BlessedHope
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,988
- 32,649
Asante sanaHapana mkuu, JFK hakufariki kesho yake... Alifariki kama nusu saa baada ya kupigwa risasi...
To be more precisely ni kwamba alipigwa risasi saa 12:00 PM November 22 eneo la Dealey Plaza (mbele kidogo ya Jengo la Texas Book Depository ambako inasadikiwa Oswald alikaa)
Alifikishwa hospitali ya Parkland Memorial saa 1:38 PM
Katibu msaidizi wa mawasilino ya Ikulu, Malcolm Kilduff alitangaza kuwa Kennedy amefariki majira ya saa 1:45... Inaaminika kwamba alikuwa amefariki kama saa 1:00 PM ila hakutangazwa muda huo ili makamu wake wa Rais Lyndon aweze kuondoka eneo la hospitali kwa usalama wa wake in case kama ilikuwa ni organized assassination maana yeye ndiye second in power..
Pia swali lako kuhusu nduguye... Naamini unamuongelea Robert (au maarufu Bobby)... Hapana hakufa kesho yake... Kama kumbukumbu yangu iko sawa, alikufa mika mitano baadae (1968)
Nadhani nimejibu swali kwa sehemu..


