NUKUU YA LEO
I think soon after i became director of the CIA -President Obama pulled me into the oval office and said "Look, i just want you to know that your top priority is to go after Osama Bin laden
Nadhani mara baada ya kuwa mkurugenzi wa CIA, Rais Obama aliinita mimi kwenye ofisi yake ya oval na kuniambia " Nakata ujue kuwa wewe ndie mtu mwenye kipaumbele kikubwa kumfatilia Osama Bin laden.
Haya ni maneno aliyotamka mwanasheria, mwanausalama na mkurugenzi wa zamani wa CIA, Bwana Leon Panetta aliezaliwa mwezi June 28 1938, jijini carlifonia akiwa ni mzaliwa wa wazazi wenye asili ya kiitaliano.
Panetta, baada ya kumaliza chuo kikuu alienda jeshini ya kufanya kazi katika kitengo cha intelijesia ya jeshi kwa miaka 2 kabla ya kutoka jeshini na kujiunga katika ulingo wa siasa.
Uelewa, haiba na ujasiri aliokuwa nao panetta ndio nguzo kubwa za mafanikio yake katika utumishi wa umma kwa muda wote aliofanya kazi ya serikali ya marekani.
Baada ya uteuzi wake mwezi january mwaka 2009, kuliibuka minong,ono mingi juu ya uwezo wake na nafasi aliyopewa ya ukurugenzi wa taasisi nyeti katika usalama wa marekani yaani CIA-Director. Wengi waliaamini utumishi wake wa miaka 2 kama afisa wa intelijensia jeshini usingetosha kuhimili mikikimikiki ya CIA.
Lakini pia ikumbukwe Panetta alikuwa White House Chief of staff, yaani ni msimamizi wa watumishi wa ikulu, mara nyingi anakuwepo kwenye morning breafing ya hali ya usalama kwa rais. Kuwepo katika vikao hivi kuliweza na kulitosha kabisa kumpa uzoefu Panetta , kupitia hivi aliweza kujua siri nyingi na mambo mengi ya kiusalama kuhusu taifa la marekani.
Kama ambavyo Watanzania walipiga kelele baada ya uteuzi wa Dr. Modestus Kapilimba kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa TISS ndivyo wamarekani walivyopiga kelele uteuzi wa Leon Panetta. Dr Kapilimba kafanya kazi sana BOT na idara iliyokuwa inashughulikia vitambulisho vya taifa NIDA bila kujua ni undercover agent wa TISS leo hii yeye ndio Top icon ya Tiss,hii ndio tabia ya jamii ya kijasusi
Turudi kwa Panetta, pamoja na watu kuwa na wasiwasi juu ya uwezo wake tayari Obama alishampa assignment ambayo wengi walipwaya na kufanya vibaya..
Leon Panetta akiwa na Rais Obama
Leon Panetta akiwa na Dianne Fienstein aliyekuwa akipinga uteuzi wake.
Itaendelea.......
Wakati mwingine jongoo hubadilika na kuwa nyoka.