"Mwanangu vipi kuhusu yule binti naona siku zinaenda na wewe uko bussy sana wala huoneshi kujali kama awali, ooohoo angalia wasije kuwahi wenzako!"]
["Daah, baba bwana... Mbona siku bado ila nitajitahidi basi wiki hii nimtafute mshenga tuandike barua ipelekwe au unasemaje baba"]
[["Akaah mimi sio muoaji shauri yako mwanangu ila kumbuka alivyokusaidia yule binti..!"
["Nakumbuka baba"]
[["Basi ufanye hima kama utashindwa kumtafuta huyo mshenga basi itabidi uje huku tukutafutie"]]
["sawa baba"]
Yalikuwa ni maongezi kwa njia ya simu baina ya Kamishna Shebby pindi alipokuwa ndani ya ofisi yake pale gerezani akizungumza na babaake ambae ni mzee Mwinchande aliyekuwa nyumbani muda huo na kumkumbushia swala la kumuoa Dk Asha.
Ukweli jambo la mr X ndilo lililomchanganya sana Shebby na kusahau jambo la ndoa kwa wakati huo huku akiumia kila alipokumbuka vifo vya askali wenzake na kuzidi kupata motisha ya kumtafuta mr X.
Kesho yake majira ya asubuhi na mapema Kamishna Shebby mara baada ya kufanya mawasiliano ya siri na Cj4 kama ilivyokuwa kawaida na taratibu yao waliyojiekea na kupeana riport zote muhimu walizozibaini katika mikakati yao ya siri juu ya mr X, ndipo Shebby alipomuelekeza Cj4 kuwa ataelekea huko hotelini kukutana tena na Hussein akitaka ampe kazi itayofanya awe anatoka mara baada ya kusikia kuwa tokea siku alipomuacha hajatoka kwenda popote kutembea wala hakukuonekana dariri za mtu yeyote kutaka habari zake wala wale maspy wa mr X.
Na kweli majira ya saa nne asubuhi Shebby aliwasili pale hotelini na kukutana na Hussein bubu.
"Karibu baba karibu sana"
alikaribisha Hussein akiwa mwenye furaha pindi alipofungua mlango na kumkuta aliyemgongea kuwa ni Kamishna Shebby
"Ahsante sana baba"
alijibu Shebby na kuingia ndani.
"sasa baba ilikuwa nije kesho lakini nimekuja leo kwa sababu frani zitazofanya nikuongezee muda wa kuendelea kuwepo hapa lakini nilikuwa naomba unisaidie jambo moja"
"Usijali baba, usijali kabisa nakusikiliza na kabla hujasema naamini niko tayari kama litakuwa ndani ya uwezo wangu"
alijibu na kukaa vizuri Hussein huku akimuangalia na kumsikiliza Kamishna Shebby kwa umakini mkubwa.
"Sawa mzee wangu, ni hivi... Kipindi nilipokuwa nauguza jeraha la mguu nilitokea kupendana na binti ambae ndie alikuwa daktari wangu alienisaidia kwa kiasi kikubwa sana hadi nikafikia hatua hii ya kuwa kama awali..."
"Ndio baba endelea"
"Sasaa, nilimuahidi kuwa nitafanya mpango wa kujitambulisha kwao ili tufanye taratibu za kufunga ndoa na kuwa mke na mume.... sasa Shida yangu baba nakuomba wewe uwe mshenga wangu unisaidie kuandika barua ya posa nikupeleke hadi nyumbani kwao na wewe ndie utayeingia na kunitambulisha sambamba na barua."
"Mh! mwanangu lakini mbali na kukutibu tu umechunguza tabia yake kiumakini?"
"Kwa hilo baba sina shaka"
"Haya mwanangu mimi kwako sina pingamizi kwa hilo, fanya tuiandike hiyo barua na hata leo hii ukitaka unipeleke niko tayari kwa hilo kwa moyo mmoja ila nasaha zangu kwako ziko palepale usiwaamini wanawake wala usiwachukie kumbuka kuwa Wanawake ni Wauaji"
aliongea Hussein na kumfanya Shebby atabasamu na ndipo alipotoka na kurejea tena akiwa na bahasha sambamba na karatasi na kwa msaada wa Hussein wakaanza kuiandika barua.
* * * * * *
"Mamaaa, mamaa, mama kaa tayari tayari leo usitoke kwenda popote"
"Kivipi Asha mwanangu mbona ratiba zako sizielewi!"
"mama bwana, ni hivi... yule mchumba niliekwambia barua yake inakuja leo"
"Hee, ni wewe kweliii Asha au mwengineee"
"Ni mimi mama mbona huamini!?"
"Mh! unajua toka uliponambia siku ile nilichukulia mzaha kwa itikadi zako za kutojichanganya na watu, sasa sijui imekuwaje kuwaje hadi ulikubali kuacha shughuli zako na kumtibu mgonjwa yule tena ukidiliki kukaa kwao kwa zaidi ya miezi miwili na kama haitoshi unarudi na kuniambia ndio mchumbaako? au mlikuwa mnafahamiana muda mrefuu!!!"
"hahaha hapana mama ni mapenzi tu, basi si unajua wewe ndie mama na wewe ndie baba. Ikija barua ijibu malizana nao bhaasi ahhaha"
"Hahahaaa haayaa mwanangu nimekuelewa"
Yalikuwa ni mazungumzo ya dk Asha akiwa na mamaake ndani ya nyumba moja ya kifahari ambayo walikuwa wanaishi wao wawili tu yaani mama na mwana.
Haikujulikana kama yule mama alikuwa na watoto wengine ama laah, lakini mara nyingi pale alikuwa anaishi na Asha ambae yeye alikuwa mtu wa kutoka mno na alihakikisha mamaake anakuwa ni mwenye furaha siku zote.
Baada ya masaa matano kupita yule mama akiwa amekaa sebuleni mara alarm ya mlango iligongwa na alipoinuka kufungua alikutana na mlinzi wao wa getini akiwa kasimama mlangoni.
"Samahani mama, kuna mzee furani anahitaji kuonana na nyinyi vipi nimruhusu apite?"
"Mruhusu tu"
"Sawa Asante mama"
alijibu mlinzi na kukimbilia tena getini na kumruhusu kuingia ndani ya jengo huyo mzee aliyemzungumzia ambae alikuwa ni Hussein bubu mara baada ya kuoneshwa nyumba husika na Shebby ambae alikuwa kasimamisha gari mita hamsini na eneo lilipokuwa geti la kuingilia kwa kina Asha.
"Habari mama"
"Salama karibu"
alijibu yule mama ambae alikuwa na mwili wa wastani mara baada ya kusalimiwa na Hussein na kumruhusu akae.
Hussein hakuchelewa kujielezea kilichomleta pale na yule mama hakuonesha kupinga wala kuwa na maswali mengi zaidi ya kukubali na kuipokea ile barua
"Ahsante sana mama kwa ukarimu wako, vipi lakini mzee bado hajarudi kazini.?"
"haha Hapana usijali mzee kwa bahati mbaya hatunae siku nyingi"
"Oooh pole sana mama"
alijibu Hussein na kunyanyuka akijiandaa kuaga mara baada ya kupewa tarehe ya kuja kuchukua barua ya majibu lakini kabla hajaaga alikumbuka kitu frani
"samahani mama hivi unaitwa nani.?"
"Ahaa mi naitwa Zena Hamisi Kidongo"
alijibu huku akiwa katabasamu yule mama lakini ikawa tofauti kidogo kwa Hussein mara baada ya kulisikia lile jina.
"ZENA HAMIS KIDONGO!!?"
"Eeeh kwani vipi baba mbona umeonesha kulishangaa kidogo jina langu baya sana nini?"
"Hapana mama, hilo jina sio geni sana labda nikuulize unamfahamu Mariam Hamis Kidongo"
"MARIAM? Haah!! huyo ni Marehemu dadaangu kabisa we umemjuaje na alifariki miaka mingi sasa"
alistaajabu yule mama na kumuangalia kwa makini Hussein ambae alijikuta anakaa chini kabisa akiwa kapigwa na bumbuwazi zito usoni mwake na machozi kuanza kumtoka akiikumbuka barua ya mariam iliyomuelekeza kuhusu ugonjwa wake na habari juu ya mtoto wake wa kike ambae alikuwa anaitwa Asha na kuanza kuamini kuwa huyu aliyekuja kumchumbia huenda akawa ni mwanae kabisa kwani hata jina alilotajiwa na Shebby pindi walipokuwa wanaandika barua ni Asha Hussein
"Zenaa.. Oooh! Mi naitwa Hussein.. aaagh ndioooo Hussein Bakari... Hussein yule wa dadaako Mariam"
aliongea huku machozi yakimtoka Hussein kama mtoto
"Haa! Ina maana wewe ni Shemeji Hussein tuliyesikia umefungwa maisha sijui Kunyongwaa aaagh Ashaaaaaaaa ni mtoto wako aliekuachia dada!!aaaaaaaa Munguuuuu"
alistaajabu yule mama na kuangusha kilio kilichomstua Asha mara baada ya kusikia anaitwa na kuanza kushuka haraka juu alipokuwa na kufika sebureni ambapo hakuamini alichokuwa anakiona na hakujua kisa na mkasa mpaka mamaake na yule mzee ambae alijua ni mshenga kugalagala chini wote wakiwa wanalia kwa uchungu mithili ya familia moja iliyopokea taarifa ya kifo cha ghafra kwa mtu waliyempenda na kumtegemea.
"Mamaa .. maaamaa!!! Vipi nini kimetokea tena?"
alifika haraka pale sebureni Asha huku akiuliza kwa mshangao na kumuinua mamaake ambae hakuwahi kumuona akiwa analia kwa uchungu kiasi kile tangia apate fahamu zake mara baada ya kurudi kutoka India alipokuwa amepelekwa akiwa bado mdogo na wafadhili walioishi nae kwa zaidi ya miaka kumi kabla ya kufariki kwao nae na alipofuzu masomo yake ya udaktari hakutaka kuendelea kubaki nje zaidi ya kurejea nyumbani Tanzania ambapo alipokelewa na mamaake yule ambae alimuonesha mapenzi kama mtoto wake wa kumzaa mbali na ukweli kuwa mamaake mzazi hakuwa yeye.
"Mamaa mamaaa hebu nyamazeni basi mnambie nini kimetokea! Eti we mzee umeleta habari gani tena iliyomkosesha furaha mamaangu?"
aliuliza kwa hasira Asha na kumuangalia Hussein bubu ambae yeye aliacha kulia kwa sauti na kukaa kitako akimtazama Asha akiwa haamini kama hii leo anakutana na mwanae ambae hakuwahi hata kum beba akiwa mtu mzima tena mrembo na asilimia kubwa alifanana na mamaake ambae alikuwa mwanamke wa kwanza kumpenda kwa dhati Hussein mbali ya kuwa alikuja kumtenda vibaya.
"Asha, hapana mwananguuuu.... Usiongeeee kwa sauti hiyooooo... aaaaaaah Najua itakuwa ngumu kuelewa harakaharakaaa mamaaa .. ila huyo mzee unayemuona mbele yakooo ndiee....ndieeeee.... ndie babaako Mzaziiiiii....hiiiii"
aliongea kwa kujikaza kisabuni yule mama mbali ya kuwa alikuwa na uchungu mzito moyoni mara baada ya kujitonesha kidonda cha kumkumbuka marehemu dadaake.
"Whaat!! Mamaaa!!?.."
alitaharuki Asha na kugeuka kumtazama Hussein kwa mshangao wa hali ya juu na kumtazama tena mamaake ambae sasa nae alikaa kitako na kuanza kujifuta machozi kwa kanga huku akimuangalia mwanae Asha ambae alikuwa bado kataharuki.
"Asha mwanangu, huyo ni babaako.. Huyo ndie Hussein babaako ambae tulikuficha ukweli miaka yote ila leo nitahadithia kila kitu na yoote ambayo huenda hata Shemeji Hussein hukuyajua... naomba Asha unisikilize kwa umakini sana mwangu."
aliongea kwa uchungu Zena huku akijifuta tena machozi ambayo yalikuwa hayakomi kumtoka na kumfanya Asha aungane nao na kukaa kabisa pale chini huku upande wake wa kushoto alionekana Hussein na kulia kwake alionekana mamaake ambae ni Zena.
"Asha... Asha kwanza naomba utambue mimi si mamaako mzazi, nimeumia sana leo na naikumbuka sana barua ya dada aliyoniachia sambamba na maneno yake ambayo yote yalisafiri na maji mara baada ya mafuriko siku chache baada ya kifo chake kabla hawajaja wale wafadhili kukuchukua kwa msaada ulipokuwa darasa la nne baada ya kupita miaka sita ya maisha magumu na maajabu yako shuleni.
Mwanangu japo ilionekana sahihi kukuacha uende kulelewa na watu wengine tena ukiwa na umli wa miaka kumi tu na japo faida yake nimeiona na naiona mapaka sasa unanilea lakini ukweli nimeenda kinyume kabisa na maagizo aliyoniachia dadaa ambae ni mamaako. aaagh! Hussein unisamehe sikuwahi kumleta Asha wala kumwambia ukweli ambao dada alinisisitiza pindi atapokua nimwambie...
Eee Mungu nisamehe lakini sidhani kama nimechelewa, naahidi sasa nitawaambia ukweli wote nilioujua kuhusu Asha Dada na Hussein."
sauti ya mkwaluzo iliyoonesha dhahili imebeba maumivu mazito kutoka moyoni ilisikika ikitoka midomoni mwa Zena na kumfanya hata Dk Asha aanze kulengwa na machozi huku Hussein bubu yeye ndio kabisa alibaki kaganda kama sanamu akili na masikio yote aliyaelekeza kwa Zena japo macho muda wote yaliganda kwa Asha.
Alimeza funda la mate Zena huku akirekebsha sauti yake kwa kukohoa kidogo kwa kujikaza kiume na kuanza kusimulia kisa chote kilichokuwa nyuma ya pazia juu ya maisha ya Mariam na Asha......
MIAKA 23 ILIYOPITA
..................Simulizi Ya Zena....................
Sintoisahau ile siku dada aliponipigia simu akiwa anaongea kwa shida sana akinisihi niende haraka kwake kwa sauti ambayo ilinitisha na kunipa wasiwasi hali iliyonipelekea niache shughuli zote nilizokuwa nafanya nyumbani na kukimbilia kituo cha daladala pasi na kumuaga yeyote wala kumsubiri mama ambae alikuwa ameenda kwenye shughuli ya harusi ya mtoto wa rafikiake mwananyamala,
nilisimama kituoni na muda mfupi ilitokea daladala iliyokuwa inaelekea kule nilipokuwa naenda ambako ndipo alipopanga dada Mariamu na mara baada ya daladala ile kusimama kituoni nilipanda na baada ya mwendo wa dakika kadhaa gari ilifika kwenye kituo nilichokuwa nashuka na kushuka huku nikitembea mwendo wa haraka haraka kumuwahi dada ambae nilikuwa najua kuwa anaumwa lakini sikuwahi kuwaza kama ugonjwa aliokuwa anatuambia ungeweza kumzidia na kumfikisha katika hali mbaya kiasi kile kama nilivyotafsiri kupitia sauti yake niliyoisikia simuni muda mfupi.
Sikuamini pindi nilipoingia ndani moja kwa moja na kumkuta mtoto wa dada ambae ni Asha kipindi hiko akiwa na miaka minne tu akiwa analia pale chini huku akimtingisha mamaake aliekuwa amelala huku nzi wengi wakiwa wamemjalia sehemu ya koo na mdomo ameuacha wazi ulimi kiwa umemtoka mithili ya mtu aliyekuwa amebanwa na kitu shingoni.
'Daaadaa!!....daadaaaa..!' Niliita kwa uchungu na kumsogelea pale chini huku machozi yakinitoka nikiwa sielewi nini kimempata dadaangu kufikia katika hali ile ya kushindwa hata kuitika na kubaki akinitazama tu huku macho yake yakitokwa machozi mfululizo na kunijengea imani ni kiasi gani alikuwa anapata maumivu makubwa sana ya ugonjwa ambao hadi dakika huo nilikuwa sijaujua hadi pale nilipojitutumua kumuinua kwa lengo la kumrudisha kitandani kabla sijafanya taratibu za kuita gari ya kumuwahisha hospitali na hapo ndipo niliposhangaa kuona uchafu uliokuwa unatoka chini kidogo ya shingo ya dada karibu na eneo la bega tena ajabu ulikuwa unatokota kadri alivyokuwa anataka kujaribu kusema kitu ama kumeza mate na kunifanya nitaharuki na kugundua sababu za nzi wengi kumzonga dada Mariamu.
'Aaaaaaaah..daadaangu nini tena kimekupata?!!'
Nilijikuta najisemea mwenyewe huku machozi yakinitoka kila nilipokuwa namuangalia na Asha alivyokuwa analia tena huku akiwa kashika bakuli ya plastiki mkononi akitingisha miguu ya mamaake bila kujali uwepo wangu.
"maamaaa tata ujiiii... mama ujiiiii.."
Sauti na maneno ya Asha yalizidi kuniliza na kubaini kuwa zaidi kilichokuwa kinamliza Asha ni njaa na ilionesha wazi hakukupikwa chochote siku hiyo toka asubuhi na masikini ya Mungu mtoto mdogo kama Asha ambae bado akili yake ilikuwa haijakomaa, hakuwa anajua nini kimempata mamaake hadi wamekaa na njaa muda wote na hakuwa na chochote cha kufanya kwa umli wake zaidi ya kumtingisha kwa kumuamsha mamaake apike basi huo uji ambao niligundua ndio kilikuwa chakula kikubwa alichokizoea yule mtoto.
Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kutoka kuomba msaada kwa majirani mara baada ya milango mengine miwili ya ile nyumba iliyokuwa na vyumba vitatu tu alipopanga dada kuonekana makufuri yakining'inia na kuashiria wahusika hawakuwepo na kwa bahati mbaya hata wale majirani niliowafata ambao asilimia kubwa niliwakuta wanawake baada ya waume zao kuwa kwenye mishughuliko hawakuweza kabisa kunipa msaada.
Hali hii ilinishangaza mno kwanini wale majirani wamekuwa na roho mbaya kiasi kile kwani kila niliyemfata kumuomba tena huku nikiwa nalia kama mtoto alionesha kunihurumia na nia ya kunisaidia lakini nilipomuelekeza nyumba yenyewe basi hubadilika na kuzuka sababu nyengine tofauti huku wengine wakidiriki kunicheka kabisa na kunitajia kiasi kikubwa cha pesa kama nitakuwa nataka msaada wao.
Nilihumia na sikujua sababu za msingi kwanini waltu wa pale walimchukia sana dadaangu na kushindwa kunisaidia walau kumbeba kumfikisha barabarani stendi ya Taxi kwani kiukweli eneo lile alipokuwa anaishi dada hakukuwa na njia ya kuruhusu gari lolote kufika hata bajaji.
Sikuwa na jinsi nilijikaza tena kiume na kupiga moyo konde nilikimbia kama mwizi ama kichaa moja kwa moja hadi pale stendi na kuwaita vijana wawili ambao nilipatana nao kiasi furani cha pesa na kukubaliana nami kwenda kum beba huyo mgonjwa kumleta kwenye Taxi ambayo nayo niliongea na dereva wake aliekubali kutusubiri.
Nilitangulia ndani na kumfunika dada vizuri hususani sehemu za juu kuuficha uchafu uliokuwa unavuja na kutoa harufu kali kwa kitenge changu ambacho nilijifunga kiunoni na kujikuta nabaki na skin tight ndefu ambayo awali nilikuwa siwezi kutembea mtaani nikiwa nimevaa yenyewe tu pasi na kujifunga walau kanga ama kitenge lakini siku hiyo nilijikuta najisahau kabisa kwa kuchanganyikiwa na laiti kama nisingekuwa na walau hiyo skin tight basi hata uchi kabisa ningetembea pasi na kujijua wala kujihisi.
Lakini kila nilipokuwa namuangalia dada alinionesha machoni kuwa kuna jambo anataka kunambia lakini anashindwa na nilipomtazama kwa makini alinipa ishara kwa kuangalia kwenye dressing table yake na kuniangalia mimi, alifanya vile kama mara tatu ndipo nilipoenda kuangalia hapo kwenye dressing table kuna nini na nilipekuwa kuangalia ndipo nilipoiona bahasha kubwa ya barua ikiwa imeandikwa jina langu kwa nje na ndipo nilipomuangalia dada ambae aliniashilia kwa macho kuwa ndio hiko kitu alichomaanisha lakini kwangu sikuona umuhimu wa kukaa chini kuanza kusoma barua wakati dadaangu amelala anateswa na maumivu makali..!!
Nilichofanya niliitumbukiza kwenye handbag yangu ile barua na
kuwaruhusu wale vijana waingie ambapo walipoingia niligundua mshtuko wao na adha ya harufu ya ajabu waliyokutana nayo mule ndani ambayo mimi sikuihisi nilipoingia hadi pale nilipojionea kidonda cha dada kilichokuwa kinavuja uchafu na hata hivyo sikukerwa hata chembe kwa ile harufu zaidi ya kuniongezea simanzi.
"Dada, mzima huyu?"
"Aaagh! Fanu maswali gani hayo? we kamata huko tum bebe tumpeleke.... unauliza mzima!! sasa toka lini mtu aliyekufa akawa anatoa ukoromo?"
maneno ya kijana wa mwanzo yalinichoma sana japo sikuweza kujibu chochote lakini niliumia sana kuona dadaangu kipenzi akifananishwa na maiti angali yu hai kwa kigezo cha ile harufu..!?
Aaaaah!! ama kweli wanaadamu tunakufuru kubwa.
Afadhali kauli ya yule mwenzake aliyemjibu kidogo ilinifurahisha japo sikuipenda pia kwani dadaangu alikuwa hakoromi bali alikuwa anaugulia maumivu makali aliyokuwa anayapata lakini kile kidonda ndicho kilichokuwa kinaifanya sauti yake kusikika kama mkoromo kutokana na kutokota kwake kadri alivyokuwa anachezesha koromeo.
Nilimnyanyua na kum beba Asha ambae bado alikuwa kashikilia bakuli lake akilia na kutoka nae nikiwa nyuma ya wale vijana waliom beba dadaangu Mariam na sikukumbuka hata kufunga mlango zaidi nilikuwa makini na kumshika Asha ubavuni nilipom beba kutokana na kulia kwake na nilipandwa na hasira zaidi mara baada ya kupita hatua chache kwa majirani wale ambao walininyima msaada awali na kuwakuta wameeka vigenge vya umbea kwenye baraza zao huku macho yao yakiwa kwetu na tolipofika karibu walinyamaza na kuishia kutututazama na tulipopita ndipo waliangua kicheko kikubwa kwa pamoja.
'''HEEHEEEEEE KAPIMEEEEEEEE'''
Nilitamani nirudi nikachambane nao lakini nilishindwa na kubaki nimefura hasira iliyochanganyika na maumivu mpaka tulipofika pale stendi ambapo kila aliyetuona hakuacha kutushangaa wakati dada alipokuwa aningizwa kwenye ile Taxi nami nikamnunulia soda na Keki mbili Asha mara baada ya kumalizana na wale vijana,
na hapo kidogo kelele za kilio cha mwanangu Asha zilipungua pindi tulipoingia kwenye ile Taxi na kumueka mbele huku mimi nikikaa nyuma na kumpakatia dada ambae sauti aliyokuwa anaitoa iliyo mithili ya ukoromo ilizidi kuongezeka na kuniumiza zaidi kwa kugundua kuwa maumivu yanazidi mwilini mwa dadaangu kipenzi.
Nilimuamuru dereva kutuwahisha mwananyamala hospitali na kumpigia simu mama muda uleule gari ilipoanza kutoka na kumuelekeza hali ya dada huku nikimficha juu ya kidonda cha ajabu kilichokuwa shingoni kwa dada kwa kujua kuwa mamaangu anakuwaga na uoga unaoambatana na presha ya kushuka hasa anapomuona mwanae anaumwa sana ama kazidiwa hivyo hata ile kauli yangu kuwa nampeleka hospitali ilitosha kumstua kule aliko na mara baada ya taxi yetu kufika hospitali mwananyamala niliwakuta tayari mama na baadhi ya rafiki zake waliokuwa kwenye shughuli wakiwa na nyuso za huzuni getini huku mamaangu akiwa peku kabisa licha ya kuwa alitoka nyumbani akiwa amependeza na zaidi alivaa viatu ambavyo alinunuliwa na dada Mariam.
Ilibidi nishushe kioo na kuwapungia kuwaelekeza kuwa Taxi wanayoitazama inayoingia sasa ndiyo niliyomo na kweli walianza kuifatilia hadi iliposimama ndani ya ile hospitali na ndipo mama alipoingia kumchungulia dada pindi nilipomuacha na kwenda kuwaita manesi ambao walikuja haraka na kitanda cha matairi kwa nia ya kuja kum beba dada.
Moyo uliniuma sana nilipotoka na kumkuta mama akiwa analia huku ameshikwa na wale shoga zake na manesi wa mwananyamala sitoweza kuwasahauuu..... aaaaaagh nakumbuka jinsi walivyokuwa wanampakia dada kwenye kitanda kile mithili ya mzigo mbali na kelele za ukoromo wa maumivu na kusababisha kile kitenge nilichomtanda kwa kuziba eneo lile la jeraha kufunuka na kudondoka na hapo kila mtu aliyekuwa jirani alistaajabu kushuhudia ule uchafu ambao hata mimi nilishangaa kuona umezidi mara dufu huku lile tundu likiwa si dogo kama nilivyoona awali bali liliongezeka na ilitaka moyo sana kulitazama.
''"Aaaaaaaaaaaaaaaaaaagh, Mariaaaaamu Mwananguuuuuuuuu"''
Sintoisahau kauli hii ya mama angu.. mamaetu kipenzi aaagh,
Sikujua kabisa kama ile siku niliyomuambia 'mama umependeza sana leo umekuwa kijana kabisa' asubuhi yake pindi aliponiaga anakwenda kwenye shughuli ya harusi ya rafiki ake wa miaka mingi Mwananyamala kama itakuwa ndio siku yetu ya mwisho kucheka pamoja....!
Aaaaah sikuwaza wala kuhisi kama ipo siku mamaangu atanitoka ghafra namna ile tena mbele ya macho yangu na watu wengi kiasi kilee aaaah, masikini Zena mimiii nitalia na nani na tulizaliwa wawili tu na dadaangu ambae ndio nae alitoa ukoromo wa sauti ya juu uliotokea kwenye lile tundu na kurusha uchafu mwingi sambamba na damu mithili ya bomba mara baada ya kitenge kilichokuwa kinaburuza na kukanyagwa na nesi kudondoka na mama kupiga ule ukelele uliopelekea kuanguka chini.
aaaaaaaaaah kwanini hamkunambia ndugu zangu kama mmepanga kuondoka pamoja kwenye ulimwengu wa mauti na kunifanyia suprize iliyoutesa moyo wanguuu na kuniachia upweke wa milele!!??...... aaaaaaaaaaah
Nilijikuta nami nawasindikiza mama na dada kwa kupoteza fahamu pindi nilipokuwa nashuhududia vifo vyao ambapo mama alitapatapa na kukata roho pale chini muda mfupi baada ya kudondoka huku dada Mariam nae alimalizikia muda mfupi baada ya kutoa ule mkoromo mkubwa mithili ya firimbi uliorusha mafunda ya uchafu na damu.
Sintosahau maneno ya yule daktari alipokuwa ananipa maelezo ya uthibitisho wa vifo vya ndugu zangu siku moja baadae pindi nilipopata fahamu na kuruhusiwa wodini.
Alinambia kuwa kifo cha mamaangu kilisababishwa na presha iliyoshuka ghafra kupita kiwango vilevile dadaangu Mariam kifo chake kilisababishwa na kansa hatari ya koo.
Sintosahau kabisa hata mara baada ya ndugu na majirani kuungana nami hospitali na kuchukua maiti kurudisha misiba ile ya kihistoria moyoni mwangu mpaka nyumbani na baada ya taratibu za mazishi kukamilika hatimae mama na dada wote walizikwa siku moja na makaburi yao yalifatana. aaaah! Mungu awaeke mahali pema.
Siku moja kupita baada ya mazishi ilibidi nitoke na vijana wa kiume wachache sambamba na mzee wetu wa mtaa tuliokuwa tunaishi tuliyezoea kumwita babu japo hakuwa na undugu wa damu na sisi lakini alikuwa jirani mwema na alisifika kuwa mzee mwenye busara sana.
Safari yetu ilikuwa ni kule alipokuwa anaishi dada Mariam kwa niaba ya kukusanya vitu vyote lakini hatukuamini baada yakufika na kukutana na habari za uvamizi na wizi uliotokea siku moja iliyopita ambapo vitu vyote muhimu vya dada viliibiwa na chumba kubaki cheupe mithili ya mtu aliyehama.
Japo ilituuma lakini tulipiga moyo konde na kushukuru tu, kwani iwapo tumempoteza mtu kabisa sembuse hivo vitu?
tuliwaaga wale wenyeji tuliowakuta kwenye vile vyumba viwili ambavyo siku ile nilipokuja kumchukua dada vilikuwa na makufuri tu.
Yule mzee alinisaidia kuongea na wale majirani visilani mara baada ya kumuhadithia mkasa ulipoanzia ambapo kwa busara zake aliweza kuambua sababu kuwa kumbe dada Mariam alikuwa ni mtu wa kujiona ona sana kipindi anaishi pale na mashoga zake watatu waliopanga pamoja huku mmoja wao akiwa si mwanamke bali ni shoga kabisa tena mbaya zaidi waliitumia ile nyumba kama dangulo la kuingiza wanaume hali iliyokuwa inawakera sana majirani kwa vile kujiona kwao, kutoshiriki kwenye misiba ya wenzao na matatizo mengine huku wakiwa ni watu wenye nyodo nyingi na ndio sababu kuu za kuwachukia wote na kuwatenga. Hapo kidogo nilielewa lakini bado sikulidhika na yale waliyonionesha lakini niliamua yote kuyapuuza na kurudi nyumbani sambamba na yule mzee na wale vijana.
ulipita mwezi mmoja baada ya kumaliza matanga ndugu wote walitawanyika na kuniacha nikiwa na mwanangu Asha mtoto wa marehemu dada bila msaada wowote wa kimalezi zaidi ya kuniachia maneno ya pole na maisha mema na huo ndio ukawa mwanzo wa maisha mapya ya misukosuko na mazoea baina yangu na Asha.
Lakini kabla hazijaanza tabu na misukosuko ambayo sikutaraji kama yatatukuta mimi na mwanangu yule niliumizwa na kulizwa na kitu kimoja ambacho nilikikumbuka mwenyewe baada ya kusahau kwa muda mrefu..... Kitu chenyewe ni barua, barua ambayo ilionesha wazi kwa nje ilinihusu mimi, barua ambayo sikujua imebeba nini hasa ndani yake, barua ya mwisho ambayo muandishi wake nilijua kama hatoniandikia tena barua nyengine milele, ila kwa barua ile niliweza kuihisi sauti yake akiongea pindi nilipokuwa nasoma hati ya maandishi yake, barua toka kwa marehemu dada Mariam ambayo licha ya kupotea kwake kutokana na janga kubwa la mafuriko ya mwaka lililokuja kutokea wiki chache baada ya kuisoma lakini maneno yake yaliendelea kuishi akilini mwangu kila nilipomkumbuka yeye ama nilipomuangalia Asha.
Barua yenyewe ilikuwa hivi............
Itaendelea. .....