Makapuku Forum

4/JK Rowling Amezaliwa July 31 1965
Umewahi kuangalia mfululizo wa muvi za Harry Porter ? Ni mfululizo wa muvi kama za kichawichawi....siyo uchawi wa yule Mtu mwepesi tapeli wa JF
Wakati wewe unaburudika basi elewa kuna mwanamke pale amekinga ndoo inajaa hela utafikiri anakinga majibombani
Ana utajiri unaokadiriwa kufikia USD 1 billion
.......
 
khaa kumbe mpaka Kelly duuh kweli mziki nimeujua siku hizi
 
3/Madonna Alizaliwa Agosti 16 1958
Huyu ni bibi mpenda starehe na kutembea na viMario....alikuwa na vituko kumzidi Lady Gaga
Enzi zake alitamba vilivyo na vibao vyake matata kama vile Like A Virgin na kuiteka dunia
Pia anazo ngoma kali nyingine kama vile Like A Prayer na Vogue
Kupitia muziki ameingiza mpunga mrefu pia amejihusisha na filamukibao zikiwemp za utupu ..yeye kwake ni pesa tu
Ana utajiri unaofikia USD 800 Milioni
.......
 
2Dr Precious Moloi Motsepe Sijajua mwaka aliozakiwa.....Waafrika kwa kuficha umri hatujambo
Ni Msauzi ambaye couple yake na mumewe ni maarufu
Anamiliki ma kampuni kadhaa....ni mfanyabiashara na pia anajihusisha na masuala ya mitindo
Anao/wanao utajiri unaofikia USD 2.5 Bilion
........
 
1/Oprah Winfrey Alizaliwa Januari 29 1954
Utotoni akitokea familia ya kimaskini Hivyo kupitia changamoto kibao
Akiwa na umri mdogo alibakwa na nduguye ...haikuidhia hapo
Akiwa na umri mdogo tu akapewa ujauzito ila akapoteza kichanga chake baada ya kujifungua(mtoto walifariki) ila akaendelea na ndoto zake......Huku Bongo Sizonje hawataki mabinti waliopataujauzito waridi shule(mi nampinga)
Hajabahatika tena kupata mtoto
Mweneshaji huyu wa zamani wa vipindi vya luninga ana vidole 6 mguu wa kushoto ....pamoja na kuwa na utajiri mkubwa lakini amejikubali na kuviacha kama vilivyo licha ya utotoni kuchekwa
Halle Berry naye mguu mmoja ana vidole 6.,..
Ana utajiri unaofikia USD 3 Bilioni
.
.
.
.
.
Shukrani kwa mliosapoti mada
Tukutane Jumatatu
Mwisho
...........
 
Muziki: Wikend Tulivu


Ilikuwa ni wiki yenye mambo mengi, hatimaye leo ni Ijumaa na japo nayo inaelekea kuisha lakini sichoki kuamini kuwa umekuwa na siku njema kabisa. siku ya mwanzo wa mapumziko kwa wengi wetu lakini usisahau ndo wiki ya kurejesha nguvu iliyotumika katika siku tano 'za kazi'. Ni siku ya homework na bed-work kwa wale wenye majukumu na hatuwachi mbali wale wazee wa selfie yaani oneself. Hongera sana.

Unajua hupaswi kuifanya Ijumaa kuwa ngumu, ni siku ya kutafakari, kujipanga na kupanguliwa. leo hata sijui niandike nini maana siku imekuwa rahisi kuliko urais wenyewe. Ni mwendo wa sharubati na monde kwa kwenda mbele yaani si mchezo. Si unajua kuna makande, yeah, mchakanyiko wa nafaka zinazopikwa pamoja. Mmmh, na wapo wanaochanganya vinywaji sasa, makande ya vinywaji, azam juice, mo soda, safari lager, savana na konyagi ili mradi tu kulifanya tumbo litambue kuwa nalo ni sehemu ya mwili.

Muziki sasa, kapuku mwenzangu leo tunahama kidogo kwenye ile myuzikiz zetu na tunaenda kwenye muziki wa taratibu, yeah haina kubamba wala kubambia. Unakaa chini na unatikisa mguu taratibu, ukiona umeguswa sana basi unaamka kwa adabu na kwenda kumtuza mwimbaji. Ndivyo alivyokuwa anafanya hata mzee wetu kipenzi Ali H. Mwinyi. Sasa leo kaa chini uburudike na wimbo huu hapa mtamu kabisa.

 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…