mgonjwa wake na kumyeyekea mno hali iliyofanya afauru kuanza kumteka akili yeye Shebby mpaka wazazi wake wakatokea kumpenda Asha na kuombea aolewe na mtoto wao bila kujua kiundani Asha ni nani.
Kama walivyosema wahenga 'Mapenzi hayajalibiwi' na ndivyo ilivyokuwa kwa Asha mara baada ya kuzidi kuwa karibu na Kamishna Shebby ndivyo alivyojikuta anazidi kumpenda kweli na moyo wa huruma kuanza kumjia kila alipomuona akilalama kupoteza kwake kumbukumbu na mara nyingi alitamani amsaidie kwani alijua yote yanayomsibu lakini alipokumbuka kiapo alichoapa mbele ya Tyga kuhusu kutii na kufatwa matakwa ya mr X, ilimlazimu aache kama ilivyo japo kuna muda alikuwa anaumia kweli juu ya Shebby na kupelekea hadi machozi kumtoka.
Na ndipo usiku mmoja ambao ndio ulikuwa wa mwisho kuwepo pale kwa mzee Mwinchande alipokata shauli na kuamua kumtibu Shebby akiwa kwenye usingizi mzito baada ya kumchoma sindano maalum ya usingizi na kufanikisha zoezi la kumtoa kisindano kilichokuwa kichwani mwake kilichomfanya asiwe na kumbukumbu vizuri.
Lakini usiku huo huo aliporudi katika makazi yake ndipo alipokutana na ujumbe mwengine kutoka kwa Mr X ukimlazimu afanye haraka kuzuia ujio wa mtu mmoja ambae alisahauliwa kuwa ni adui mkubwa wa mr X ambae anakuja jijini na askali mmoja shupavu kwa niaba ya kumchunguza wapi alipo Mr X.
))("Fanya Mbinu unayojua wewe Lady Ninja kuhakikisha huyo mzee hafikishwi jijini akiwa hai")((
alituma agizo mr X sambamba na docoment zenye maelekezo zaidi kuhusu huyo mzee ambae alikuwa na urafiki na mzee Mwinchande ambae nae ni adui wa mr X kwa mujibu wa maelezo aliyokuwa anampa Asha.
)(("Worry out I'll do my Best"))(
alijibu ujumbe ule Asha na kuchomoka kama kawaida yake usiku huku akiacha ujumbe mezani swala ambalo mamaake aliyekuwa anaishi nae alishalizoea japo hajawahi kuhisi vibaya mwanae anaendaga wapi na kufanya nini zaidi alimuombea arudi salama na kukubali pale alipokuwa anajibiwa kifupi tu na Asha pindi alipomuuliza mara nyingi alisema 'nimepigiwa simu ya dharula, nimeona haina haja ya kukusumbua usiku'
Na kutokana mwanae alikuwa special kwa utabibu wa mifupa wala hakuhoji zaidi yule mama ambae ni Zena.
Signal maalum za satelite zilitumwa na kuonesha kidoti cha gari iliyokuwa imem beba mzee Cyplian kupitia saa aliyovaa Asha pindi akiwa kwenye gari yake ndogo aina ya Toyota Crester nyeupe akielekea Morogoro na alipokaribia Chalinze signal ilionesha gari husika inakaribia maeneo yale na kwa mwendo inayotembea ingetumia dakika ishirini tu kufika pale na hapo ndipo alipoisogeza gari yake maeneo ya Shelly na kushuka kisha akaelekea ile njia ya Tanga huku akiwa makini na kupiga hesabu ya mbinu ambayo alipanga kuitumia na kwa hesabu zake haraka haraka ziligota pindi alipoiona basi moja iliyokuwa inatokea Tanga na kusimama pale juu maeneo ya Polisi Chalinze na ndipo alipoisogelea na kujichanganya na vijana waliokuwa wanauza matunda kisha kimakusudi alidondosha pochi yake na kumfanya ainame kuiokota ndipo alipobonyeza pete yake maalum ya mionzi mikali na kuirengesha usawa wa ringi ya taili za mbele kulipoingia waya za breki na kuzikata pasi na mtu yeyote kujua na wakati huo pia alipoangalia saa yake signal ilimuonesha ile gari iliyom beba mzee Cyplian imebakiza dakika tano tu kupita pale Chalinze.
("Camoon, go, go, go")
aliwazia na kujisemea moyoni Lady Ninja ambae safari hii alivaa mavazi ya kiislam hususani kwa wale washika dini na wenye itikadi kali kwani alivaa hadi nikabu usoni mwake.
Na kweli mara ile gari ilianza kuondoka kwa mbembe sekunde zile zile na ile gari aliyokuwamo mzee Cyplian ndio ilikuwa inafika eno lile na kilichofuta pale ni kishindo na honi nyingi mara baada ya dereva wa basi kushindwa kulicontrol basi lake kwa kukosa breki na kukata kona huku akiyagonga magari mengine na kulikosakosa lile alilokuwamo mzee Cyplian.
Kipindi hayo yote yakitokea Lady Ninja alikuwa makini sana tena kama sie yeye vile aliwashuhudia hadi polisi wakifika maeneo yale kudumisha usalama na ndipo nae alipoanza kusogea upande wa chini huku akijiapia hawezi kuondoka hadi ahakikishe mzee Cyplian amepoteza maisha pale na ndipo alipokuwa anaangalia kule ilipotokomea gari iliyombeba muhusika aliona aliona dariri zote za kufauru mission yake hasa pale alipomuona kijana ambae aliamini ndie dereva wa mzee Cyplian akiwa anavuja damu huku kachanganyikiwa akili.
Alikutana nae macho kwa macho na alishangaa kuona macho ya yule askali dereva akiwa anamtazama kwa kumshuku mno na hapo alinyanyuka kumfata kule alipokuwa anaenda, nae Lady Ninja alijiandaa kumlipua kwa mionzi iliyokuwa kwenye pete yake lakini kama bahati yule askali ambae alikuwa ni Cj4 alidondoka na kupoteza fahamu kipindi hiko Lady Ninja aliingia kwenye gari yake na signal ilikuja toka kwa mr X kuwa mission yake imeenda vizuri na ndipo hapo aliwasha gari yake taratibu na kuanza kuondoka huku akimuwazia yule askali ni mtu mwenye mbinu kiasi gani hadi alimtilia shaka kuhusika na ajali ile ambayo ingekuwa vigumu sana kwa mtu wa kawaida kusema eti imetengenezwa.
Na hapo ndipo alipokuwa njiani alipokosana kugongana na Jeep ambayo alipoiona tu alitabasam kwani aliijua vizuri kuwa ni ya mumewe mtarajiwa ambae ni Kamishna Shebby na alifanikisha kutoka maeneo yale na alipofika mbele kutokana na fikra juu ya askali yule aliyezimia kule aliona ni vyema apoteze ushahidi kabisa mara baada ya kusimamisha gari maeneo ya kibaha ambapo alimpa lifti bint mmoja na walipofika Kibamba aliipaki gari njia panda ya kijiji cha Hakipo.
"Samahani dada, naomba ukae hapa huku ukikanyaga kanyaga breki nataka kucheki huku nyuma kama taa inawaka maana hiyo display sielewi imekuaje sasa."
Aliongea Asha na kumfanya yule binti mpenda lifti kukaa kwenye kiti cha usukani bila kujua ni trick ya yule mtu nae alianza kufanya kama alivyoagizwa lakini Asha alipozungukia nyuma tua aliwasha mionzi yake hatari iliyomulika lile gari kwa dakika moja na papo hapo ilianza kuwaka moto huku akiwa amelock milango yote alianza kuondoka taratibu eneo lile na kumuacha bint wa watu akiteketea garin
"NOOOOO"
Alizidi kupiga kelele Asha mara baada ya kutoka kwenye mawazo mazito na kukumbuka mission ile ya mwisho aliyomfanyia mr. X kupelekea kuua watu wengi wasio na makosa kwa ajili ya manufaa ya mtu mmoja aliyemgeuza kuwa kipofu kiakili na mawazo juu yake pasi na kujitambua na leo hii alitaka akamuue mtu ambae anajua fika alikuwa ni babaake mzazi.....
Itaendelea