Makapuku Forum

1 YOHANA 5

14. Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake,ya kuwa tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake,atusikia.

TUOMBE

Asante Baba kwa ulinzi wako mchana kutwa,tunaomba toba kwa mabaya yote tuliyotenda kwa mawazo ,maneno,matendo na kwa kutotimiza wajibu wetu mbalimbali tusamehe twakusihi.

Tunajikabidhi mikononi mwako tulinde tuondoe katika hatari mbalimbali tukumbatie usiku kucha hadi tutakapoamka kesho mfalme wa Amani.

Ponya wagonjwa,fariji wafiwa na wajane ,yatima .
Tunakuomba tuimarishe tukuamini na kukupenda na kuleta mahitaji yetu mbele zako tukiamini kupokea.
Tunakemea nguvu zote za giza,pepo wachafu na tunaenda kinyume na hila zote za shetani,damu ya Yesu itawale.
Asante Baba kwa kutupa mahitaji yetu sawa na mapenzi yako,Roho Mtakatifu mfariji wetu kaa nasi tufundishe kuomba na kutii
Tunaomba na kushukuru Amen


USIKU MWEMA MBARIKIWE
 
Amen
 
Hahahahaha
 
Asante Obe kwa nyuzi za maana ubarikiwe sana
nimefurahia sana wimbo
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…