Shwari mdau!? Nilikabwa na michakato nikashindwa kuchangia kwa wakati, anyway sio ishu sana ilmradi tu humu tunafurahia na kuongezeana maujuzi na maarifa kadha wa kadha na hii ndo spirit ya Makapuku. Huurahooo.
Uliowataja hao kiukweli wanajua kucharaza gitaa na hasa kwenye band. Binafsi nimegusagusa gitaa la kawaida (not an e-one) na sikufanikiwa sana, nilikomea mwanzoni kabisa , aha aha a drop out.
Kwenye kupenda kwangu gitaa ninaweza kusema kina Ngouma, Diblo, na Kimoko hawa wanaitwa ma-lead guitarists kwa kuwa tu utaona wanaweka manjonjo kwenye chorus na vikorombwezo vingine.
Gitaa lengo ni kuleta ladha 'melody' kwenye muziki na kutokana tu na mpangilio basi unamkuta mpiga rhythm anahama na kuweka manjonjo tofauti na mpiga bass ambaye huwa ni mtulivu muda wote.