Makapuku Forum

Makapuku Forum

4c91df659b9e4937e8a3d91884ef29da.jpg



Unaenda wapi rudi kajieleze kwa mkweo
 
Muziki: Wingu Limetanda

Hivi ni mara ngapi kapuku mwenzangu ulishamwambia asante yeyote anayeifanya siku yako kukamilika kwa uzuri kabisa? Najua unatafakari hili maana nami nilikaa na kulikumbuka sana jambo la kushukuru. Unaweza kushukuru kwa namna tofauti, kwa hali na mali, kwa tabasamu na kupeana tano. Vyovyote vile, kutoa shukrani ni jambo la kiungwana na kwa sababu hiyo kwanza kabisa nakusalimia na kisha nashukuru kuwepo hapa. Unapafanya KF pawe sehemu bora kabisa.

Kushukuru, ndo ninachoongelea leo kwa ufupi, jiangalie nywele zako zilivyopendeza, msusi kafanya kazi yake, angalia mikato ya nywele, kinyozi kafanya kazi, angalia kiatu kilivyong'aa, shushaina kachukua muda wake kukiwakisha. Umeenda kula hotel, meza imesafishwa chakula kimekuja kwa wakati na maji umeletewa. Umepanda daladala, bodaboda au express umefika unapoenda. Unakumbuka kuwashukuru hawa watu.

Upande wangu sasa, hata kama huwa siwashukuru kivile lakini nakuambia ukweli kabisa, nikiendaga bakulutu na bendi ipo basi mpiga gitaa, mpiga ngoma, mwimbaji basi watacheka na buku buku au jero au wakipumzika watagonga moja moja watengeneze sauti.

Nimeongelea Bakulutu, machozi yamenijaa usoni hata lee empire mjomba wangu anajua kabisa kuwa Shaaban Dede ambaye ni jirani yake katutoka, ni msiba wa Kitaifa nyimbo zake zinajulikana na wengi. apumzike kwa Amani Shaaban Dede.

Angalia clip hii ni mahojiano yake na star TV enzi hizo mkorogo kwa watangazaji unafanya kazi yake sawasawa




Kumbuka kutip hata kama unalipia huduma ya watu niliowataja pale juu. Naamini unajua kabisa wanacholipwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom