Man city wako kuonesha kuwa zile paund walizotumia /wanazotumia ziko halaliii kabisa ...japo ni pre season si kipimo tosha wengi wanakichanganya na kutest mitambo kama misemo ya wahengaa...anyway Pep msimu unakusubiria kuliko unavousubiriaa ....
Ebhu tuache ya pep na zile paundi zake sio kesiiii...huku sasa ifike mahali Zinedine Zidane akubali kuingia sokoni na kumletea Sergio Ramos msaidizi ambaye anaweza ku materialize na aina ya uchezaji wa timu kiujumla lakini pia atakaye elewana vyema na Kaka jambazi Sergio Ramos katika kumlinda Keylor Navas na gloves zake..... Nacho na Raphael Verane hawatoshi kumpa nguvu Ramos ya kumweka salama Navas na Zidane pale Bernabeu.
Madrid ameendelea kuwa mhanga wa mashambulizi ya kushtukiza counter attack...... Ukiacha goli la Gerald Pique pekee magoli mengine mawili yalifungwa kwa aina ile ile ambayo Real Madrid wamekuwa wakifungwa tangu Msimu jana.... Hapa Zidane inamhitaji kubadili mfumo kama anaamini katika kikosi kile kile cha msimu uliopita, 3:5:2 inaweza kumfaa zaidi kutokana na aina ya mabeki wawili wa pembeni alionao (Marcelo na Dani Carvajal) kuwa swap mpaka katika wingbacks ya kulia na kushoto. Hawa jamaa ni wazuri sana katika kushambulia na mara nyingi sana wamekuwa wakitengeneza mianya ya mashambulizi ya kushtukiza pale wanapopoteza au timu inapopoteza mpira katika eneo la timu pinzani..... Kuwa na mabeki watatu wa kati kunaweza kupunguza na kuziba kabisa makosa ya mabeki hawa wa pembeni ambao mara nyingi wamekuwa wakikikimbiza mpira nyuma ya mshambuliaji kuliko kuwa mbele ya mtu anayekuja na mpira.
Kukosena kwa Christian Ronaldo katika pre season hii na katika michezo mikubwa ni wazi kuna kitu kinamis katika eneo la ushambuliaji la Real Madrid... Madrid wamekuwa na tatizo la kutumia vyema nafasi ambazo wanazitengeneza na hivyo kuwafanya ubora wa eneo la ushambuliaji kuwa chini kwa sasa kuliko akiwepo mwenye eneo lake. Gareth Bale, Karimu Benzema kama senior player katika eneo lile Bado wanahitaji kuongeza umakini kwanza wao ndipo wawajengee na umakini vijana wanaocheza kwenye mabega yao.
Zinedine Zidane kama unaipenda Suti yako basi ilinde heshima ya real Madrid....... friend Match haina nguvu sana ila kucheza na Barcelona kuna nguvu sana haijalishi unacheza wapi.
Ernesto Valverde Bado anaendeleza kile alichokikuta na kazi kubwa aliyonayo ni kuendelea alipoishia Louis Henrique.... Kazi kubwa ya kwanza ni kumbakisha Neymar Jr katika jezi namba 11 ya Fc Barcelona, lakini pia kazi kubwa ya pili ni kumtafuta mrithi au mbadala wa ball Dancer Andres Iniesta mapema kabisa. ........