Makapuku Forum

Makapuku Forum

Sehemu ya 30


Jina lake liliandikwa kwenye kitambulisho kilichokuwa kinaning'inia shingoni mwake. DK ASHA ndivyo jina lilivyosomeka kitambulishoni. Kazi ile kwake ilikuwa ndogo sana ingawa mguu wa Shebby ulifumka vibaya eneo la goti.
"Pole sana kaka ila usiogope utakuwa sawa tu na utatembea kama zamani." Alimfariji kwa sauti ya haiba ya kike wakati akiandaa vitu vyake sawa tayari kuanza kumshughulikia Shebby. Moja kwa moja aliupachika mguu wa shebby kwenye mashine maalum mara baada ya kumchoma sindano nne za paja zilizoua mawasiliano yote ambayo yangeweza kumletea maumivu Shebby. Aliifanya kazi yake kwa uhuru na umakini bila Shebby kuhisi chochote. Mwanadada alianza kucheza na nyama za Shebby huku akipekechua mifupa kwa umakini upasuaji ukachukua nafasi.

*******
Taarifa za tukio la Mkuyuni zilisambaa kama umeme kila pande ya nchi. Kwa siku mbili tu mpaka nchi jirani habari zilifika. Mapaparazi na waandishi wa habari za kina walithibitisha juu ya vifo vya utata vya maaskari zaidi ya kumi na tatu huku majiruhi majeruhi mmoja akiwa Kamishna Shaabani aliyejeruhiwa vibaya eneo la mguu.
Kila mtu alisikitishwa na kushangazwa na habari zile. Wana habari walimganda Kamanda mkuu wa jeshi la polisi ambaye hakuwa na wakati wa kuzungumza nao kuthibitisha chanzo rasmi cha tukio lile. Maswali yalipomuandama aliwajibu kwa kifupi kuwa "Uchunguzi bado unaendelea."
Hata muheshimiwa Rais ambaye ndio kwanza ulikuwa mwaka wake wa sita na wa kwanza baada ya uchaguzi wa pili ikuluni, alistushwa na kushangazwa pia. Alimuagiza haraka waziri wa mambo ya ndani na yule wa ulinzi, kuunda kamati rasmi ya kuchunguzi sababu za tukio lile na waliowashambulia polisi. Kamati ilipoundwa ilianza kazi kwa kumuhoji kamishna Shebby mwenyewe baada ya kufanyiwa upasuaji na kuunga upya mifupa. Lakini cha ajabu baada ya Shebby kufanyiwa upasuaji hakuwa tayari kutoa maelezo yoyote.

* * * * * *

Zilipita siku tano baada ya tukio lililobaki kuwa hadithi isiyokuja kusahaulika kwa baadhi ya familia waliopoteza wapendwa wao hususani kituo cha Mkuyuni. Siku hiyo ndio ilikuwa siku maalum ya kuwaaga wale waliofariki kabla ya kwenda kuwazika sehemu tofauti zilizopendekezwa na wanafamilia wa kila marehemu.
Viongozi mbalimbali walihudhuria tukio lile lililofanyika katika viwanja vya leaders wakiongozwa na Mh Rais mwenyewe akiwa sambamba na viongozi wakuu wa usalama bila kumsahau mkuu wa jeshi la wananchi ambaye alitoa hotuba fupi iliyowafurahisha wananchi wengi walioguswa na tukio lile hasa pale alipoahidi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuutafuta ukweli wa mambo kama lile tukio lilihusiana na ugaidi ama laa!
Mbali na hotuba fupi ya mkuu wa majeshi na ile ya Kamanda mkuu wa jeshi la polisi lakini kitu chengine kilichowaliza wananchi ni ule wasifu uliokuwa unasomwa wa wale askari hususani urafiki wa Kimaro na Kamishna Shebby ambaye ndiye pekee alinusurika huku akimpoteza swahiba wake mkubwa aliyejua siri zake nyingi Sajent Kimaro. Watu wengi walitamani sana kumuona Kamishna Shebby na kusikia chochote toka kwake. Ingawa alikuwepo pia akiwa kwenye kiti maalum cha walemavu akiwa upande ule wa watu maalum huku kulia na kushoto walikaa wazazi wake, na nyuma yake alikaa yule daktari wa kike ambaye mzee Mwinchande aliamua kutumia pesa nyingi zaidi za kumlipa ili tu mwanae ahudumiwe naye mpaka atapopona. Hii iliwaaminisha wengi hadi mh Rais kuwa jinsi gani yule mzee alivyokuwa na uchungu na mapenzi mazito kwa mwanae licha ya serekali kutoa kiasi kikubwa cha pesa na kuahidi kuwa kama ikishindikana wampeleke nje ya nchi lakini bado mzee Mwinchande hakuwa nyuma kuhakikisha mwanae anakuwa sawa na kurudi katika hali yake.
Ulifika muda wa Kamishna Shebby kusogea jukwaani na kusema chochote mbele ya umati kabla shughuli ya kuaga kuanza rasmi. Taratibu yule dada daktari alianza kumsogeza kwa kiti kile maalum cha magurudumu huku waandishi wa habari wakihakikisha wanachukua vizuri lile tukio kwa kamera zao. Watu walinyamaza kwa shauku ya kumsikia atasema nini askari yule pekee aliyenusurika. Kwa utulivu baada ya kufikishwa mbele ya vipaza sauti Shebby alitoa miwani meusi iliyokuwa imeziba uso wake na wananchi wote waliyashuhudia macho yake vyema. Wekundu na uvimbe wa macho uliosababishwa na kilio cha muda mrefu ulijidhihirisha usoni mwake. Lakini alipoitoa sauti kuzungumza aliushangaza umati na kumstua hata Rais kwa kile alichokitamka. Kila mja alimtumbulia macho na kushangazwa na maneno yake.
Aliwatazama watu waliokuwa wamehamaki na ndipo aliporudia tena maneno yake kwa msisitizo kuwathibitishia kuwa kile asemacho ndicho alichomaanisha.
"Ni kweli kabisa ndugu zangu....SIJUI KITU." Aliweka kituo baada ya kauli yake kwa msisitizo kamishna Shebby na kuendelea kulia huku akitazama msururu wa masanduku yenye maiti yaliyowekwa eneo lile maalum la kuagia. Alijikaza kiume na kuendelea kuzungumza.
"Wazazi wangu na marafiki leo wamejaribu kunisimulia na kuniuliza nipate kukumbuka kilichotokea lakini bado najihisi huenda si mimi niliyekuwepo huko kwani sikumbuki nini kilitupata jamani sina cha kuongea zaidi ni kweli kabisa Sijui Kituu." Alifafanua na kusisitiza kwa mara ya tatu ambapo kauli yake haikuwa rahisi kuaminika hata kidogo.
"Huyu itakuwa kachanganyikiwa si bure.. eti haelewi kitu? yeye si ndie alikuwa kiongozi huko!!" alihoji mmoja wa raia aliyehudhuria tukio lile. Baada ya hapo ndipo yule daktari alimuondoa kamishana eneo lile taratibu. Zoezi la kuwaaga marehemu lilipoanza kamishna Shebby alifungua kuwa mtu wa kwanza kuaga. Alipewa nafasi ile kuanza kuwaaga wenzake na kila alipofikishwa kwenye sanduku na kuitazama picha kubwa ya marehemu iliyowekwa juu ya sanduku kutokana na miili kutofunuliwa kwa sababu maalum, aliumia sana. Alipoifikia kwenye jeneza lililokuwa mwili wa Sajent Kimaro aliishiwa nguvu zaidi alipoitazama picha ya Kimaro alizidi kuchanganyikiwa na kulia kama mtoto.
"KHAA!! Kimaro rafiki yangu mpaka wewe? ooh... Mbona sielewi jamaniii aaaagh!!!!" Aligugumia kwa sauti na kuzidi kuwachanganya watu huku wengine wakithubutu kusema kuwa anafanya kusudi.
"bwana hata kama sijasoma lakini siwezi kuwa mjinga kiasi hiki, hivi toka lini mtu aliyepoteza kumbukumbu kweli kabisa na kusahau tukio lote sasa anawakumbuka vipi watu aliokuwa nao? hahahaaa huyu Kamishna si bure kuna kitu tu anaficha na huenda yeye akawa ndie aliyesababisha wenzake kufa.. we fikiria wooote wafe abaki yeye tu!!.. kama nani? Malaika au......" Ilikuwa ni sauti ya dada mmoja mrefu akiwa sambamba na rafiki zake wamesimama miongoni mwa waliohudhuria tukio lile.
Shughuli za uagaji zilimalizika baada ya masaa matatu. Misafara ya viongozi ilianza kuondoka eneo la viwanja huku gumzo kubwa kwa wananchi na waandishi wa habari likiwa ni kuhusu Kamishna Shebby kusahau kilichowakuta hali ya kuwa yeye pekee alisalimika na ndie aliyepaswa kutoa maelezo yakinifu mbele ya umma.
......
 
UF. ...
d34a792dca0e431006287c03a8ba3606.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom