Lee
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 44,001
- 150,526
Sehemu ya 28. ..
.....ha ha ha ha a a a Tatizo wanawake hamfikirii kabla ya kutenda. Ila nami nakwambia hii uliyoipata leo ni bahati kubwa sana ni bora tu uitumie vizuri. Nakuahidi ukiniacha hai lazima nije kukutafuta na utalipa damu zote zilizovuja leo wewe na Mr X. Naapa sitokuja kukuacha hai kama leo utaniacha hai na umwambie mr. X asijidanganye mwisho wake UPO na atakufa kifo kibaya na cha mateso!" Alinena kishujaa Kamishna Shebby japo kwa taabu. Lakini maneno yake ndio kwanza yaliongeza kicheko kwa yule ninja wa kike. Hapo ndipo alipomshuhudia akiitupa chini ile bunduki ya udunguaji na kuchomoa bastola ndefu na kuiload kisha kumuelekezea pale chini usawa wa paji la uso. Kamishna Shebby alisali sala zake za mwisho nafsini na kufumba macho kusubiria risasi itavyofigisa nyama zake na kuutoa uhai wake bila kupata jibu ya kile alichojitoa kukitafuta.
Akiwa kafumba macho pale chini Kamishna Shebby huku akiamini kuwa ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake mara alisikia kitu kikipenya kwenye paji lake la uso mithili ya mwiba wa nyuki na kumsababishia maumivu makali sana. Aligundua haikuwa risasi hata akafumbua macho lakini alijikuta akiona maluweluwe. Nuru ilizidi kupotea machoni mwake midomo ikazidi uzito taratibu mawasiliano fahamuni yalikata na kuzirai.
*****
|GEREZANI|
Baada ya kuona usiku umeingia na hakuna majibu yoyote. Mzee Mwinchande alipendekeza apigiwe simu mtu wa karibu aliyetoka na Shebby. Kwa msaada wa mkuu wa gereza msaidizi walipiga namba ya Sajent Kimaro ambayo nayo iliita tu bila kupokelewa. Wakajikota wote wakiingiwa hofu.
"Mi nahisi kijana kutakuwa na tatizo tu si bure kwani hata jinsi simu ya Kamishna wako ilivyokatika sijaelewa!"
"Mh! sina imani sana mzee wangu.. Eti we bubu ni sehemu gani waliyoenda kamishna na Kimaro?" Alimgeukia Hussein yule msaidizi na kumpachika swali.
"Mkuyuni.. Mkuyuni Morogoro" Alijibu Hussein na pale pale kamishna msaidizi alipopekua kwenye kompyuta ya ofisi na kuingia kurasa maalum ya polisi na kutafuta namba ya simu ya mkuu wa kituo Mkuyuni Morogoro.
"Ngoja kidogo mzee wangu hapa nimelipata jina na namba za ocs wa Kituo Mkuyuni huyu bwana John kwanza tuongee naye tuone anaweza kutusaidia vipi ili tuweze kuwapata." Aliongea mkuu msaidizi wa gereza huku akiandika namba za simu za ocs John na kuzipiga. Lakini cha kushangaza nayo iliita zaidi ya mara tisa pasipo kupokewa. Hii iliwazidisha shaka na ndipo walipoamua kupiga namba rasmi za kituoni na kuziacha zile za mikononi. Namba hii haikuchelewa ilipoita tu ikapokewa.
[''Hallow hapa ni kituo kikuu cha polisi Mkuyuni sijui nani mwenzetu kutoka wapi na tukusaidie nini tafadhali...?'] Ilisikika sauti ya kike upande wa pili. Ndipo msaidizi mkuu wa magereza alipojitambulisha na kutoa hitaji lake hata kupiga simu pale.
[''Sasa samahani mkuu ametoka kidogo kuna wageni walikuja hapa wameelekea mabondeni kwa kazi maalum'']
"Ni ugeni gani huo tafadhali naomba nijuze."
["aaagh! ni ugeni wa ghafla wa Kamishna Shaaban kutoka huko.'']
"Okey, unaweza kutuma ujumbe wangu sasa hivi kwa mkuu wako?maana ni muhimu saana tena sana kuzungumza naye muda huu."
[''sawa nipatie dakika tano''] Ilijibu sauti upande wa pili na simu kukatika. Walishusha pumzi baada ya kupata uhakika kina Shebby wapo huko na wametoka na Ocs wa pale.
* * * * * *
- MKUYUNI -
...........................
Baada ya kukata simu inspekta wa kike aliyebaki kiongozi kwa muda huo akichukua nafasi ya mkuu wa kituo. Alitoka nje ya kituo kwa mshangao uliozaliwa na kelele za raia wengi waliokuwa wakielekea upande ule.
"Afande.. Afandee tumesikia risasi kule mabondeniiii....uuhhhapphhhh wanakufa watu kule na mapolisi wenzenuu Uuuuuphhuuiiiiii" Aliongea bwana mmoja huku akiwa anahema sana na kumtia hofu mwana mama yule Inspecta. Kituo kizima kilibaki na askari wawili pekee na gari moja ukiachilia askali wanne na gari lengine ambalo lilipeleka maiti ya yule aliyenyongwa hospitali ya Morogoro mjini.
"We unasemaje ati?"
"Ndio hivyoo mamaaa kuna Kibwengoo huko mabondeni anaua watuu" Aliongea raia mwengine. Wananchi waliendelea kukimbilia maeneo yale ya kituo ambayo walihisi ni salama kwa maisha yao. Walihofu kiumbe anayeuwa watu ambondeni anaweza kuhamia sehemu za juu na kuwadhuru nao. Akiwa haelewi nini afanye kama kiongozi kwa bahati nzuri muda uleule mwakanga mkali wa taa za gari iliyokuja inakuja kasi ilimulika na kusimama karibu naye. Ilikuwa ni difenda yao ile iliyopeleka maiti.
"Vipi, nasikia wakuu wamepatwa na matatizo huko?" Aliuliza inspecta mwengine yule wa kiume akiwa ndani ya gari ambaye alikuwa kaimu wa ocs John kabla ya yule mama.
"Sielewi kwa kweli hata simu hazipokelewi na niliposikia kelele na kutoka nje ndo nimezipata tetesi sasa hivi na baadhi ya watu waliokuwa wanakimbia."
"Mama we endelea kubaki na kudumisha usalama hapa sisi tunaelekea huko huko" Aliongea yule inspekta wa kiume na kumuamuru dereva wake aondoe gari haraka kuwahi mkuyuni stendi kuu ili waelekee huko mabondeni kwenye matatizo.
Muda mfupi baadaye timu ile ya askari waliotoka hospitali iliwasili eneo la nyumba ya mzee Mnyungunyungu. Ukimya ulitawala sana mara baada ya wananchi kukimbia kipindi waliposikia risasi zikirindima maeneo ya jirani na pale.
Wakiwa wamejifunga tochi maalum kichwani kwa niaba ya kuwasaidia kuona kutokana na giza nene lilikuwa limefunga nyakati zile eneo la msitu, askari wale wachache walisonga mbele kwa maelekezo ya inspekta wao. Kwa uangalifu mkubwa sana walipiga hatua mara baada ya kukutana na maiti ya kwanza ya askari mwenzao kabla ya pili ambayo ilikuwa ya yule babu. Walizidi kuhamaki na kupigwa bumbuwazi walipoikuta maiti ya mkubwa wao ambaye ni Ocs John akiwa amefumuliwa vibaya kifuani. Nafsi ziliwaingia hofu askari wale lakini walijikaza kisabuni na kuzidi kusonga kwa tahadhari bunduki zao zikiwa tayari mikononi kukabiliana na lolote. Hali kama ile hawajawahi kushuhudia wala kuifikiria kama watakutana nayo katika kazi ya upolisi. Wakiwa wananyata mara baada ya kuupita mwili wa ocs John mara walijikuta wote wakistuka sana na askari mwengine akajikuta anafatua risasi bila kutaraji na kurukia pembeni kwa hofu. Kilichowastua vile hakikuwa chengine bali ni muito wa simu wa ghafla uliosikika kutoka katika sare za Ocs John na kumfanya inspekta wao aangue kicheko pasipo kutaraji hali ya kuwa naye aliruka na kujibaza pembeni kwa hofu. Akaisogelea maiti ya ocs wake baada ya kugundua kilichowatisha ilikuwa simu, ndipo taratibu aliitoa kwenye mavazi ya Ocs John.
"Angalia kiongozi isije kuwa bomu hilo tumeekewa mtego na kitendo cha kuipokea kwako kisije kutupukutisha na sis..!!?" Alitoa hadhari askari mmoja huku akirudi mbali zaidi na eneo alipokuwa inspector kwa hofu. Maneno yake kidogo hata inspekta yalimtisha na kutafakari moyoni lakini ilim'bidi aoneshe moyo wa kishujaa ili asiwatishe zaidi. Aliichomoa bila kujali na kuitazama namba ya anayepiga. Ilikuwa ni namba ngeni simuni haijaseviwa. Alishusha pumzi na kuomba Mungu kimoyomoyo iwe heri pindi anapoipokea ile simu na papo hapo alibana pumzi na kuipokea.
******
Baada ya kusubiria jibu kwa zaidi ya saa moja bila mafanikio mzee Mwinchande alimuamuru tena yule mkuu msaidizi wa gereza kupiga tena namba za mkuu wa kituo Mkuyuni. Bila hiyana yule mkuu msaidizi wa gereza ilibidi adondoke tena hewani.
Safari hii simu iliita mara ya kwanza ikakatika bila kupokewa lakini alipojaribu mara ya pili akiwa hana matumaini kama simu itapokelewa mara alisikia sauti ya mtu ikiuliza upande wa pili na kubaini kuwa safari hii simu imepokelewa.
"Hallow! Halllow naomba nipate habari juu ya kamishna wetu aliyesafiri kwa kazi maalum huko kwenye kanda yako vipi kuna taarifa gani?" Huku akiwa kaweka sauti kubwa mkuu msaidizi wa gereza alisema.
["Ndio afande. Ukweli sasa habari huku si nzuri kuna tatizo limewapata askari wote waliokuwepo kwenye tukio la mtu aliyejiua kwa mazingira ya kutatanisha. Na upelelezi wa kina juu ya chanzo chenyewe umegeuka na sasa wote kuna majibizano ya risasi huko mabindeni. Tafadhali tunaomba mtuongezee nguvu kwa kuwa sasa hali ni mbaya sana hapa Mkuyuni amani imesimama kabisa raia wanakimbizana ovyo na wauaji bado hatujawapata"]
Sauti ya upande wa pili ilimfanya mzee Mwinchande apagawe na kufoka kwa sauti huku Hussein bubu ambaye alikuwa bado hajarudishwa kwenye chumba cha jela aliyofungwa akidondokwa machozi.
"Haiwezekaniiiiii Mwanangu afe hivi hiviih.. hebu muulize kama wamemuona na mwananguuu! Aaang!.." alifoka mzee Mwinchande. Afande yule msaidizi wa gereza alipomuuliza upande wa pili insoekta aliyepokea simu alijibiwa kuwa imeonekana maiti nyengine ya yule aliyekwenda na Kamishan Shebby ambaye ni Sajent Kimaro. Hapo ndipo mkuu wa gereza msaidizi chozi lilipomdondoka na kuamini sasa kama Kimaro hayupo duniani basi hata Shebby anaweza kuwa marehemu. Mawasiliano yalifanywa haraka na kujulishwa askari wa Morogoro mjini juu ya tukio lililokuwa linatokea Mkuyuni muda mfupi ili wakatoe msaada.
"Haaah! Haiwezekani hata kidogo!!" Aliongea kwa sauti ya juu mzee Mwinchande akionesha kuchukizwa zaidi. Pale pale haraka alitoa simu yake na kutafuta jina moja na kuipiga namba hiyo. Ilikuwa ni namba ya kamanda mkuu wa polisi kanda ya mkoa Morogoro.
"Halloow! Yaaani ndugu yangu mwanangu mnaacha afe hapo Mkuyuni bila kumpatia msaada wowote? aahg!! siamini mdogo wangu"
["Vipi kaka, mbona sielewi?"] Alijibu kwa taharuki kamanda wa Morogoro baada ya kugundua anazungumza na mzee Mwinchande.
"Wewe kama Kamanda wa mkoa nitakuelewaje unafikiri? Tuma vijana wakutosha haraka mkamsaidie mwanangu kama bado yuko hai lakini nataka nikwambie askari wako wengine wa Mkuyuni pamoja na Ocs wao wameuawa usiku huu."
[Khaaa! Unasema?!!!] Kamanda mkuu wa Moro alitaharuki na palepale simu ilikatika. Alichanganywa na maneno ya mzee Mwinchande haraka akawaamuru vijana wake waelekee Mkuyuni kujua kulikoni. Wakati huo mzee Mwinchande baada ya kumkatia simu kamanda wa Morogoro haraka alimpigia simu waziri wa mambo ya ndani na kumlalamikia juu ya tukio la mwanawe habari iliyomshangaza waziri na kusikitishwa mno kabla hajamuahidi kuwa atatuma kikosi maalum usiku ule kwa helkopta ya kijeshi kwenda kumtafuta mwanaye ambaye wadhifa wake ulitolewa mbele ya mheshimiwa rais.
Kwa upande wa Hussein bubu yeye kilio chake kilikuwa cha peke yake. Hata pale aliporudishwa kule kwa wafungwa wenzake muda wote alikuwa analia kama mtoto huku akiilaumu nafsi yake kwa kukubali kumuhadithia kitu alichokaa nacho zaidi ya miaka 25 bila kumwambia mtu lakini leo hii anajikuta anamponza na kumsababishia matatizo makubwa kijana wa watu ambaye hakuwa na hatia hata kidogo na hadi dakika hiyo hakuwa na hakika kama yu hai au nae amekufa kama wenzake.
"Eee Mungu baba Muumba mbingu na nchi, najua wewe ndiye muweza na mpangaji wa kila kitu... Nakuomba umuepushe mja wako asiye na hatia katika balaa lililo mbele yake muda huu na yote hiyo ni kutokana na huruma yake ya msaada. Basi nami nakuomba baba msaidieee Mponye na umueke mbali na Kifo mpaka atapofikia umri wa utu uzima sana na hata kama atakufa basi asife kwa sababu ya kesi hii tena. Nakuomba baba nitendee muujiza ili niweze kulipa kisasi kwa Mr. X mimi mwenyewe pasi na kuhusika mtu mwengine yeyote. Nakuomba Mungu uniwezeshe niweze kumuua Mr X kwa mikono yangu japo kuua ni dhambi."
Yalikuwa ni maombi aliyokuwa anaomba Hussein ndani ya moyo wake huku machozi yakim'bubujika muda wote. Hakupata nafasi yakuuliza chochote zaidi baada ya kurudishwa selo ingawa alijua kuwa Mkuyuni kumechafuka na kina Shebby hawako sehemu salama kwa muda huo. Alibaki kasimama akiwa kashika nondo za mlango wa chumba alichokuwa analala huku akiangalia korido ile ndefu iliyokuwa kimya kwa nyakati zile za usiku. Alivuta taswira na kukumbuka kamishna Shebby kuwa mtu pekee wa kwanza kumuonesha thamani kubwa ndani ya jela. Aliamini hakuna na hatotokea mpaka mtu kama yeye mapaka siku atayoingia kaburini. Sheby alikuwa kijana wa ajabu sana kwake. Alijiuliza vipi leo hii afe kabla yake!? Aliumia sana Hussein na kumlilia Kamishna Shaaban kama mtoto wake wa kumzaa.
Hadi kunakucha Hussein alibaki kasimama palepale mlangoni. Alishindwa kabisa kulala na kusogea popote zaidi ya kububujikwa machozi yaliyobeba kumbukumbu nyingi za huzuni na hasira kuhusu MR.X Usiku huo aliomba mambo mengi sana huku jambo kubwa alitamani sana Mungu amfanyie muujiza ili amuue Mr. X kwa mkono wake mwenyewe. Aliamini kama atafanikiwa hilo basi hata kifo chake atakifurahia kuliko kufa akamuacha mr. X duniani akizidi kuwamaliza watu wasio na hatia wataotaka kuufichua ukweli ambao aliamini chanzo cha yote ni mkewe yule aliyekuwa binti mrembo kutoka Arusha.