Twende sawa mkuu ...

Ukiachia ubora wa Juventus kuanzia eneo la kiungo kurudi nyuma, Bado juve wamekuwa na makosa ya kuruhusu mpira udunde katika eneo lao kabla ya kuondoa......... Bonucci na Chielin ni wazuri sana katika making lakini pia uwezo wao wa kucheza high balls ni mzuri hii ni kutokana na heights waliyonayo.

Pamoja na ubora wa Bonucci na Chielin katika making, Bado watapata ugumu kutokana na Christian Ronaldo na Karimu Benzema wanapenda zaidi kucheza wakitokea pembeni. Ila ugumu hautokuwa kwa Chielin na Bonucci pekee bali hata kwa Ronaldo na Benzema kutokana na aina yao ya uchezaji kupenda kucheza wakitokea pembeni, hii itatoa nafasi kwa beki Juventus kujiandaa na kujipanga vizuri....
Gonzalo Higuan na Paolo Dybala, hawa ni watu wa kuchunga sana kwa beki za Real Madrid..... Aina ya uchezaji wao na kusuasua kwa siku za hivi karibuni, ukiachana na captain Ramos kuwa kayika ubora katika eneo la ulinzi la Madrid, basi shaka kubwa inakuja juu atakayepangwa nae katika mchezo huu eidha Varane, Nacho au Pepe. Pair yeyote inaweza kuanza ila shaka ni namna Madrid alivyoshindwa kutoka Bila nyavu zake kutikiswa katika michezo yake mingi hususani hii ya UEFA champions league.

Miralen Pjanic na Semi Khedira watakuwa wakishindana kwa takwimu tu mwisho mwa mchezo wao na kina Toni Kroos na Luca Mondric........ eneo hili linaweza kuwa bize zaidi katika kujilinda kwa timu zote na kusababisha eneo la ushambuliaji kushuka chini kutafuta mipira.

Dani Alves, Dani Carvajal, Alex Sandro na Marcelo...... Huku pembeni ndipo mpira wote wa fainal utakapokuwa unacheka, ubora wa timu zote hizi mbili upo pembeni kwa mabeki wao wa pembeni ambao wamekuwa ndio mhimili wa kutengeneza nafasi za magoli na matokeo kwa ujumla.

Upande anao cheza Marcelo na Ronaldo ndio upande wenye hatari zaidi kutokana na kasi ya Marcelo na movement za Ronaldo, lakini pia Benzema naye amekuwa akitumia sana upande huo katika zile movement zao za zig zag yeye na Ronaldo...... Juventus wasipokuwa na hesababu makini na upande huu basi huu upande ndio wenye kombe la Madrid katika mchezo huu.

Upande wa Kulia anapocheza Dani Alves na Juan Cuadrado ndio upande wenye hatari zaidi kuliko pande zote za Juventus turin......speed na foot work nzuri ya Juan Cuadrado inaweza kuwa sumu kwa safu ya ulinzi ya Madrid, kwa siku za karibuni combination yake na Dani Alves imeonekana kuwa ndio combination bora na hatari zaidi kwa Juventus.... Real Madrid wanapaswa kuwa makini na upande huu kama wanalitaka kombe na historia mpya.

Marcelo vs Dani Alves ndio Battle inayosubiriwa kwa hamu kubwa pale Cardiff Wales Leo..... Alafu tumalizie na maximilano Allegri dhide ya Zinedine Zidane.

Historia ya UEFA champions league ndio inayoanza kumhukumu kwanza Real Madrid, kabla Juventus hawajaweza kumhukumu.... Na real Madrid wanaanza kupambana na historia na Juventus kwa wakati mmoja....
Yote heri ila tutegemee fainali nzuri sana ...
Mmi juve ananyanyua kwapa ....na hapa mzee wetu yule(Buffon) anahitaji hili kombe kuliko juve wenyewe