Makapuku Forum

Makapuku Forum

Katika dondoo za bbc. ...

........Idara ya Usalama ya Israel imeamua kuondoa vifaa tata vya uchunguzi katika masuala ya usalama katika eneo takatifu mjini Jerusalem,mahala ambapo Waislam wanapaita Haram al-Sharif na Wayahud wanapaita hekalu la mlimani.

........Mdahalo wa wagombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya hatimaye umefanyika mjini Nairobi. Sehemu ya pili ya mdahalo huo, kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alijikuta yuko jukwani peke yake baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutoshiriki mdahalo huo uliomalizika jana Usiku

........Katika mfululizo wa kuangazia wagombea nane wa Urais katika uchaguzi mkuu ujao nchini Kenya leo tunamuangazia Dr. Japheth Kavinga Kaluyu.

......Ripoti ya global witness imebaini kuwa DRC imepoteza asilimia 20 ya
mapato ya madini karibu dola za kimarekani milioni 750 zinazopita mlango wa nyuma na kupoteza mapato ya serikali katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

.........Jana ilikuwa ni siku ya mwisho kwa mamilioni ya watu ambao wamefanya kazi kinyume cha sheria nchini Saudi Arabia kuondoka katika himaya ya ufalme huo au kukabiliana na faini ama kifungo.

.......Wakati matokeo ya kura za Urais yalipotangazwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya, vita vilizuka kutokana na madai ya udanganyifu.

-Miaka kumi baada ya ghasia zilizotokea nchini Kenya baada ya Uchaguzi wa mwaka 2007/2008 wakenya wanaelekea kwenye uchaguzi mwingine je wamejifunza lolote kutokana na uchaguzi uliopita.

........Zikiwa zimebaki wiki chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini Kenya, baadhi ya wanasiasa nchini humo wamenukuliwa wakiirushia tuhuma nchi ya Tanzania kuhusika na uchaguzi huo ikiwemo kuanzishwa kwa vituo vya kuhesabia kura .
 
Ni faida gani basi mliyopata siku zile kwa mambo hayo mnayoyataharikia sasa? Kwa maana mwisho wa mambo hayo ni mauti

Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru na kuwa mbali na dhambi na kufanywa watumwa wa Mungu mnayo faida yenu ndiyo kutakaswa na mwisho wake ni uzima wa milele

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu
WARUMI 6:21:23

Muwe na asubuhi iliyo njema mbarikiwe sana
Ubarikiwee sana mke wangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom