Muziki wa Wadhamini
Naamini ukimya uliotamalaki humu kwa makelele haumaanishi mmelala bali mnavuta pumzi, kitu ambacho ni muhimu sana.
Kapuku nakushukuru sana na umuhimu wako humu, yes wewe unayesoma hapa hauelezeki, sina kipimio cha kupima umaarufu wako. Tumeamka asubuhi kwa magazeti na
shululu , BBC na UF chini ya lianko langu
lee empire , na tukashukuru kwa sala na
Shunie . Nani hakuipitia historia ya leo nimwambie
Jimena atukumbushe na kisha tukapata 10 kubwa na mtaalamu mwenyewe
Bitoz , asanteni sana wadau. Na sisahau mambo ya michezo chini ya mtaasisi mwenzangu
Nyagei
Sitaki kuharibu mchango wa mdhamini wetu wa usiku huu
Shunie ambaye hatajali endapo nitawakumbuka wafuatao maana ninawakumbuka sana na wakiburudika na hizi nyimbo ni furaha kwangu, uko wapi
husna muba , Arusha baridi limekufunika
Clkey , mama wawili
Tumosa unajua unavyonifanya kujisikia amani hapa unaniunga mkono kwenye harakari zangu, simsahau
Mondray na
Transcend mapumzikoni. Uko wapi
Mkushi wa kusi ,
Mndali ndanyelakakomu ,
mzeewakungoa ,
Madame S ,
koncho77 ,
dingimtoto ,
dumejeuri demi usipotee sana,
Linamo ,
BlessedHope umemisika sana.
Mdhamini ambaye ambaye ni aunt yangu hatajali kuwataja wadau hawa hapa. Nisimkasirishe mdhamini kwa blah blah zangu akaninyima safari yangu muhimu.
na hapa anakuja Darasa na B. Pol
tuwe na usiku mwema makapuku wote