Makapuku Forum

Makapuku Forum

MKESHA WA MAWAZO

^^^^^^^^
HUSSEIN BUBU
______________
Usiku wa siku hiyo ulikuwa mgumu kwa Hussein kupata usingizi kwani muda wote mawazo yalimpeleka mbali sana huku akiwa haamini kama leo yuko huru na kumbe yule daktari bingwa Asha aliyesaidia kumtibu mtu aliyemsaidia yeye kwa moyo ni mwanae na kwa uwezo wa Mungu alifanya kazi ya kumsaidia jeraha baya alilopata Shebby mpaka amepona kabisa na kujikuta wanakuwa wachumba?
Alijikuta anageuza msikiti chumba cha ile hotel mala baada ya kujiazinia mwenyewe na kuanza kusali usiku kucha ambapo kila alipopumzika aliomba dua na kumshukuru Mungu na kuendelea kusali.
("Aaaaaah! kweli Mungu wewe ni Mkubwa sana na mwenye sifa za kipekee, Nakuomba kama ulivyonitendea muujiza wa kutoka jela na ukafanya kunikutanisha na mwanangu ambae nilijua habari zake nikiwa jela na kukata tamaa ya kumuona tena, basi baba nakuomba kama ulivyofanya hayo yote basi iwe hivyo na kwa Mr X niweze kumjua na kulipa kisasi kwa mikono yangu")
Na hiyo ndio ilikuwa dua kubwa ya Hussein bubu katika nafsi yake kila alipopumzika na kumshukuru Mungu na alisali huku mawazo yake hayo ambayo alikuwa nayo toka jela yakijirudiarudia akilini mwake

^^^^^^^^^^^
KAMISHNA SHAABAN
___________
Si Hussein tu, mambo yalikuwa hivyo pia kwa Kamishna Shebby ambae nae alikosa lepe la usingizi kwa kufikiria mengi sana huku akivuta picha siku ya kwanza anakutana na Hussein bubu.
("Daaah! Mungu kweli wa ajabu na ameeka siri nzito sana katika maisha ya kila kiumbe yalivyo mbele kutokana na mzunguko anaomuonesha kabla daa.... Yaani kumbe muda wote natoa msaada kwa mtu ambae imeandikwa ndie baba mkwe wangu!!! ")
aliendelea kuwaza Shebby
("Nina sababu zote za kumtafuta mshenzi mr.X na kulipa kisasi bado niko sahihi kwa hili")
aligeuka Shebby pale kitandani na kuchukua simu iliyokuwa pembeni ya mto na kumtumia txt Cj4 akimjuza kila kitu kilichotokea kule walipopeleka posa ambacho awali hajamjuza.
)('So huyo mkeo mtarajiwa Hussein kumbe ni babaake?')(
iliingia sms ya Cj4
na Shebby kumjibu ndipo sms ya Cj4 ilipoingia nyengine
)('Kuwa makini sana na mchumbaako hupaswi nae kumwambia habari zozote za mipango yetu')(
))('Sawa lakini kwanini unasema hivyo')((
)('Kumbuka upo kwenye mchezo na mr X sasa usikubali uchezeshe na mr X kwenye huu mchezo ila wewe ndie umchezeshe mr X ktk huu mchezo na hapo tutamshinda.. Kumbuka kama Hussein bubu tumemumtoa kama chambo harafu mwanae kumbe ni mchumbaako nina shaka hili mr.X analijua na isije kuwa na huyo mchumbaako akawa anachezeshwa na mr X kwenye huu mchezo pasi na yeye kujijua')(
SmS ya Cj4 ilimfanya Shebby ashushe pumzi na kuirudia mara mbilimbili huku moyoni akikili kuwa kuna upana mkubwa sana wa kimbinu na fikra baina yake na Cj4

^^^^^^^^^
DOKTA ASHA
______________

Kwa upande wa Dokta Asha yeye ilikuwa tofauti kidogo, naweza kusema yeye ndie alikuwa na mawazo mazito pengine kuliko wote.
Alijikuta anagalagala kitandani akigeuka huku na kule kuulazimisha usingizi ambao ulimuhama kabisa kutokana na mawazo mengi yaliyoibuka kichwani mwake mara baada ya kuujua ukweli na kuonana na babaake.
Muda wote maswali mazito yasiyo na majibu kamili yalizidi kuandama kichwa cha Asha na kumnyima amani ya kusinzia usiku kucha.
("Hivi kwanini lakini imekuwa hivi? aagh! Kwanini sasa?
Aaaaaaaaaa!!? Kumbe Mungu Yupo? leo ndio Nimeamini lakini Kwanini?!!")
alijiuliza maswali haya Asha mara nyingi kupita kawaida huku akijipigapiga kichwa chake na kadri alivyokuwa anajiuliza ndivyo hasira zilivyozidi kumshika na kuvimbisha kifua chake na hapo ndipo alipoamua kunyanyuka kwa style ya aina yake nusu sarakasi kwa jinsi alivyoizungusha miguu na kujibetua kiwiliwili akitegemea kichwa kabla ya kujirusha na kutua nje ya kitanda tena akiwa kasimama mbele ya dressing table yake ndogo anayotumia kujiremba na hapo ndipo alipoisukuma kuisogeza pembeni na ukutani pale kulipozibwa na dressing table kulionekana picha yake mwenyewe lakini ajabu alipoiondoa ile picha kulionekana batani kama za simu ambazo alitumia kuingiza namba alizozijua mwenyewe na hapo hapo kwa ajabu pale aliposimama kulipokuwa na dressing table kulipoanza kudidimia kwenda chini taratibu akishuka kama lifti na hatimae Asha alibukia kwenye chumba kimoja kidogo sana kilichokuwa na Kompyuta screen touch maalum za kisasa zikiwa kwenye kila upande wa kuta za kile chumba pamoja na kiti kimoja sambamba na mashine special za kuscan huku taa za rangirangi zikiwa zinawaka muda wote na Kompyuta zote zilikuwa on.

Alikaa harakaharaka huku akili zake zikiwa na mawazo mazito ndipo alipoandika ujumbe uliosomeka.
'NATAKA NIKUONE'
na kusimama akihema huku akizunguka zunguka kusubiri jibu lakini mara jibu lililokuja alipolifungua liliustua zaidi moyo wake ambalo liliandamana na picha ya babaake aliyemjua siku hiyo tu tena ujumbe ulisema
'KWANZA MALIZA KAZI YA KUIONDOA ROHO YA HUYU'

"Whaat..!!?"
alitaharuki Asha na kushindwa kujua aujibu vipi ule ujumbe na akiwa anatafakari mara ujumbe mwengine uliingia na alipousoma ulimpa maelekezo husika sambamba na kumuonesha picha ya hoteli ambayo alifikia Hussein na kona zote za ulinzi wa ile hoteli.
('I can't do this')
aliwaza Asha na kufungua ripoti za nyuma alizokuwa anatumiwa sambamba na picha juu ya watu ambao mission zake alizimaliza na kiasi cha pesa alichokuwa anatumiwa.
Moyo ulimuuma na kujutia kwanini amekubali kushawishika na kazi za mtu ambae hakuwahi kumuona hata siku moja katika maisha yake?
Kulikuwa na siri nzito sana moyoni mwa dk Asha juu ya safari ya maisha yake nchini India ambayo hakukuwa na yeyote anayeijua zaidi yake yeye mwenyewe.
...................
(^((^((^(((^^"Aaaagh!! Kweli nyie WANAWAKE NI WAUAJI hatari sana tena msiorudi nyuma WALA KUFIKIRIA hasa pale mnapopewa nafasi ama amri huitumia vizuri ili mzidi kuimanishwa na muonekane bora kuliko wanaume. Ila KUMBUKA kuwa wewe si wa kwanza kutumiwa na mr.X na laiti UNGEMJUA YAKINIFU huyo anaekutuma kesho anaweza kukuua hata wewe endapo atasikia upo kwenye mazingira hatarishi na maisha ya siri yake..... hahahahaaaa tatizo WANAWAKE HAMFIKIRII hah haha Ila nami nakwambia hii uliyoipata leo ni bahati kubwa sana ni bora tu uitumie lakini nakuahidi ukiniacha hai lazima nije kukutafuta na utalipa Damu zote zilizovuja leo.
Naapa sitokuja kukuacha hai kama leo utaniacha hai na umwambie mr.X asijidanganye MWISHO WAKE UPO na atakufa kifo kibaya na cha mateso aaghhh.." ^^)))^)))^))^))^)
.................
Ilimjia kichwani sauti hii ambayo aliiongea Kamishan Shebby kumwambia yule Ninja wa kike kule Mkuyuni pindi alipobong'onyolewa mguu, hii inamaanisha kumbe dk Asha ndie yule ninja aliyetumwa Mkuyuni na ni kibaraka wa mr X lakini kilichomuuma leo ni kuujua ukweli juu yake harafu kutomjua Mr X
"WHO FUC** ARE YOU..!!!?"
alipiga kelele za hasira Asha na kupiga teke kile kiti kilichokuwa mbele yake na kukipaisha hadi kwenye screen moja ya computa na kuivunja palepale.

Hayo ni maajabu machache sana kati ya mengi aliyokuwa nayo Dokta Asha.
Mzuri wa sura na umbo lakini nyuma ya pazia ni hatari sana ana nguvu na trick za kila aina za kimafia.
Ukweli yeye ni Muuaji wa Kimataifa wa siri anayetumiwa na Mr X muda mrefu na kashawaua wengi sana nyuma ya pazia waliojaribu kumpekenyua Mr.X kwaajili ya kumchafua.
Yeye ndie yule Ninja wa Mkuyuni na mr X ndie aliyesababisha kumueka jilani na Kamishna Shebby mara baada ya kumuarifu atautumia mtandao wake kumshawishi babaake Shaaban ambe ni mzee Mwinchande pasi na kujua chochote akubali kumwita yeye ambae kwa nje dunia ilimjua kama daktari awe tabibu namba moja na Mr X huyohuyo ndie aliyemtupa ajenge mahusiano na Kamishna Shebby ili aolewe nae na iwe rahisi kumdhibiti na kujua mbinu zote zitazopangwa juu yake kwani Shebby ndie alionekana mwenye kihelehele cha kumjua sana mr X.
Lakini mbali na hayo yoooooote Ukweli ni Kwamba Dk Asha hakuwahi kuongea ana kwa ana na Mr X wala kumuona.
Na ndio kitu kikubwa kilichokuwa kinamuumiza sasa... lakini kwanini miaka yote anafanya kazi na kuwasiliana na mtu asiyemjua ?
kaanza anza nae vipi na wapi hadi imefikia kuamini na kumtumikia hali ya kuwa hamjui ?
Imekuaje awe na sifa ya udaktari bingwa lakini kumbe pia ana sifa ya uuaji?
Hakika maisha ya Asha yalibeba maswali mengi sana ambayo kama hujayasoma na kuyajua maisha yake nyuma ya pazia yalivyokuwa basi hutoweza kuwa na majibu yake.

''I hate You Mr X.... I'll Find You..... and I'll Kill You''
aliongea kwa hasira kwenye mike moja maalum iliyoconnectiwa na mitambo yake iliyokuwa mule ndani Asha na kuituma moja kwa moja kwa Mr X na hapo ndipo alipoanza kuvunja vunja computa na kuharibu kile chumba chake cha siri huku akilia kwa uchungu lakini mara majibu yalirudi kwenye kompyuta moja ambayo alikuwa bado hajaivunja na alipoyafungua alistaajabu baada ya kusikia sauti ya Mr X ambayo mara nyingi huwa inaeditiwa juu kwa juu pindi inapotumwa na kila siku hua inabadilika badilika na safari hii ilikuwa nzito na ilianza kwa kicheko kikubwa sana kumuonesha Asha Mr X jinsi gani anajiamini na amemdharau sana licha ya kwamba alikuwa Ninja mmoja hatari mno asiyejulikana.
' '''hahahahahahaaaa Asha wewe ni mtoto mdogo sana ambae huna mbinu hata robo ya kunitambua zaidi ukijieka wazi utakuwa ndio Umejiangamiza mwenyewe hahahahaaa, Ukitaka kupambana na mimi na wewe itakubidi ufanye zoezi kama nililokuagiza umwambie Shebby afanye hahaha, tulia kwenye mchezo wetu Asha nakupa siku saba tu kama nilivyompa babaako Hussein miaka ile na uanze kuhesabu kuanzia Kesho.
Kumbuka wewe ni nyota wa mchezo wangu wa Vipofu.
wewe ni Kipofu wangu mzuri kati ya vipofu wangu wengi wanaocheza mchezo huu wa pamoja unaonieka salama mpaka sasa na kunifurahisha kila ninapoutazamaa hahahaaaa Asha Hussein pole sana, ni bora ungejiengua mapema kipindi kile nakusajili katika Mchezo wangu.
Umekaa na kukua katika mchezo huu na umekomaa nao Asha utawezaje kutoka? hahahahaaa kama ulikuwa Huujui Mchezo niliokuweka ucheze basi unaitwa Mchezo Wa Vipofu uliounza pindi tu ulipoingia kwa mara ya kwanza ndani ya ndege iliyokufikisha India ukiwa na wafadhili wako niliowaua miezi michache baadae hahahahahahahaaaaaaaa My Name is Mr X huwezi kucheza na mimi kwani nilishakupofua miaka mingi huna macho Asha.
hahahahahahahaaaa'''''''
Ilimalizikia ile sauti kwa kicheko kilichomfanya Asha abadilike zaidi na kubinuka sambasoti mara alipoikwanyuma kwenye umeme ile computa na kuibamiza chini kwa hasira na hapo ndipo alipojibinua tena na kufungua sehemu moja kulipokuwa na kijimlango chengine na ndipo mbele yake alitazamana na mavazi yake ya kazi sambamba na silaha zote.
"We tumia macho yako mimi natumia hisia zangu...Lazima Tuone Kati ya mimi Kipofu na wewe Mwenye Macho nani Atashinda Mchezo"
aliongea maneno haya Asha na kuanza kuvaa mavazi yake ya kazi kwaajili ya kuianza kazi ya kupambana na Mr X kutoka kwenye Mchezo wa Vipofu....



MIAKA 17 NYUMA -
-------------------------------
MCHEZO WA VIPOFU
( ASHA HUSSEIN )


Akiwa haamini kama kweli ni yeye leo hii yupo kwenye ndege ile kubwa ambayo ilikuwa inachana mawingu angani huku pembeni yake amekaa na bwana mmoja raia wa India akiwa na mkewe mwenye asili ya Kizungu, aliendelea kugeuka geuka na kuwatazama watu wale aliowajua kama mr & mrs Rajesh ambao hawakuisha kumuonesha tabasamu mtoto yule wa makamo waliyemjua kwa jina la Asha Hussein.

Safari ilikuwa ni nzuri na salama kwao na muda wote Asha aliwaza maisha aliyomuacha mamaake na kujiapiza kamwe hatoenda kuichezea bahati ile iliyomuangukia miguuni mwake pindi atapoanza masomo yake nchini India kama ilivyokuwa nia na madhumuni ya wale watu ambao walikuwa ni wafadhili waliojitolea kwenda kumsomesha kwao hasa kutokana na uwezo wa ajabu wa akili waliougundua kuwa nao yule mtoto pindi walipokuwa na ziala ya kuwatembelea na kuwasaidia watoto wasomao kwenye shule ambazo zilitokana na mfuko wao walio-share na serikali ya Tanzania zilizowajumuisha Yatima na watoto waishio kwenye mazingira magumu ili wapate elimu.
Akili za Asha na uwezo wa kufauru alama za juu hususani masomo ya sayansi ndio kilikuwa kivutio kikubwa kwa wale wafadhili kufata taratibu na kumchukua kwa niaba ya kwenda kumuendeleza kwao ambapo waliamini ndipo kuna elimu bora zaidi itayoweza kumuinua kipaji chake hususani katika sekta ya utabibu kwa vile alivyofauru sana Biology na maneno yake mwenyewe alipoulizwa anataka kuwa nani mara zote Asha alijibu kuwa Doctor.

Ndege waliyounganisha kutokea SA iliwasili ktk jiji la Mumbai baada ya safari ndefu ambapo wasafiri walianza kushuka na kwa mara ya kwanza mboni za Asha ziliweza kuitazama Mumbai na kukanyaga ardhi ya India akiwa na miaka kumi tu, huku akiwa anashangaa ukubwa wa ule uwanja na ndege kubwa nyingi ambazo zilikuwa tofauti na zile alizoziona Dar se salaam Tanzania.
Walitembea taratibu huku akigeuka geuka nyuma kuangalia ule uwanja Asha alikutanisha tena macho na baba mmoja muafrika aliyemuonesha tabasam na kumkumbuka kuwa walionana toka uwanja wa ndege Tanzania na alimpatia zawadi ya kimdoli cha bata pindi alipokuwa ndani ya ndege kabla haijaruka DsM na hapo Asha nae alitabasam na kumpungia yule mtu.
Walifika nje ya uwanja na kuingia kwenye gari moja ya kisasa aina ya Hummer milango sita iliyokuwa inawasubiri wenyeji wake ambapo kwa Asha alikuwa anajionea maajabu tu lakini ndio ulikuwa ukweli bibi na bwana Rajeesh walikuwa watu wenye pesa sana.
Lakini walipoanza kuondoka yule bwana muafrika nae aliingia kwenye taxi na kumuamuru dereva aifatilie ile Hummer taratibu ila achunge asiwe anaikaribia sana.

Na kweli aliweza kuifatilia ile Hummer hadi ilipofika eneo husika na kusimama nje ya geti moja kubwa na kwa upande wa yule bwana wa kiafrika aliyekuwa kwenye Taxi alimuamuru dereva apitilize kwenye ile njia asisimame.
hadi baada ya mwendo mfupi alimuamuru aingie kwenye Hoteli moja iliyokuwa jirani na kule walipoiacha ile Hummer na baada ya yule bwana kumlipa ujila wake yule dereva taxi aliondoka na kumuacha mteja wake akiingia kwenye jengo la lile hoteli hadi sehemu ya mapokezi.

Kulikuwa na siri nzito yule bwana iliyomfanya afike india na muda mwingi katika kila stage anayopiga kuna mtu alikuwa anachart nae na kumpa maelekezo kunachoendelea.
)(' Weldone, kazi nzuri Tyga andaa mbinu ya kuwa nae ndani ya mwezi mmoja')(
Ulikuwa ni ujumbe mfupi kutoka kwenye simu ya yule bwana aliyeitwa Tyga pindi alipokuwa ndani ya chumba cha hoteli ile mara baada ya kumaliza taratibu zote za malipo.
)('Woryout Boss')(
alijibu kwa kifupi na kuendelea kukichunguza kile chumba pande zote na baada ya kulidhishwa nacho alitupia kibegi chake kidogo alichokuwa nacho kitandani sambamba na Kapelo aliyovaa kisha akavua nguo zote na kubaki na bukta ndogo na hapo alianza kujinyoosha kwa kufanya mazoezi ya ajabu ya kujipinda pinda na kila kiungo kilijigosha hadi alipokuwa anajipinda kukawa kimya bila kugosheka kiungo ndipo aliporidhika na kuingia bafuni kuoga.

Aliporudi alikuta simu yake ikiwa imeingia ujumbe wa picha na video uliomfanya atabasam na mara alipoufungua alianza kushuhudia garden huku camera ikionesha kuchukuliwa bila utulivu lakini haikumzuia kuona mazingira machache hadi sehemu za ndani za nyumba moja ya kifahari huku akisikia sauti za watu waliokuwa wanaongea na mtoto aliyebeba ile kamera mpaka pale alipokiona chumba alichokuwa anakaribishwa yule mtoto na mara aliona kitanda kipindi hiko sasa kamera ilitulizwa na hapo ndipo alipomuona mtoto Asha akikaa pale kitandani baada ya kuelekezwa mazingira ya chumba chake na bafu.
("Good baby, soon Asante kwa ushilikiano wako")
aliongea yule jamaa na kuzitazama picha muhimu zilizotumwa na kuyasoma mazingira ya nyumba ya bwana Rajeesh na chumba cha Asha.

Wakati hayo yakiendelea kwa bwana Tyga upande wa Asha baada ya kuoneshwa mazingira na mrs Rajeesh muda wote yeye alikuwa na ule mdori aliozawadiwa na yule baba wa kiafrika ambae hakuwa anamjua pia hakuwa anajua ule mdori ni nini hasa.
Hata Rajesh na mkewe walichukulia ile kama zawadi na walijua ule ni mdori kama ilivyo midori mengine bila kujua mdori wa Asha uliotengenezwa kwa mfano wa bata ni mdori maalum uliokuwa na uwezo wa kutuma mawasiliano ya sauti na picha huku ukirekodi kwa video kamera maalum zilizotengenezwa kama macho ya ule mdori huku kwenye upande wa mdomo wa mdori kwa ndani kulikuwa na memori maalum iliyounganishwa na kinasa sauti huku wire mwengine uliokuwa upo ndani ya ule mdori ukiwa na kadi special inayoconnect vyote na kutuma signa kwa wahusika wa ule mdori.

Mara nyingi Asha alipenda kucheza na mdori wake kutokana na kukosekana mtoto saizi yake wa kuongea nae kwenye nyumba ya Rajesh kipindi akingojea nafasi ya kupelekwa shule kama alivyoahidiwa na hali ile ilimfanya azunguke nae karibu kila kona ya nyumba na kuwasaidia watu wamiliki wa mdori kuzidi kuchukua picha muhimu za jengo ile kupitia mdori ule wa bata.

Baada ya wiki mbili Asha alipewa habari za kupata shule na aliambiwa angejiunga nayo siku tatu zijazo.
Habari ile ilimfurahisha sana na siku ya siku ilipofika mr. Rajesh pamoja na mkewe waliingia kwenye gari sambamba na Asha kumpeleka kwenye hiyo shule maalum ambayo huko watu walikuwa wanasomea lengo tu.
Yaani kama unataka kuwa daktari wa mifupa basi utasome udaktari wa mifupa kama unataka kuwa daktari wa moyo halkadhalika utasomea ndoto yako hiyo basi ilimradi lazima baada ya miaka kumi utakuwa professional kabisa.

Lakini siku hiyo walipokuwa njiani kuelekea kwenye hiyo shule ambayo ilijitenga kidogo na jiji la Mumbai na hata njia ya kufika kwake ilikuwa lazima ukatishe kwenye msitu mmoja wa serikali ambao ulikuwa kimya sana ndipo unaibukia kwenye milima ilipokuwa hiyo shule ambapo kulikuwa na majengo mengi makubwa na hostel za wanafunzi.
Nia na madhumuni ya chuo kile kuwa mbali na jiji ni kuwapa wanafunzi muda wa kusoma na kutuliza akili zao na hata Rajesh alipendezewa na shule ile na kuamini itamfanya Asha asome na kutimiza malengo yake.
Katika hali ambayo hawakuidhania wala kuitarajia bwana Rajesh alipokuwa anakaribia kumaliza kile kieneo chanye msitu mara mbele yake kwenye kona alilikuta roli likiwa limeharibika tena limeziba bara bara lakini punde tu aliposimama walitokea vijana watatu wakiwa wamejifunga vitambaa usoni na kuanza kulishambulia gari la mr Rajesh na kuharibu haribu matairi yote na kuyatia pancha.
"Msiniue jamani msituue semeni mnataka sh ngapi niwape tafadhalini"
aliongea Rajesh baada ya wale vijana kuacha kurindimisha risasi na kuwaamuru wote waliokuwa ndani ya gari ile watoke nje.
kwa Asha ilikuwa ni kilio na mikojo kuanza kumtoka kwa hofu na kujilaumu kwanini amekubali kuja kwenye nchi ambayo kumbe haina amani hata kidogo,
alikuwa hakuwahi kusikia milio ya risasi ikipigwa live hapo kabla zaidi ya kuangalia kwenye picha za kivita.

Lakini Mbali ya Rajesh kujitahidi kujitetea na kuitetea familia yake haikutosha kuwatia moyo wa huruma wale watu ambao walionesha walikuwa hawahitaji pesa za Rajesh zaidi walianza kummiminia risasi tano za kifua palepale na kumpeleka Rajesh chini mbele ya macho ya mkewe na Asha.
"Nehiiiiiiiiii"
alipiga kelele mke wa Rajeshi na kumlalia mumewe aliyeanguka chini muda mfupi huku damu nyingi zikiruka na kutapakaa eneo lile lakini nae alipigwa risasi ya kichwa na hapo ndipo alibaki Asha akilia huku akiwa kafumba macho kwani alijua tu lazima na yeye auliwe na wale watu na hakuweza kujitetea vyovyote kwani hakuweza kuzungumza kihindi wala kiingereza chake kilikuwa cha kitoto sana kile cha kutajisha lakini Rajesh ilikuwa rahisi kuongea nae kutokana nae kujua kiswahili japo rafudhi yake haikuwa nzuri.

Lakini akiwa kachuchumaa amefumba macho Asha akilia kwa uchungu huku mwili ukiwa umekufa ganzi ndipo mara alisikia muungulumo mwengine wa gari ikija kasi na kufunga breki karibu na gari yao iliyoshambuliwa na hapo ndipo aliposikia milio ya risasi ikirindima mfurulizo na vioo vya gari vikipasuka kwa zaidi ya dakika tatu na kumfanya azidi kutetemeka kwa hofu na kujikojolea zaidi huku akiwa hajui nini kinaendelea.
Lakini baada ya ukimya alisikia sauti za viatu na hatua za mtu akimsogelea na hapo alijua sasa ndio mwisho wake hivyo alisali kwa na kutulia akijiandaa kuisikia risasi ikipenya mwilini mwake lakini ajabu haikuwa hivyo alishangaa kuhisi akishikwa bega na huyo mtu baada ya kumsogelea zaidi.
"Inuka binti Usiogope"
aliisikia hii sauti iliyomfanya ageuze shingo kumuangalia muhusika ambapo hakuamini hata kidogo mara baada ya kuiona sura ambayo haikuwa ngeni machoni mwake
.....

Itaendelea
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom