Katika dondoo za bbc ...
[emoji117] Shughuli za kibinadamu ikiwemo ukataji wa miti kiholela nchini Tanzania, wachangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
[emoji117] Uchafu wakithiri nchini DRC, watu kumi na wanne wafa kwa ugonjwa wa kipindupindu
[emoji117] Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aibuka na ushindi wa viti vingi katika bunge la nchi hiyo
[emoji117] Vyombo vya Usalama nchini Mali vinasema vimeokoa zaidi ya wageni thelathini kutoka katika kituo kimoja cha Utalii, kilichokuwa kikishambuliwa na watu waliokuwa na silaha.
[emoji117] Maofisa nchini Nigeria wamearifu kwamba nusu ya chakula cha msaada kilichokuwa kimepelekwa kwa watu waliosambaratishwa kutoka katika makaazi yao na kundi la wana mgambo wa kiislam hakijawafikia walengwa
[emoji117] Nchini Uganda kuna asasi inayotoa ushauri wa masuala ya kisheria bure kwa wananchi na ili kufanikisha zoezi hilo imekuwa ikitekeleza shughuli zake kupitia mitandao ya kijamii.
[emoji117] Ulaji wa samaki unaonekana kupungua maeneo ya pwani ya Kenya kutokana na gharama ya juu ya kitoweo hicho