Makapuku Forum

Muziki: Kwanini Isiwe Mbili Wakati Una Moja

Ni Jumatano leo na inaishiria, naamini hakuna ubaya nikijiaminisha kuwa umekuwa na siku nzuri sana leo ambayo ni mwangwi wa namna siku ya kesho itakavyokuwa. Kama haikuwa siku yako, worry not, kesho ni siku nyingine tena na kama ada, jua litawaka tena. usisubiri sana though.

Hakuna ubishi kuwa wote, well nisifanye sweeping generalization maana huchelewi kutaka datum ambayo kiukweli haya ni mawazo yangu tu na nimejiamisha tokana na kuyakabili mazingira. Kuwa na wivu wa maendeleo si kitu kibaya, kukinzana kwa ajili ya kurahisisha maisha si jambo baya, kutofautiana kwa ajili ya kujenga umoja si jambo la kukemewa. Kila mmoja ana mawazo sahihi kwa wakati sahihi, na leo nakukumbusha tu kuwa kuridhika si tabia ya mwanadamu. Tufanye tunayofanya kwa ajili ya kujiletea maendeleo na kurahisisha maisha. Popote ulipo hongera sana kapuku kwa kile unachofanya.

Muziki sasa, wakati wanaanza walikuwa watatu Nhlanhla Nciza, Theo Kgosinkwe na Tebogo Madingoane baadaye Tebogo mwaka 2004. Wanaitwa Mafikizolo, na pamoja na kifo cha Tebogo bado wameendelea kufanya vizuri katika muziki wakichanganya mitindo ya kisasa na ile ya jadi na kuwafanya kuwa ni kundi la kipekee ambalo maonesho yake huhudhuriwa na wapenda burudani wengi.

Burudika Kapuku muheshimika na kumbuka, wewe ni mtaalamu unayelifanya Jukwaa hili liwe la kipekee.



Baadaye tutakuwa na chaguo la Wapendanao na leo mtaasisi mwenzangu kajaa kwa chaguo lake

Asante Obe kwa music
 
Muziki wa Wadhamini

Naamini ukimya uliotamalaki humu kwa makelele haumaanishi mmelala bali mnavuta pumzi, kitu ambacho ni muhimu sana.

Kapuku nakushukuru sana na umuhimu wako humu, yes wewe unayesoma hapa hauelezeki, sina kipimio cha kupima umaarufu wako. Tumeamka asubuhi kwa magazeti na shululu , BBC na UF chini ya lianko langu lee empire , na tukashukuru kwa sala na Shunie . Nani hakuipitia historia ya leo nimwambie Jimena atukumbushe na kisha tukapata 10 kubwa na mtaalamu mwenyewe Bitoz , asanteni sana wadau. Na sisahau mambo ya michezo chini ya mtaasisi mwenzangu Nyagei

Sitaki kuharibu mchango wa mdhamini wetu wa usiku huu Shunie ambaye hatajali endapo nitawakumbuka wafuatao maana ninawakumbuka sana na wakiburudika na hizi nyimbo ni furaha kwangu, uko wapi husna muba , Arusha baridi limekufunika Clkey , mama wawili Tumosa unajua unavyonifanya kujisikia amani hapa unaniunga mkono kwenye harakari zangu, simsahau Mondray na Transcend mapumzikoni. Uko wapi Mkushi wa kusi , Mndali ndanyelakakomu ,mzeewakungoa , Madame S , koncho77 , dingimtoto , dumejeuri demi usipotee sana, Linamo , BlessedHope umemisika sana.

Mdhamini ambaye ambaye ni aunt yangu hatajali kuwataja wadau hawa hapa. Nisimkasirishe mdhamini kwa blah blah zangu akaninyima safari yangu muhimu.



na hapa anakuja Darasa na B. Pol



tuwe na usiku mwema makapuku wote

Nawe pia Obe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom