Makapuku Forum

Makapuku Forum

Update EURO WOMEN CUP
b9c65734cf22b0d91126dbee6469860b.jpg
Bingwa mtetezi ameondolewa rasmi na Denmark.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
***********END************
Kwa hisani ya Mbwana Samatta tukutane kesho kwenye Sports segment nyingine.
Shukran Nyagei
 
Wale wa isidingo. .....

Ilipoishiaaa......

...............Barua yenyewe ilikuwa hivi................

................................................................................

Mdogo angu Zena, naandika barua hii nikiwa na maumivu makali sana sehemu za shingo na kifua hususani kooni na hivi sasa uvimbe ambao awali ulikuwa kwa ndani lakini sasa umezidi kutokeza nje ya shingo, najua muda wowote unaweza kupasuka na kuimaliza safari yangu ya hapa duniani kuianza safari mpya kwenye ulimwengu wa ahadi kwa kila mja aliyeumbwa.
Uvimbe huu si wa jipu la kawaida bali ni ugonjwa ambao nimeuficha kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na aibu na kutopenda niwatie majonzi mapema lakini kwa kuwa sasa naona ule wakati wa kuumbuka umefika nimeamua kukuweka wazi ukae ukijua kinachoniua ni nini..
Hiki kinachonitafuna Zena ni Kansa.
Kansa ambayo imesababishwa na wadudu wabaya waliotoka kwenye mbegu za mwanaume nisiyemjua ambae kumbe alikuwa na ugonjwa m baya sehemu zake za kutungia mbegu nami bila kujua nilijikuta nazipokea mdomoni kwa kumnyonya uume wake mpaka anafika kilele kinywani mwangu nikijua nampagawisha ili nimchune vizuri kumbe nilikuwa naeka lehani maisha yangu mara baada ya bakteria hatari ambao sijawahi kuota kama wapo walipoingia na kueka makazi pembeni ya koo langu kutokana na ukweli huwezi kutema chote kile kichofika kwenye ulimi na hiyo ndio ikawa mwanzo wa tatizo ambalo nilikuja kugundulika tayari nimechelewa.

Ni aibu lakini nimeamua kutubu kwa kukuandika ukweli huu mdogo angu Zena nakusihi kama nawe una tabia ya kunyonya tupu za wanaume kwa kuamini ndio unamkoleza nakusisitiza acha haraka tabia hiyo na hili uje kumfunza hadi mtoto ninayemkabidhi kwako baada ya kifo changu.
Narudia Zena kumbuka kinachoniua dadaako na simjui ni mwanaume yupi aliyeniachia hawa bakteria walioshindika kutokana na kuwafanyia mchezo huu karibu kila mwanaume niliekutana nae kimwili kasoro mwanaume wangu wa kwanza na yule wa pili ambae ndie baba halali wa mtoto huyu nae ni shemeji ako niliyemuacha kimakosa mimi mwenyewe baada ya kumsaliti sana ambae ni Hussein.

Zena nakukumbusha pia hata utapoolewa ukiwa na mumeo usikubali kumuacha awe anakunyonya tupu yako mpaka unafika kishindo kwani kuna hatari kubwa ya magonjwa ya ajabu kupitia sehemu za siri si kwa mwanaume wala mwanamke ambayo mengi hayajaibuka ila leo hii mimi nimekuwa mfano wa mavuno ya tabia hizi chafu ambazo asilimia kubwa ya vijana si wa kike si wa kiume wanafanya haya kila siku ilihali sehemu husika zipo. Basi waambie wataokusikia habari za kifo changu labda utasaidia kuwaokoa baadhi yao japo najua wengi watakupuuza na hata wataokaidi basi waache waendelee ila wajue yanaweza kuwakuta kama yaliyonikuta mimi kwani hizi ni zama za mwisho wasiige mafunzo ya kishetani yanayosambazwa kwenye mikanda ya ngono.
Kifo kinauma sana hasa kifo cha dhihaka kama hiki... Dawa pekee ya haraka niliyoambiwa na daktari ni kukata sehemu inayoshambuliwa lakini sasa mimi nashambuliwa koo maana yake hata nikikatwa haitakuwa tiba.

Huo ndio ukweli Zena najua mwanangu hatolelewa na babaake wala hajawahi walau kushikwa mkono na babaake ambae wote tunajua maisha yake anayamalizia gerezani.
Basi nakuomba pindi utapokuwa unamlea Asha mlee katika maadili tofauti sana Zena mdogo wangu na uwe unampeleka walau mara moja kwa mwaka gerezani akamuone babaake kwani taarifa za uwepo wake naamini anazo.
Kumbuka Zena kumbuka mpeleke Asha madrasa akajifunze elimu ya dini.
Naamini kifua chake kitapojaa imani na jina la mungu litapokaa kinywani naamini atafauru majaribu mengi ya kishetani na kamwe hatokuwa mwanamke muuaji kama walivyo wanawake wengi wa leo nikiwemo mimi na wewe kwa kitendo chako cha kutoa mimba zaidi ya mara mbili tulipokuwa shule.
Nakusihi nawe utubu mdogo wangu na uzingatie usije kumpa mtu mwengine amlee Asha naogopa asije kuharibika na kuwa mwanamke muuaji akaja umiza wanaume kama mimi nilivyomuumiza babaake.

Kwa heli Mdogo angu,
mimi natangulia....
Mungu akipenda tutaonana kwenye ulimwengu wa mauti pindi nawe utapokuja mwaka wowote.

^................................................................^

Barua ya dada ilifufua msiba upya moyoni mwangu huku nikilia kwa uchungu sana kwani hata mimi nilikuwa na tabia hiyo ya kunyonya tupu za wanaume lakini daaaah! kumbe harufu na uchafu ule ambao ulikuwa unatokota shingoni mwa dada ni kansa ya koo?!!
Tena chanzo chake ni mchezo ambao hata mimi nilikuwa ni mmoja wa wachezaji wake...!! aaagh nilipogundua na kukumbuka mateso ya dada hadi pale alipotoa mkoromo mkubwa tena sauti ikitokea kwenye tundu lililokuwa linarusha uchafu wa usaha na damu hadi kufa kwake.... Nami kuanzia muda huo niliapa kamwe sitoruhusu mwanaume aninyonye utupu wala mimi kumnyonya utupu na kuahidi kuutumia mdomo wangu kwa kula, kunywa na kuramba vile vilivyohalalishwa tu.

Lakini mwezi mmoja baadae lilitokea janga la mvua iliyosababisha mto uliopita jilani na pale tunapoishi kufurika na maji kupasua kwenye makazi ya watu ikiwemo nyumba yetu majira ya usiku ambapo nilichobahatika ni kujiokoa mimi na mwanangu Asha niliyeachiwa na dada na hapo ndipo tulipogeuka wahanga wa mafuriko tulioishi katika kambi maalum uwanja wa taifa baada ya kupoteza makazi kwa zaidi ya miezi miaka miwili.
Serekali yetu imejaa hila na rushwa kwakweli japo machoni na midomoni haiko hivyo kwani baada ya kupewa ile kambi kipindi cha janga lile na kutusaidia miezi michache ya awali, ndipo walipotutelekeza kabisa na hapo nami nikakata shauli baada ya kumpata bwana ambae alitukaribisha kwake kabla ya kumuhama baada ya manyanyaso na kumuonesha chuki za wazi mwanangu Asha ndipo nilipopanga maeneo ya uwanja wa fisi na kujiajili kwa kuutumia mwili wangu. aaaag Moyo unaniuma sana kwa nilichofanya kwani nilimpeleka Asha kwenye shule ya watoto walio kwenye mazingira magumu sana na yatima na kumuacha kwa muda huko mwanangu Asha si kwa lengo kuwa simpendi bali kwa kumueka mbali na mazingira yale ambayo nilijua yatamuharibu kisaikolojia pindi atapokuwa anaona mamaake kila siku nalala na wanaume tofauti tofauti.
Siku zilikwenda huku kipato changu kikiongezeka na kuwa namtembelea mara kwa mara mwanangu Asha ambae alikuwa anazidi kunipenda siku hadi siku na pia nilizidisha mapenzi kwake hasa baada ya kipaji chake cha elimu kuonekana kwa wafadhili wa kihindi miaka minne tu tokea aishi pale na alipata bahati ya kupendwa na wale watu ambapo zilifanyika taratibu za kuondoka nae kwenda kumsomesha huko japo awali nilitaka kukataa lakini kwa ushauri wa watu na walimu wake sambamba na kalatasi za serikalini na kuhakikishiwa kuwa mwanangu hawezi kupotea na hii ni kwa faida yetu wote pindi atapofanikiwa huko kwani hata mimi nilishindwa kumlea hadi nikampeleka pale ndipo akiwa na miaka kumi tu niliweza kuvunja vunja zaidi yoote niliyoagizwa na dada Mariam juu ya Asha na hiyo ndio safari ya mafanikio yaliyokuja kuibuka na kufaidi matunda ya mwanangu Asha na kwa bahati mbaya dawa nilizokuwa natumia nisipate mimba ziliniletea madhala pale nilipohitaji mtoto nilishindwa kabisa kubeba mimba na nilipochunguzwa nilihakikishiwa haitawezekana kubeba mimba na ndio sababu hadi leo sina mtoto yeyote zaidi ya mwanangu Asha ambae siku zote aliamini mimi ndie mamaake mzazi......

...... Kipindi Zena akimalizia simulizi yake iliyowafanya Hussein bubu na dk Asha kubaki wanadosha machozi kwa uchungu mkubwa huku wakiwa wameshabadilisha kila aina ya mikao wakimtazama Zena bila kujua kumbe mlango ulikuwa unagongwa muda mrefu sana na walichostushwa ni baada ya kufunguliwa na kusikia viatu vya mtu akiingia pale sebureni na walipogeuka wote walimshuhudia Kamishna Shebby akiwa amesimama baada ya kuingia tena akiwa amestaajabu kupita kiasi kwa kile alichokuwa anakiona watu wamekaa chini wameyaacha makochi na zaidi wote walikuwa wanalia.

"Vipi Asha?! samahani mama kwa kuingia pasi na ruhusa.. vipi mzee wangu mbona sielewi kwema??"
aliongea kwa taharuki Kamishna Shebby na kusogea pale walipokaa kina Hussein baada ya mama mdogo wa Asha kumruhusu kwa ishara nae akae tu sofani huku nao wakijizoazoa kuketi vizuri kwenye masofa wakiwa bado na nyuso za huzuni.
"Vipi mzee wangu, umenitisha sana baada ya kuchelewa Asha.. Mama nini kimetokea hapa?"
aliuliza Shebby huku akiwatazama machoni ndipo Hussein alipoanza kumsimulia kisa kizima na kumfanya Kamishna Shebby abaki ameduwaa.
"Kha!! Ina maana Asha ni mwanao!!! yaani kumbe wewe niliyekutuma ni baba Mkwe!? Eee Mungu mbona siamini.."
"Amini hivyo baba, mimi ni mama mdogo tu wa Asha na huyu ndie babaake kweli kabisa wala sio utani hata mimi siamini kama leo hii tumekutana"
aliongea Zena kwa majonzi
"BABA"
Kwa mara ya kwanza Hussein masikioni mwake aliisikia sauti ya mtoto wa kike akimwita baba tena mtoto ambae hakuwahi kuilea hata mimba yake, walijikuta wananyanyuka kwa pamoja Asha na Hussein na kukumbatiana kwa nguvu huku wote wakilia lakini kilio cha sasa kilikuwa ni cha furaha.
"sikuwahi kufikiria hiki kitu jamani babaangu pole sana kwa yaliyokukutaa"
"Aaaah! mwanangu usinipe pole mamaaa nisamehe sana mimi nilichelewa kujua uwepo wako aaa"
Ilikuwa ni furaha ya baba na mwana kujuana huku Zena na Shebby wakiwa wamekaa wakiwaangalia na kumshukuru Mungu kabla nao hawajasimama na kuungana nao pamoja kuwafariji.

Baada ya kuliwazana na kila mtu kurejea katika hali ya kawaida huku furaha ya aina yake ikiwa kwenye moyo wa kila mmoja ndipo Asha aliposimama na kumshukuru sana Kamishna Shebby kwa ukalimu aliomuonesha babaake huku akimuomba babaake (Hussein) kuanzia siku hiyo afanye makazi yake pale kwenye ile nyumba wakti pia akimtafutia makazi mengine mazuri ya kuishi lakini ajabu Hussein alikataa na kumwambia Asha maneno ambayo hakuyatarajia.
"Asha mwanangu nakupenda sana na nimefurahi mno kukujua, lakini wewe ni mwanamke na sasa upo mbioni kuolewa na mwanangu wa hiyari ambae nataraji atakuwa mkwe wangu mwema siku zote, kwa sasa furahia kuwepo pale mpaka mtapooana ndipo kwa amri ya Mkwe wangu ndipo nitatoka na kukaa sehemu nyengine mtayojadili kwa pamoja nikae lakini si kwa amri wala matakwa yako binafsi."
Maneno mazito ya Hussein yalitosha kuutafsiri moyo wa Asha kiasi gani babaake alikuwa na mapenzi mazito na mchumbaake hivyo alikubaliana na mawazo ya babaake ila alimuomba Kamishna Shebby amruhusu basi alipie yeye gharama za pale hoteli na kwa mapenzi ili mradi mpenzi wake alidhike Shebby alikubali.

Baada ya hayo kumalidhika ndipo Hussein alipomuomba Asha alete kalamu na karatasi kwa niaba ya kuijibu ile barua tena mbele ya Shebby mwenyewe ambae awali alitaka awapishe nje ili wajadiliane vizuri lakini Hussein alimzuia na Zena alikuwa radhi Hussein amalize kila kitu.
"Nimekuja kama mshenga na sasa naichana bahasha na kuijibu barua kama baba, Asha mwanangu taja mahali yako ya Ndoa."
"Mh! baba si utaje wewe tu"
"Hapana wewe ndie unayeolewa"
"sawa basi mi.... mi Elfu kumi tu inatosha"
"Safi sana mwanangu"
alijibu Hussein na kuendelea kuandika na alipomaliza alimkabidhi Shebby palepale.
"Mwanangu tuachane na mambo yote barua hii ifike nyumbani ukitaka kuoa hata kesho njoo nitatoa mimi hiyo elfu kumi ya Asha japo ni katika pesa zako ulizonipa, hakuna gharama nyengine zaidi ya hiyo elfu kumi huku kwetu"
alisisitiza Hussein na kumshangaza mno Shebby lakini ukweli ndio ukawa hivyo na lilikuwa jambo geni kabisa kwa mila na desturi za kibantu barua kujibiwa mbele ya muhusika wa kiume na kumkabidhi yeye moja kwa moja.

Baada ya hapo ndipo Hussein na Shebby walipoondoka huku wakiwaacha Zena na Asha wakiwa nusu wameamini nusu hawajaamini kwa kilichotokea siku hiyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom