Makapuku Forum

Makapuku Forum

Leo katika Historia

2012 - Robert Ledley anafariki Dunia.
Ni mgunduzi wa kifaa cha Ct Scan toka nchini Marekani.
25576daedfb11126818d9cf447d3f956.jpg
fefa67f733b70fa55b9fc1a428bb98ad.jpg
854beb8925432a2aabcfe110f6ffa52f.jpg

Alikuwa na umri wa miaka 86
Alikuwa ni mtaalamu wa Fizikia,Hisabati,meno na. Kompyuta
Hivyo alichokifanya hakubahatisha
. ......
 
Wale wapenzi wa mr naniiiìii najua mmemisiiii ebhu niwakumbukeeee kidogooooo......but sorry ratiba zinakuwa ndivyo sivyo....


Sehemu ya 33....

"Dokta Asha.. Dokta Asha hakika nakupenda sana. Naomba ukubali niwe wako ili tuunganike na kuwa mwili mmoja kama Mungu alivyoagiza wanadamu wenye jinsia tofauti tuishi duniani. Nahitaji uwe mke halali siku za usoni ili tuzidi kutengeneza ukaribu na kuzalisha familia bora pamoja. Naomba unikubali Asha na kama utanikataa naomba uthibitishe mbele ya wote wanaonisikia sasa hivi humu ndani. Kwanini niutese moyo wangu kwa kuficha ukweli halisi uliomo? Nakupenda sana dokta Asha nikubali tafadhali..!"
Maneno ya Shebby yalimstua kila mtu aliyekuwa ukumbini na kufanya watu wote wamgeukie Dokta Asha ambae alijikuta anainamia chini kwa aibu na mshangao. Hakuamini wala kufikiri kama kweli mgonjwa wake angekuwa na ujasiri mkubwa kiasi kile kumtongoza mbele za watu tena kwa kipaza sauti japo hata yeye mwenyewe alishaanza kuwa na hisia nae. Kila mtu alitamani kumsikia Dokta Asha nini atasema baada ya Shebby kutumbua ukweli wa moyo wake na kuuweka hadharani.
Mzee Mwinchande alitabasamu sambamba na mkewe mara baada ya kumsikia ukweli wa moyo wa mtoto wao na kuanza kumpigia makofi kwa ujasiri aliouonesha na kuwafanya watu wengine taratibu wampigie makofi Kamishna Shaaban. Hapo ndipo mshereheshaji naye alipochombeza maneno ya bashasha na kumtaka DJ apige wimbo wa Queen of My Heart (Malkia wa moyo wangu) ulioimbwa na Westlife ili umsindikize dk Asha pindi anaponyanyuka kusogelea kipaza sauti kumjibu Kamishna Shaaban baada ya kuutoa ukweli hadharani. Wimbo uliwekwa na mshereheshaji alimuomba tena Asha asimame na aseme chochote juu ya hisia zake kwa Kamishna Shebby. Huku akiwa ameinamisha uso kwa aibu Dk Asha alinyanyuka. Ingawa aibu ilimjaa machoni lakini furaha haikujificha. Uso wake ulinona furaha na machozi yalimbubujika. Moja kwa moja alikwenda kumkumbatia Kamishna Shebby pasipo kusema chochote kwenye kipaza sauti. Kama kumkumbatia tu haikutosha alimparamia mdomoni na kumtandika busu zito la huba. Hiyo ilitosha kuubainisha umma uliokuwa mahala pale kwamba alikubali kwa moyo mmoja kuwa na Shebby. Ilibidi wapigiwe makofi na kila mmoja kugongeana glass na mwenzake na shamra shamra za siku ya kuzaliwa ziliendelea kunoga.
Na hivyo ndivyo mapenzi baina ya kamishna Shebby na Dokta Asha yalivyoanza rasmi.

*******

Ndani ya gereza siku tatu baadaye Hussein bubu anastushwa na taarifa za kutoweka kimaajabu kwa yule mfungwa rafiki yake aliyetokea kuzoeana naye haraka.
Hakuzielewa haraka tetesi zile ambazo zilizuka kwa wafungwa wengine ambao walikuwa wanalala selo moja na CJ4. Hussein alichelewa kuhabarika kutokana yeye kuwa upande mwengine ambao alihamishiwa kipindi cha nyuma kwa msaada wa Kamishna Shebby.
"Kha! Ina maana kafanikiwa kutoroka?! Sasa katoroka toroka vipi? au alikuwa jini yule?" Maswali yalimuumiza kichwa Hussein baada ya kuthibitisha kuwa yule kijana hayupo tena ndani ya gereza na kuna timu ya maaskari ilitumwa kufanya msako juu yake.

|*MKUYUNI*|

Kipindi sintofahamu juu ya Cj4 kutoweka gerezani ikizidi kutafuna vichwa vya maafande, upande wa pili ndani ya kijiji cha Mkuyuni stendi ya mabasi iliyokuwa mkabala na soko, alionekana kijana mmoja aliyevaa nguo chakavu akishuka kwenye roli lililotokea mjini na kuja pale mkuyuni kwa ajili ya kupakia ndizi.
Akiwa kabeba mfuko wa rambo mkono mmoja kashika pingili ya mua aliokuwa anaumenya taratibu kwa mdomo huku akipiga hatua kutokea kule kwenye roli mara baada ya kumshukuru dereva kwa lifti aliyompatia. Miguu peku bila viatu alizidi kuchanja njia kuelekea mabondeni. Watu wengi aliokuwa anapishana nao hususani wenyeji walimshangaa wakishindwa kumtfasiri ni chizi mpya ameibukia kwao au ni mtu timamu aliyepigika na maisha?
"Samahani babu shikamoo" Alisalimia yule kijana alipokutana na babu mmoja akiwa kabeba jembe begani.
"Asante mzukulu, kugenda kwani?" Aliitika na kuuliza yule mzee ambaye Kiswahili chake hakikuwa kizuri zaidi aliongea kwa lugha ya kiruguru ambayo haikumpa tabu sana yule kijana.
"natafuta sehemu mzee nitayoweza kupata chumba cha bei nafuu sana niweze kujisitiri"
"Ng'andaaa mh! tuke huku kwani we mgeni mzukulu?"
"Ndio babu"
"Onaa! Tapata kuno kule hakuna ng'anda zimema." Aliongea yule babu na kumuongoza njia yule kijana hatimaye wakafika kwenye kijiji kimoja ambapo kulikuwa na nyumba ambayo ilikuwa kama imetelekezwa kutokana na matukio yaliyowahi kutokea mtaa ule. Alionekana kichaa mmoja wa kike akiwa pekee anayeishi pale.
"Ahano ng'anda hii mzukulu tuke kwa mjumbe ukamlongele akusaidile utawasa tu mzukulu." Alimuonesha ile nyumba yule mzee kisha kwenda naye sambamba kwa mjumbe ambaye hakuwa mbali na eneo lile na ndiye alikuwa kama mmiliki wa haki ya nyumba ile. Walipofika mzee alisalimiana na mjumbe kisha kumkabidhi mgeni wake huku akimsisitiza amsaidie.
"sawa kijana karibu, Enhee umetoka wapi, unaitwa nani, na ipi hasa shida yako"
"Mzee mi naitwa Ndonga ni mgeni kabisa nimetokea Kilosa nilipoenda kumtafuta kaka yangu ambaye sikufanikiwa kumpata baada ya kutoka kwetu Kigoma na kumtafuta kwa muda mrefu hadi nikakosa muelekeo pale Kilosa, ndipo nilipoelekezwa kuwa alihamia hapa mkuyuni sasa naomba unisaidie sehemu ya kulala hata kwa kulipia pesa kidogo kwani uwezo wa kulipia nyumba ya wageni sina. Tafadhali sana mjumbe naomba msaada wako nihifadhi mtoto wako." Aliongea kwa lugha ya upole na unyenyekevu yule kijana na kumfanya mjumbe amtazame huku akifikiria jinsi ya kumsaidia.
"Mh! kijana wanguuuu kiukweli hapa mkuyuni nyumba ni gharama japo unapaona kijijini ila kuna nyumba moja ambayo inaweza kuwa rahisi kuipata kwa kuwa ilikuwa ya marehemu babaangu kabla hajamuuzia mganga fulani ambaye naye alishafariki. Lakini sasa pale kuna matatizo kidogo yalitokea na watu wote waliikimbia ile nyumba kasoro mama mmoja ambaye kidogo akili zake hazipo sawa ndiye yupo pale. Sasa sidhani kama patakufaa ama wewe ulionaje?"
"Mh! mzee wangu yani mi siwezi kubagua sehemu ilimradi nihifadhi ubavu wangu kwa visiku hivi nikiendelea kumtafuta ndugu yangu."
"Sawa sasa itabidi nikuandikishe kisha nikupeleke sehemu yenyewe hapo mbele tu ila naomba uwe muangalifu usije kuthubutu kumghubudhi yule mama japo akili zake hazipo vizuri." Alionesha msisitizo mjumbe.
"ondoa shaka kabisa mjumbe Aaa! Mungu akubariki sana baba kwa msaada wako." Alishukuru huku akitoa noti ya shilingi elfu tano iliyochakaa sana kutokana na fundo alilolifunga sehemu za pensi lake alilofunga kwa mkwiji wa kamba ya mti. Mjumbe aliitazama pasipo kuipokea akamwambia.
"Hiyo itakusaidia katika matumizi yako mpaka utapompata nduguyo." Alisema na yule kijana akashukuru tena. Baada ya kuafikiana na mjumbe alipelekwa kwenye ile nyumba iliyokuwa imepooza mno kwa ukimya. Nje walimuona yule mama kichaa ambaye aliwaangalia tu bila kusema kitu na baada ya mjumbe kumuonesha chumba cha kutumia huku akimwambia.
"Kama utakaa wiki moja pasi na kuonana na huyo nduguye itabidi nikupeleke kwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa ili utambuliwe na ikiwezekana uandikishwe kama mkazi wa eneo hili ili kila mtu aelewe ujio wako."
"Sawa ndugu mjumbe." Aliitika na kukubali kwa kichwa.
Baada ya hapo Mjumbe alitoka mule ndani na kumuacha yule kijana akikung'uta mavumbi kwenye kile chumba kilichokuwa na mkeka na kigoda cha miguu mitatu tu.
"Shabbashh Hatua nzuri zinatengeneza nafasi nzuri pia!" Alijisemea mwenyewe yule kijana na kugonganisha mikono yake kwa tabasamu. Hakuwa mwengine yule kijana bali ni Komandoo Jumanne ama Cj4. Tayari aliianza hatua ya pili ya kazi aliyopewa kujua yaliyojificha nyuma ya vifo vya maaskari.

* * * * * *

Baada ya siku kadhaa kupita tangu kufanyike ile tafrija ya kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa Kamishan Shaaban na kuanza rasmi mahusiano ya kiuchumba baina yake na Dokta.
Siku hiyo walionekana wakiwa wawili maeneo ya fukwe huku dereva wao ambaye alikuwa ni mlinzi pia aliyetumwa na jeshi la polisi kwa niaba ya kuchunga usalama wa Kamishna Shebby, alikaa sehemu moja ya juu akiwaangalia wapendanao wanavyokokotana na kurushiana maji maeneo ya fukwe huku wakiwa na nyuso za furaha.
"Nakupenda sana Asha"
"Hata mimi Shebby tena nilikupenda toka siku ya kwanza nilipokuona"
"Haa acha utani Ashaa"
"Kweliii"
"sasa kwanini hukunambia mapema hadi nimekuanza mimi"
"aaah! si nlikuwa naogopaa!"
"tehtehteheee huyoo"
Basi ilikuwa upendo na mahaba maeneo ya fukwe pindi walipokuwa wanataniana na kuchombezana Kamishna Shebby na Dokta Asha.
Hata jioni yake waliporudi nyumbani kwenye jengo kubwa la kifahari la mzee Mwinchande, bado waliendelea na utani wa hapa na pale mpaka wanaingia kulala ambapo ulikuwa ni usiku wa tatu toka waanze kulala pamoja. Lakini kitu ambacho si rahisi kuaminika kwa mtu wa nje ni kuwa siku zote hizo Shebby na Asha bado walilala kindugu ndugu. Yaani hawakugusana miili tupu kushiriki tendo la kuvunja amri ya sita. Hii ilitokana na maelezo ya Dk Asha kuwa inahitajika Shebby aendelee kujiponesha zaidi na atapokuwa sawa aende kujitambulisha kwao pindi ataporudi na wakioana ndipo watapata uhuru wa kucheza sebene la huba pamoja muda wote kwa uhuru mkubwa na amani.
Shebby alimuamini Asha na akaa tayari kwa masharti ya kusubiri. Lakini kitu ambacho hakukijua kamishana Shebby ni pindi usingizi unapompitia kuna mchezo alikuwa anafanyiwa na Asha. Mchezo ambao ulikuwa na siri kubwa ya sababu za kufutika kwake kumbukumbu. Na hata siku hiyo Shebby alipopitiwa na usingizi tu, Dk Asha alitumia muda mwingi kumuangalia vizuri usoni na kumpekua sehemu za kichwa huku akimtazama kwa huruma na kumsikitikia. Kumbe pasipo kujua siku hiyo Shebby alikuwa macho na alijitegesha kulala tu kipindi Asha akimpekua na kumsikitikia alikuwa anamuangali kijicho pembe pasipo kufumbua vyema macho. Alama za maswali zimtwaa Shebby na papo hapo alifumbua kabisa macho na kumfanya Dokta Asha astuke.


..........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom