
ZABURI 34
3.Mtukuzeni BWANA pamoja nami,na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4.Nalimtafuta BWANA akanijibu,Akaniponya na hofu zangu zote.

Kumtafuta MUNGU kuna malipo...na kila umtafutapo utamuona..utamuona MUNGU kila wakati,maana hata kuamka kwako ni MUNGU si kwa ujanja wala akili zako ni MUNGU ndiye amekupa pumzi hii na hata umeweza kuuona tena muandiko huu,bila yeye HUWEZI
Basi ndugu yangu,rafiki yangu,mpendwa wangu,KAPUKU mwenzangu jiunge nami,ungana nami asubuhi ya leo TUMTUKUZE,TUMSIFU,TUMSHUKURU ,TUADHIMISHE JINA LAKE ..maana ametupa tena NEEMA hii ya Kuiona siku ya leo BURE...ndiyo ..ni ..BURE..JE ? Mwenzangu umelipia chochote?
Pamoja na kutuamsha salama ahadi yake MUNGU kwetu ni kuwa TUKIMTAFUTA .Atatujibu,Atatuponya na HOFU zetu zote..UNA HOFU Gani?
HAKUNA HOFU ISIYOJIBIWA NA MUNGU...MKABIDHI MAISHA YAKO ...
TUOMBE
ASANTE BABA kutuamsha salama,tutakase,tuongoze tufundishe kukutegemea ,tuponye tuhuishe,tubariki..ondoa HOFU zote Mfalme wa Amani ,wewe ni MUNGU USIYESHINDWA,HUJAWAHI KUSHINDWA,HUTASHINDWA..WEWE NI MWANZO WEWE NI MWISHO...Maana umetutoa mbali from ZERO TO HEROES...ASANTE BABA MAANA utatenda kila kitu sawa na mapenzi yako .
Tunaomba tuepushe na hatari za mwili na roho,tuepushe na mitego ya shetani kiburi cha uzima kisituangushe na kutukosesha mbingu,wivu,masengenyo,hasira,uchungu,kukata tamaa havina nafasi kwetu maana sisi ni wathamani ulituumba kwa mfano wako kwa ajili yako si kwa ajili yetu hivyo BABA tunapaswa kukutukuza.
Ponya wagonjwa mahali hapa,fariji wafiwa,wapweke,yatima ,wajane na waliovunjika moyo..ponya majeraha yote BABA katika wewe tuwe washindi

.Roho Mtakatifu tuongoze katika yote.
Tunaomba yote katika jina la Yesu Amen
NAWATAKIA SIKU NJEMA

MBARIKIWE