Makapuku Forum

Makapuku Forum

a6ca5d6dee6b6f10ff0d6f7b5943c427.jpg
Watu hawakubali kupitwa na fasheni vibongeeee oyeee
 
HUYU NDO CARL PETERS ALMAARUFU "MKONO WA DAMU" ANAYECHUKIWA MNO NA WATANZANIA.

Carl Peters mjerumani tapeli aliyewazuga machifu na kupoteza uhuru wao aliwahi kutamka kwamba, "kuwapa uhuru watu weusi ni kosa la kijinga lisilopaswa kufanywa na nchi za werevu", yaani watu weupe. Kwake yeye, watu weusi walikuwa ni watu wa kutumiwa tu.

Na kuthibitisha hilo, kila alikopita Carl Peters aliacha michirizi ya damu kwa ukatili usioelezeka aliowafanyia watu kiasi cha kupachikwa jina la "Mkono wa Damu".

Lakini wakati watanzania wanaadhimisha miaka 50 ya uhuru, Carl Peters hawezi kusahaulika kwa sababu yeye ndiye muasisi wa mipaka ya koloni lililokuwa linaitwa Tanganyika. Ni Carl Peters aliyewazuga na kuwatapeli machifu wa makabila mbalimbali na kuwaweka chini ya himaya ya Ujerumani.

Ni Carl Peters huyo huyo, aliyeratibu kwa karibu sana mkutano wa Berlin, huko Ujerumani wa mwaka 1884/85, ambapo mataifa ya ulaya yaligawana bara Afrika mithili ya shamba na kuhakikisha mipaka ya Tanganyika inakuwa kama ilivyo sasa (ukiondoa tu Rwanda na Burundi).

Kwa vyote vile, simulizi za vuguvugu la uhuru wa Tanganyika, haziwezi kukamilika pasipo kueleza mchango wake katika kueneza ukoloni. Yeye ndiye aliyekuwa kinara wa kufanikisha koloni la Afrika mashariki na kupelekea kile kilichoitwa kinyang'anyiro cha makoloni Afrika.

Harakati zake za kusaka makoloni ndizo zilizopelekea kuzaliwa kwa mipaka ya nchi inayoitwa Tanganyika ikiundwa na makabila takriban 150.

Simulizi zinasema kuwa Carl Peters alikuwa ni mjerumani mvumbuzi, mwanahabari na mwana filosafa aliyezaliwa tarehe 29 Septemba mwaka 1856 katika mji wa Hanover.

Baada ya masomo ya awali katika shule ya misheni ia Ilifeld, alijiunga na chuo cha Goettingen, Tubingen, na kasha Berlin ambako alisomea historia, filosofia na sheria.

Mwaka 1879, alihitimu Chuo cha Berlin akitunukiwa digrii katika historia.Mwaka uliofuata aliachana na kazi yake ya uanasheria na kwenda London, Uingereza alikoishi na mjomba wake tajiri.

Abuni Chama cha Makaloni ya Ujerumani
Katika kipindi cha miaka mine aliyokaa Uingereza Carl Peters, alijifunza historia ya Uingereza na kuchambua sera zake kuhusu makoloni na falsafa yake. Alirejea Berlin baada ya mjomba wake kujiua mwaka 1884 na kuanzisha Chama cha
Makoloni ya Ujerumani .

Akiwa na shauku ya kuona Ujerumani akijipatia makoloni, mwishoni mwa mwaka 1884 Carl Peters alisafiri kuja Afrika Mashariki kufanya mikataba na machifu.
Licha ya kutopewa kibali na Serikali ya Ujerumani, Carl Peters alikuwa na matumaini kwamba juhudi zake hizo zingesaidia Ujerumani kupata makoloni Afrika.

Baada ya kufika Bagamoyo hapo Novemba 1884, Carl Peters na msafara wake walitumia majuma sita wakiwashawishi machifu na waarabu kusaini mikataba ya ardhi na njia za kibiashara.

Moja ya mkataba unaojulikana sana ni ule aliomsainisha chifu Mangungo wa Msovero huko usagara (Kilosa) ambaye eti alikubali, "kumwachia himaya yake na watu wake na kila kitu" kwa "matumizi pekee ya mpango wa makoloni ya Ujerumani".

Carl Peters alirejea Ujerumani tayari kukamilisha mafanikio ya mipango yake Afrika. Tarehe 27 Februari 1885, kufuatia kumalizika kwa mkutano wa Berlin, Kansela wa Ujerumani Bismark alitangaza kuanzishwa kwa himaya ya Ujerumani Afrika Mashariki. Chama cha Ujerumani Afrika Mashariki kiliundwa mwezi Aprili na Carl Peters kutangazwa kuwa mwenyekiti wake.

Kwa kuanzia, kilomita 18 za ukanda wa pwani zilitambuliwa kuwa ni eneo la Sultan wa Zanzibar. Lakini mwaka 1887, Carl Peters alirejea Zanzibar na kupewa kibali cha kukusanya kodi. Hata hivyo, baada ya miaka miwili eneo hilo lilinunuliwa kutoka kwa Sultan wa Zanzibar kwa Paundi 200,000 na kwa kuchanganya na eneo la kilomita za mraba takriban 900,000 upande wa bara, eneo lote hilo likawa mali ya Ujerumani.

Kumtafuta Emin Pasha
Mwaka 1889, Carl Peters aliacha nafasi yake ya uenyekiti wa German East Africa na kujerea Afrika Mashariki.Safari hii ilikuwa ni katika kukabiliana na changamoto ya safari ya Henry Stanley (mwanabahari mwingine) ya kumtafuta Emin Pasha, mjerumani mvumbuzi na Gavana wa eneo la sasa la Sudan ambaye ilielezwa kuwa alikuwa amezingirwa ndani ya himaya yake na majeshi ya Mahd.

Carl Peters alitangaza azma yake ya kumshinda Stanley katika kinyang'anyiro cha zawadi ya kumwokoa Emin Pasha. Baada ya kufutika mfukoni kitita cha Maki za Kijerumani 225,000 Carl Peters na watu wake waliondoka Berlin mwezi Februari kuja Afrika Mashariki,

Kugombea Ardhi na Mwingereza
Baadaye ilikuja kubainika kwamba safari ya Carl Peter ilikuwa imelenga katika kupata maeneo makubwa zaidi hasa upande wa kaskazini ikibidi hadi kwenye mto Nile kaskazini mwa Sudan. Huku Stanley akifanya kazi kwa niaba yaMfalme Leopold wa Ubelgiji huko Congo, Carl Peters alikuwa akifanya hivyo hivyo kwa niaba ya Ujerumani.

Lakini mwaka moja baada ya kuondoka na akiwa amefika eneo la Wasoga katikati ya maziwa Victoria na Albert nchini Uganda , alipokea barua ya Stanley ikimwarifu kwamba Emin Pasha alikuwa tayari ameokolewa. Akaelezwa pia kwamba Uganda ilikuwa imenyakuliwa na Uingereza kama sehemu ya himaya yake.

Mkono wa Damu
Kwenye mkataba wa Heligoland wa tarehe 1 Julai 1890 ulioweka mipaka kati ya himaya za Uingereza na Ujerumani katika Afrika Mashariki, Uingereza ilichukua Zanzibar na eneo la kaskazini mwa Zanzibar ikimaanisha Kenya na Uganda wakati Ujerumani ilichukua Tanganyika bara zikiwemo Rwanda na Burundi. Zaidi ya hapo Ujerumani ilitwa eneo la mlima Kilimanjaro na kufanya mpaka wa Tanzania na Kenya uwe kama ulivyo hivi sasa.

Mwaka 1891 Carl Peters alitangazwa kama Kamishina wa eneo linaloitwa German East Afrika, makao yake yakiwa Kilimanjaro.

Hata hivyo, ilipofika mwaka 1895 taarifa zilifika Ujerumani kuhusu ukatili wa kutisha uliokuwa unafanywa na Carl Peters kwa watu weusi kiasi cha kupachikwa jina na "Mkono wa Damu".

Carl Peters alirejeshwa Ujerumani na tume ikaundwa kuchunguza madai hayo, na mwaka uliofuata alihamishiwa London. Mwaka 1897 Carl Peters alitiwa hatiani dhidi ya ukatili wake kwa watu weusi wa Tanganyika. Adhabu aliyopewa ilikuwa kufukuzwa katika utumishi wa serikali.

Akiwa London alianzisha kampuni binafsi iliyoitwa Dr. Carl Peters Exploration Company ambayo ilifadhili safari kadhaa kwenda German East Africa na British Territory karibu na mto Zambezi. Safari hizi ndizo zilizopelekea kuchapishwa kitabu chake cha The Eldorodo of the Ancients.

Baada ya kusamehewa na Mfalme Wilhelm II na kurejeshewa kiinua mgongo chake, mwaka 1890 Carl Peters alirejea Ujerumani wakati kukiwa na vugu vugu la vita ya kwanza ya dunia.

Baada ya kuchapisha vitabu kadhaa, Carl Peters alistaafu na kurejea Bad Harzburg ambako alifariki tarehe 10 Septemba 1919 akiwa na umri wa miaka 63.Baada ya vita kumalizika Carl Peters alitangazwa na mtawala wa wakati huo Adolf Hitler kuwa ni shujaa wa Ujerumani na vitabu vyake vikachapishwa upya.
Hapa Tanganyika hata hivyo," Mkono wa Damu" anakumbukwa zaidi kwa ukatili kwani kote alikopita aliacha nyuma mizoga na mazizi matupu baada ya kuchomo moto vijiji vya watu hata pale pasipo na ulazima kufanya hivyo.

Alilazimisha watu kubeba mizigo mizito katika safari zisizo na mwisho za kutafuta makoloni na unyang'anyi wa nchi za watu. Kwa kuwalaghai machifu kama vile Mangungo wa Msowero huko Morogoro, Karl Peters alifanikiwa kuiweka Tanganyika mikononi mwa wajerumani kama koloni katika mipaka inayojulikana sasa.

Imenukuliwa.
227c6054f98d720ff9039ddc7dbf32fd.jpg
Shukrani Husna
Umeniongezea kitu kichwani
......
 
MFAHAMU JONAS SAVIMBI MTUKUTU WA KUPINDUKIA ALIYEISUMBUA ANGOLA.

Februari 22, 2002 vyombo vingi vya habari duniani kote vilitawaliwa na habari kubwa ya kuuawa kwa mfalme wa pori na mwanaume aliyeisumbua serikali ya Angola kwa zaidi ya miaka 27 akiongoza vita vya msituni dhidi ya vikosi vya serikali.

Jonas Malheiro Savimbi, alikuwa mtoto wa pekee kwa baba yake Lote, aliyekuwa mfanyakazi wa reli ya Benguela na mhubiri wa kanisa la Protestanti lililokuwa likifadhiliwa na Wamarekani.

Pamoja na baba yake kuwa muumini wa dini kamwe Jonas hakuwa muumini, tangu utoto wake alikuwa mtukutu.

Alisoma katika shule za Kiprotestanti na Kikatoliki, lakini akiwa na miaka 24 alipata udhamini wa kwenda kusoma Ureno ambapo alimalizia masomo yake ya sekondari na somo la lazima la siasa huku akishindwa kuanza kwa wakati masomo ya udaktari wa binadamu aliyotakiwa kuyachukua.

Mwaka 1966 alianzisha vuguvugu la Unita kama harakati ya kukomboa Angola kutoka ukoloni wa Ureno.

Katika nyakati zake za awali, kabla ya kuanzisha Unita, alijiunga na chama cha wapigania uhuru wa MPLA mwaka 1964, muda mfupi baadaye alijiunga na chama cha FNLA.

Mwaka huohuo alipata fursa ya kufanya ziara maalumu China na aliahidiwa kupatiwa nafasi zaidi kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi na misaada ya zana za kijeshi.

Hatua hiyo ilitokana na mgongano wa kimasilahi, baada ya FNLA na MPLA kuanza kupingana kuhusu nani anastahili kupewa nchi iwapo watapata uhuru, hivyo muda mfupi baadaye wakoloni hao walitoa taarifa kueleza kwamba Savimbi anapigana kwa ajili ya masilahi yao.

Hatua hiyo ilisababisha kuungwa mkono na Marekani iliyokuwa na masilahi tofauti na MPLA iliyoungwa mkono na Wasovieti tangu mwaka 1974 na kilijipambanua kufuata mrengo wa Marxist-Leninst kuanzia mwaka 1977, wakati Savimbi alijipambanua kufuata sera za Mao na kuungwa mkono na China.

Vita baina ya MPLA na Unita hata hivyo ilikuwa na sababu nyingi za ndani na kwa hiyo kuanza kutumiwa kama chanzo cha mvutano wakati wa vita baridi baina ya Marekani na USSR.


Mwaka 1966 baada ya kurejea kutoka nchini China ambako alienda kupata mafunzo ya kijeshi alirudi na kuunda UNITA na kuanza kupambana na serikali ya kikoloni sambamba na vyama vingine ambavyo vyote vilikuwa vikipigana kumtoa mreno.

Hapa ndipo jina la Jonas Savimbi likaanza kusikika kote duniani kutokana na mbinu kubwa za kijeshi alizonazo huku akisapotiwa na wananchi kutoka kabila lake la Bieno.

Huku akipata sapoti kubwa kutoka China na baadaye Marekani, aliongoza vita vikali kwa muda wa miaka zaidi ya 20 huku akiwa ni tishio kubwa kwa Serikali ya Luanda. Kuna muda aliwahi karibia kuipindua serikali ya Rais Dos Santos.

Akiwa na uwezo wa kuzungumza lugha saba kiufasaha zikiwemo tatu za ndani ya bara la Afrika na nne nje ya bara aliweza kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali kuwaomba msaada wa zana za kivita na alifanikiwa kuwa na jeshi imara.

Aliwahi kunusurika kuuawa mara kadhaa likiwemo jaribio la Februari 1990 ambapo aliponea chupuchupu na kukimbilia nchini Marekani na kufanikiwa kuonana na Rais Bush ambaye alimuahidi kumuongezea zana zaidi za kijeshi na baada ya kupona alirejea nchini Angola kuendeleza mapambano.

Baada ya kunusurika kuuawa zaidi ya mara 20 na vikosi vya serikali ya Angola huku taarifa za kuuawa kwake zikiripotiwa zaidi ya mara 15 hatimaye 22 Februari 2002 Jonas Savimbi aliuawa.

Maauaji yake yalitokea kwenye mapigano baina ya vikosi vyake dhidi ya serikali kwenye mto uliopo jimbo la Moxico eneo ambalo alizaliwa. Mapigano hayo ya kushtukiza yalipangwa baada ya vibaraka kutoa siri za mahali alipo Savimbi na baadhi ya wasaidizi wake muhimu, haikuwa kazi rahisi kumuua.

Aligundulika alipo kuwa amejificha baada ya kufanya kosa la kutumia satellite phone na huo ndio ukawa mwisho wake. Osama alikuwa hafanyi kosa kama hilo,ndio maana ilikuwa vigumu kubaini alikuokuwa amejichimbia.

Kwenye shambulio hilo kali kuwahi kufanywa na vikosi vya serikali dhidi ya kikosi cha Savimbi walifanikiwa kumpiga risasi 15 mwilini mwake, alipigwa kichwani, kifuani na sehemu za miguuni na aliweza kumudu na kuendeleza mapambano kwa zaidi ya saa nne kabla ya kuishiwa damu na kuanguka chini na kufariki.

Tukio la kuuawa kwake bado limeacha maswali mengi mpaka leo inakuwaje na aliwezaje kuhimili kuendeleza mapambano hata baada ya kupigwa risasi 15 mwilini mwake?

Alizikwa kwenye makaburi ya nyumbani kwao ya Luena na kuhudhuriwa na wapiganaji mbalimbali wa UNITA.

Mauaji yake yalimaanisha mwisho wa mapigano ya msituni nchini Angola, Chuma kilikuwa kimeangushwa, wasaidizi wake hawakuwa na mbinu na uwezo kama Savimbi.

Baada ya kifo chake serikali kuu ilitangaza ya kwamba hatimaye wameangusha mbuyu wa chuma uliowasumbua miaka mingi.

Wapo wanaoamini mpaka kesho kwamba Jonas Savimbi hakuwa binadamu wa kawaida, walimuona ni binadamu wa pekee mwenye uwezo mkubwa kuliko binadamu wa kawaida.

Wenye imani potofu walimfananisha na jini au mzimu unaotembea popote na wakati wowote bila kujali hatari iliyo mbele yake.

Hadi mauti yake yanamkuta ameacha watoto na wake wengi ambao idadi yake haijawekwa wazi kulingana na sehemu kubwa ya maisha yake alikuwa akiishi msituni.

Ndivyo ilivyokuwa kwa Jonas Savimbi ambaye kitendo chake cha kugomea kurudiwa kwa uchaguzi wa rais wa nchi hiyo na kuamua kuingia msituni kulipelekea kuuawa kwake.

Savimbi alifanya kosa moja kubwa alilazimisha vikosi vyake kuingia msituni kupambana na serikali akiwa bado hajajipanga vyema, ni bora angekubali kurudia uchaguzi dhidi ya Rais Dos Santos.

Bahati mbaya hakulikumbuka hilo, aliwaza jambo moja tu kuingia msituni kuandaa kikosi chake tayari kuuondoa utawala wa Dos Santos.

Aliingia msituni kipindi ambacho tayari kikosi chake kilikuwa kimeingiliwa na vibaraka ‘spy’ kutoka ndani ya kabila lake, vibaraka hawa waliandaliwa kwa ustadi mkubwa na ndiyo walihusika kutoa siri zote za nini kilikuwa kinaendelea kwenye kikosi cha Savimbi.

Fahari news.
fc3c95cb8f2444f90f57633816251a8f.jpg
Ni naona kuingia msituni sawa tu ni vigumu kwa wapinzani barani Afrika kushinda uchaguzi
Hata baada ya kifo cha Savimbi rais Dos Santos aliendelea tu kutawala

Pia wamarekani kama kawaida yao kila penye vurugu kuna mkono wao
.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom