Makapuku Forum

Makapuku Forum

alikuzidi ketei itakuwa


...yaani kuna mambo nitaweza kumtetea anko wangu lakini kuna mambo siwezi kumuwekea dhamana kabisa. Huwa nikikumbuka nasema japo nilikuwa bado yosso asingetumia udhaifu wangu wa kutojua kiingilishi kwenda na mtoto yule wanapojua wao. Yaani kuwaacha tu kidogo wakapotea, wakapanda mlima na kufikishana kileleni
 
...yaani kuna mambo nitaweza kumtetea anko wangu lakini kuna mambo siwezi kumuwekea dhamana kabisa. Huwa nikikumbuka nasema japo nilikuwa bado yosso asingetumia udhaifu wangu wa kutojua kiingilishi kwenda na mtoto yule wanapojua wao. Yaani kuwaacha tu kidogo wakapotea, wakapanda mlima na kufikishana kileleni
pole mpendwa ndio ukajitahiidi hadi ukajua kiinglishi ili usizidiwe kete tena
 
...yaani kuna mambo nitaweza kumtetea anko wangu lakini kuna mambo siwezi kumuwekea dhamana kabisa. Huwa nikikumbuka nasema japo nilikuwa bado yosso asingetumia udhaifu wangu wa kutojua kiingilishi kwenda na mtoto yule wanapojua wao. Yaani kuwaacha tu kidogo wakapotea, wakapanda mlima na kufikishana kileleni
Si tuliyamalizaaa lakiniiii

Mbona mimi ya Joyce sikukumbushiii au ulikuwa unajua sina moyoo ??
 
Muziki: Fikiria Ajira

Ni jioni tena na ndo tumeshaimaliza siku. Hongera sana uliyemaliza kazi na kazi njema kwa wewe unayeelekea au bado unapiga kazi. kazi ni kazi ila iwe halali tu kwa mujibu wa sheria na kanuni bila kusahau taratibu zinazokubalika na familia.

Nilikuwa na siku nzuri leo, sana na muda wote nilitembea huku natabasamu hasa nikikumbuka kuwa nilitoka home bila kuoga ila nikajikandika mafuta usoni na kujipulizia pafyumu kibao (natumia Lara Wild Cologne) na deodorant ya Speed Stick magic 24. Nikawa natabasamu kama customer care wa Jaza Ujazwe. Safi sana kwenu wote mlioamua kuianza na kuimaliza siku bila kuoga, tupo wengine tunapenda harufu za vikwapa.

Nimesoma humu kuwa kuna nyuzi zimeanzishwa na kutishia uhai wa Makapuku Forum, hivi hizi zinazoanzishwa zina maudhui kama ya MF? na je MF inashindanishwa nazo kwa kipi? MF ni kokoro, kuna kila kitu utapata humu, mafundi wa siasa hadi wapigakura, wapenzi hadi wapenzi wasikilizaji, walimu hadi wanafunzi, maprofesa hadi mapropesa, waheshimiwa hadi watoa heshima. Wote tumo humu na hatushindani na yeyote, wanaweza kudhani wanashindana na MF ila ukweli unabaki kuwa ukweli hauna kutu MF ni zaidi ya thread, ni Jukwaa.

Muziki na utamu wa gitaa ndiyo sasa wakati wake, ndugu Makapuku wenzangu (fikiria kama natoa risala vile) mara nyingi tangu nianze kuleta hii kipengele ya muziki na utamu wa gitaa nimekuwa sijawaangalia sana wanaochipukia kwa kucopy nyimbo ambazo zimetamba. leo ni siku yao na kwa kuwa wako kwenye siku yao basi tuwaheshimu pia.

Kwetu hapa kulikuwa na BSS ambayo mwanzoni ilikuwa poa sana na niilifuatilia vizuri, baadaye ikawa too commercialized kiasi kwamba ikawa ni matangazo mengi kuliko kuwaandaa vijana kuibuka kwenye muziki. Nikahamia TPF hawa walifanya vizuri sana pia.

Leo nitakuonjesha ladha kidogo ya TPF, angalia muziki live ulivyotulia na kama kawaida gitaa linasikika kwa utamu kabisa.
Burudika na kitu cha Tabu Ley Muzinaaaaaaaaaaaaaaaa

Hadi wakati mwingine, nakupenda mdau mwenzangu wa Makapuku. Usisahau ajira uliyonayo na unayoisaka sio tu kwamba inafaida kwako bali ni muhimu kwa maendeleo yetu kama taifa. Zidi kutabasamu hata kama hujaoga.

 
DAWA ASILIA YA KUZUIA KUCHOROPOKA KWA MIMBA ( MISCARRIAGE )

Tunda la Mzambarau : Majani ya Mzambarau ni dawa ya asili inayo saidia kuzuia kutoka kwa mimba.

Tatizo la mimba kuharibika na kutoka (kuchoropoka) kabla ya umri wake unaotakiwa kukamilika, limekuwa likiwasumbua wanawake wengi.
MISCARRIAGE NI NINI ?
Kwa kawaida, ili mtoto azaliwe, ni lazima mwanamke afanye tendo la ndoa akiwa katika siku zake za kupata ujauzito ambapo mimba hutungwa. Baada ya mimba kutungwa, mtoto hukaa tumboni kwa muda wa miezi tisa ambapo hupitia hatua mbalimbali za mabadiliko hadi kuwa binadamu aliyekamilika.
Inapotokea kuwa kitoto kimetoka tumboni kwa namna yoyote ile, kikiwa na umri wa chini ya miezi mitano (wiki ishirini), tatizo hilo huitwa Miscarriage.
Katika hali hii, kitoto kinakuwa hakijakamilika na hakiwezi kujitegemea chenyewe kwa mahitaji muhimu kama kupumua, jambo ambalo husababisha kifo.

NB: Mtoto akitoka akiwa ameshapita umri wa miezi mitano, tatizo hilo huitwa Pre-mature birth (kuzaa njiti).
NINI HUSABABISHA MISCARRIAGE?
Zipo sababu nyingi zinazosababisha ujauzito uchoropoke.

Matatizo ya Vinasaba (Genetic Factors)
Hitilafu katika Kromosomu (Chromosomal abnormalities) ambayo husababisha vinasaba kuwa katika hali isiyo ya kawaida, inatajwa kuwa sababu kubwa zaidi inayosababisha ujauzito uchoropoke ukiwa na umri wa chini ya wiki 13.
Matatizo haya husababisha damu ya mama ishindwe kuendana na ya mtoto na kusababisha reactions ambazo humdhuru mtoto na kumfanya ashindwe kuhimili hali ya tumboni kwa mama. Hivyo ujauzito kuharibika.

2. Upungufu wa Homoni (Progesterone Deficiency)
Homoni ya Progesterone hufanya kazi kubwa kuanzia mimba inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa. Progesterone ndiyo huchochea uimara wa ukuta wa Placenta ambao mtoto hujishikiza. Upungufu wa homoni hii husababisha ukuta wa mji wa mimba kushindwa.

3. Umri Mkubwa
Kwa kawaida, mwanamke anapofikisha umri wa miaka 35 au zaidi, misuli (sphincters) ya mji wake wa uzazi hulegea na kupungua nguvu za kuweza kuhimili na kutunza kiumbe kinachokuwa ndani ya mji wa uzazi. Kulegea kwa misuli hii husababisha mimba kuchoropoka kwa urahisi.

4. Magonjwa
Wanawake wanaosumbuliwa na magonjwa kama kisukari, unene kupindukia (obesity), Polycystic Ovary Syndrome, malaria kali, magonjwa ya zinaa na mengineyo huwa katika hatari kubwa ya mimba zao kutoka.

5. Hitilafu Katika Kizazi
Baadhi ya wanawake huwa na mfuko wa mimba (uterus) ambao muundo wake siyo wa kawaida (T- Shaped Uterus). Wanawake wenye tatizo hili, huwa na hatari kubwa ya mimba zao kuharibika kabla ya kutimiza umri wa miezi tisa.

6. Maambukizi ya bakteria au fangasi
Maambukizi ya bakteria au fangasi husababisha misuli ya kizazi kushambuliwa na kisha kupoteza uwezo wake wa kuhifadhi ujauzito, jambo ambalo husababisha mimba kuchoropoka.

Sababu nyingine ni pamoja matumizi ya pombe kali, uvutaji sigara, matumizi ya dawa za kulevya, kemikali, matatizo ya kurithi n.k

DALILI ZA MIMBA KUCHOROPOKA (Symptoms of a miscarriage):

1. Kutokwa na damu sehemu za siri
Dalili kubwa za miscarriage ni mama mjamzito kutokwa na damu (nzito au nyepesi) sehemu za siri kwa vipindi au mfululizo. Damu hizi hutoka kama zile zitokazo mwanamke anapokuwa kwenye siku zake na huambatana na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu.

2. Maumivu makali ya viungo

Dalili nyingine za mimba inayotaka kuchoropoka ni maumivu makali ya mgongo, kiuno, nyonga na tumbo chini ya kitovu. Maumivu haya huanza taratibu lakini huongezeka kadiri muda unavyozidi kusonga mbele. Pia huambatana na kutokwa na damu kama ilivyoelewa hapo juu.

3. Kutokwa na uchafu sehemu za siri
Dalili nyingine kubwa ya Miscarriage ni mama mjamzito kuanza kutokwa na uchafu wenye rangi sambamba na mabonge ya damu sehemu za siri.

ANGALIZO: Dalili hizi pekee hazitoshi kuashiria kuwa tayari ujauzito umeharibika ila mama mjamzito anapoona moja kati ya dalili hizi au zote, anashauriwa kuwahi hospitali kuonana na daktari haraka iwezekanavyo.

Endapo mama atachelewa, atakuwa anajisababishia matatizo zaidi kwani sumu za kiumbe kilichoharibika huharibu mfuko wa uzazi na kusababisha matatizo makubwa siku za mbeleni ikiwemo ugumba.

TIBA ASILIA KUZUIA TATIZO LA KUCHOROPOKA KWA MIMBA.
Zipo tiba za aina mbalimbali zinazo tibu tatizo la kuzuia kuchoropoka kwa mimba. Miongoni mwa tiba hizo ni hii ifuatayo :
MAHITAJI :
i. Majani ya Mzambarau
ii. Maji safi na salama kiasi cha lita moja.

MATAYARISHO NA MATUMIZI :

Chemsha majani machanga ya mzambarau kwenye lita moja ya maji mpaka yatakapo anza kutoa supu.

MATUMIZI :
Kunywa ujazo wa robo glas 1 mara 2 kwa siku asubuhi na jioni kwa muda wa siku ishirini na moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom